Category Archives: #TAFAKARI YA LEO

#TAFAKARI YA LEO; KUPATA UNACHOTAKA…

By | August 21, 2021

Lazima ukifanye kiwe kipaumbele cha kwanza kwako, ukatae kuzuiwa na chochote kile. Safari ya mafanikio huwa ina vikwazo vingi. Kwanza unakutana na ugumu wenye lengo la kukukatisha tamaa, huo tu unatosha kuwaondoa wengi. Ukivuka ugumu huo unakutana na tamaa ya vitu vingine vinavyoonekana ni vizuri zaidi, tamaa inawaondoa wengi pia. (more…)

#TAFAKARI YA LEO; MAWAZO MAZURI NI YA WOTE…

By | August 20, 2021

Kila mawazo mazuri unayoyapata, huwi umeyapata wewe tu, bali wengine pia wanakuwa wameyapata. Unapochelewa kufanyia kazi mawazo mazuri unayoyapaga, unatoa mwanya kwa wengine kuyafanyia kazi na kunufaika nayo zaidi. Usitunze mawazo mazuri kwa ajili ya baadaye, badala yake yafanyie kazi, maana unapochelewa ndiyo unazidi kuyakosa mawazo hayo mazuri. Ukurasa wa (more…)

#TAFAKARI YA LEO; KUJIDANGANYA NI RAHISI…

By | August 19, 2021

Safari ya mafanikio ni ngumu, lakini kujidanganya ni rahisi. Kwa kuwa wengi wanapenda urahisi, hivyo hukimbilia kujidanganya. Kwenye safari yako ya mafanikio, ukweli ni kile unachotaka na uongo ni chochote unachojiambia ambacho ni tofauti na unachotaka. Je wewe unachagua nini, kuwa upande wa ukweli kwa maana ya kupambania unachotaka? Au (more…)

#TAFAKARI YA LEO; GHARAMA YA USHAURI WA BURE…

By | August 18, 2021

Watu wapo tayari kukupa kila aina ya ushauri hata kama hujawaomba. Watakupa ushauri huo bure kabisa na kukuonyesha kwamba ni muhimu kwako. Wengine wataenda mbali zaidi na kukulaumu kama hutafanyia kazi ushauri wao. Lakini kama tunavyojua, hakuna kitu cha bure, ushauri wa bure una gharama kubwa ambayo ni kukutoa kwenye (more…)

#TAFAKARI YA LEO; UPWEKE WA SAFARI YA MAFANIKIO…

By | August 17, 2021

Unapoamua kufanya makubwa na ya tofauti, utajiona kama uko peke yako. Dunia itaonekana kutokujali kabisa na kusubiri uanguke ili ikucheke. Lakini manbo hayako hivyo, kuna wengi sana ambao wako nyuma yako, japo wapo kimya kimya. Watu hao wananufaika na kile unachofanya na pia wanapata matumaini ya wao pia kufanya makubwa. (more…)

#TAFAKARI YA LEO; KUWA MAKINI NA TAARIFA UNAZOPOKEA…

By | August 16, 2021

Uongo na uzushi huwa unasambaa kwa kasi kuliko ukweli. Hiyo ni kwa sababu uongo uba mbwembwe nyingi na unagusa hisia hivyo kusambaa kama moto. Ukweli hauna mbwembwe wala hauchochei hisia. Hivyo kuwa makini sana na taarifa unazopokea, kama huwezi kuzithibitisha kama ni kweli au la, angalia kasi ambayo taarifa hizo (more…)

#TAFAKARI YA LEO; TATIZO NI KIPAUMBELE…

By | August 15, 2021

Kama kuna kitu unafanya na hufanikiwi, ila unaona wengine wanafanya kitu hicho hicho na wanafanikiwa, mnatofautiana kwenye vipaumbele. Wale wanaofanikiwa kwenye kitu hicho wanakuwa wamekipa kipaumbele cha kwanza, kwa sababu wameyafanya maisha yao kukitegemea kitu hicho. Wewe ambaye hufanikiwi kwenye kitu hicho hujakipa kipaumbele cha kwanza, kwa kuwa maisha yako (more…)

#TAFAKARI YA LEO; KUKOSEA NI MWANZO WA KUJIFUNZA…

By | August 14, 2021

Huwa hatupendi kukosea kwa sababu tunachukulia kukosea ni kutokujua na kushindwa. Lakini kukosea ndiyo mwanzo mzuri wa kujifunza. Unapokosea unakuwa na fursa ya kujifunza kipi kinafanya kazi na kipi hakifanyi kisha kuchukua hatua zilizo sahihi. Usiache kufanya maamuzi au kuchukua hatua kwa sababu unaogopa kukosea, kukosea ndiyo mwanzo wa kujifunza, (more…)

#TAFAKARI YA LEO; TATIZO UNAHANGAIKA NA VITU RAHISI…

By | August 13, 2021

Ukisikia tu kuna kitu rahisi na kinakipa sana, mbio unakimbilia kukifanya. Kwa kuwa wengi wanapenda urahisi, mnajikuta wengi mpo kwenye kitu hicho, ushindani unakuwa mkali na wengi hamnufaiki. Mnasikilizia tena wapi ni rahisi, na kupakimbilia. Miaka inaenda unashangaa hupigi hatua kubwa. Unajiona labda una bahati mbaya, lakini tatizo ni moja, (more…)

#TAFAKARI YA LEO; CHANGAMOTO YA MOTISHA…

By | August 12, 2021

Unaweza kutoa motisha kwa nia njema kabisa, ili kuwasukuma watu wafanye kile unachotaka wafanye. Maana binadamu kwa asili ni wavivu na wazembe, bila motosha ni vigumu sana kufanya kitu. Lakini pia binadamu ni wajanja, wanaweza kuuchezea mfumo wowote ule ili waweze kujinufaisha zaidi. Hivyo kama unatoa zawadi, wanatafuta njia ya (more…)