Category Archives: #TAFAKARI YA LEO

#TAFAKARI YA LEO; KABLA JAMBO HALIJAKUSUMBUA…

By | February 21, 2021

Kabla hujaruhusu jambo lolote likusumbue au kukupa wasiwasi, jua kwanza kama lipo ndani au nje ya uwezo wako. Lililo ndani ya uwezo wako ni lile unaloweza kuchukua hatua na ukalibadili na lililo nje ya uwezo wako ni lile ambalo hakuna hatua unaweza kuchukua. Mfano umetoka nyumbani kuna mahali unataka kuwahi, (more…)

#TAFAKARI YA LEO; MUDA HAUKUSUBIRI….

By | February 20, 2021

Dunia haikusubiri wewe mpaka uwe tayari kuanza. Kila siku jua linachomoza na kuzama, miaka inayoyoma na muda wako hapa duniani unazidi kupungua. Wakati unapanga kusubiri au kuahirisha chochote, jikumbushe hili. Unaweza kufa muda wowote, jua hilo na likusaidie kwenye kuyaishi maisha yako ya kila siku, ndivyo alivyosema na kuishi Mstoa (more…)

#TAFAKARI YA LEO; UNATUMA UJUMBE GANI?

By | February 19, 2021

Sisi binadamu tuna uwezo mkubwa wa kumsoma mtu kupitia anachosema, jinsi anavyokisema na kile anachofanya. Hivyo kila unachofanya na kusema, kuna ujumbe unatuma kwa wengine, ambao wanausoma vizuri na kuamua wewe ni mtu wa aina gani. Mtu anapokuhudumia unajua kabisa kama mtu huyo anakujali au la, kama anapenda anachofanya au (more…)

#TAFAKARI YA LEO; KUKOSEA NA KUPATIA…

By | February 18, 2021

Hakuna yeyote anayeweza kukosea mara zote au kupatia mara zote. Kila mmoja wetu kuna mambo anakosea na mengine anapatia. Tunapaswa kuwa wanyenyekevu ili kujua wakati tunapokosea na pia kuweza kujifunza kwa wengine. Kama unadhani wewe unapatia tu na wengine wanakosea tu, hutaweza kujifunza na mara zote utafanya makosa zaidi. Hata (more…)

#TAFAKARI YA LEO; ANZA NA ULICHONACHO…

By | February 17, 2021

Kwa malengo na mipango uliyonayo, hapo ulipo tayari una vitu vingi unavyoweza kuanza kufanya. Lakini wengi huwa hawaanzi, badala yake wanatafuta sababu za kwa nini hawawezi kuanza. Kila mtu huwa anapata kile anachotafuta, anayetafuta sababu za kutokufanya kitu anazipata na anayetafuta mahali pa kuanzia anapapata. Wewe unataka nini, kama ni (more…)

#TAFAKARI YA LEO; MAAMUZI MAKUBWA YANAFANYWA NA WACHACHE…

By | February 16, 2021

Maamuzi yoyote makubwa na muhimu huwa yanafanywa na watu wawili mpaka watatu wenye ushawishi mkubwa na kisha kusukumwa kwa wengine wakubaliane nayo na kuonekana ni maamuzi ya wengi. Ni vigumu kwa watu wengi kufikia maamuzi kwa pamoja kwa sababu kila mtu anakuwa na mtazamo wake ambao unatofautiana na wa wengine. (more…)

#TAFAKARI YA LEO; TATIZO SIYO SABABU…

By | February 15, 2021

Huwa unapanga kufanya kitu, halafu sababu zinaingilia na wewe unaruhusu sababu hizo ziwe kikwazo. Tatizo kubwa zaidi linakuja pale sababu inapokuwa hiyo hiyo kila siku, miaka nenda miaka rudi, sababu ni ile ile. Mfano husomi vitabu kwa sababu huna muda, miezi inakwenda, husomi na sababu ni hiyo hiyo kwamba huna (more…)

#TAFAKARI YA LEO; PESA, MUDA NA NGUVU…

By | February 14, 2021

Pesa ni nyenzo inayokuwezesha kupata muda na nguvu zaidi. Kama kuna kitu unafanya mwenyewe kwa masaa 10 kwa siku, ukitumia pesa unaweza kupata wengine wanaokupa masaa hayo kumi na nguvu zaidi. Wengi wamekuwa wanajisifia kwa kuokoa pesa, kabla hawajaangalia ni kuda na nguvu kiasi gani wanapoteza. Mara zote unaookka pesa, (more…)

#TAFAKARI YA LEO; UPANDE WA PILI WA JAMBO…

By | February 13, 2021

Watu wawili wanapogombana au kutokuelewana, jua kila mmoja amechangia kwa namna fulani pale walipofikia. Japo ukisikiliza upande mmoja mmoja, utasikia kila upande ukilaumu upande mwingine na upande huo kuonekana ni sahihi. Lakini utakuwa umefanya makosa makubwa kama utasikiliza upande mmoja pekee, kwa sababu kila jambo huwa lina pande mbili. Kabla (more…)

#TAFAKARI YA LEO; IKABILI HATARI…

By | February 12, 2021

Matatizo mengi kwenye maisha huwa yanaanza wakiwa madogo kabisa, ambayo kila mtu anaweza kuyatatua. Lakini wengi huwa hawayakabili yakiwa madogo, badala yake wanayaficha au kuyapuuza na hilo linayapa nafasi ya kukua na kuwa hatari zaidi. Wewe usifanye hivyo, kama kuna tatizo au hatari, kabiliana nayo, usiifiche wala kuikimbia. Ukurasa wa (more…)