Category Archives: #TAFAKARI YA LEO

#TAFAKARI YA LEO; UAMINIFU NDIYO USTAARABU…

By | February 11, 2021

Ustaarabu unajengwa kwenye msingi wa uaminifu, pale watu wanapoweka ahadi na kutekeleza ahadi hizo. Uaminifu unapokosekana, watu hawaaminiani na kila mtu anaumia. Unaenda kwa daktari ukiamini atafanya kile chenye manufaa kwako, kadhalika kwa mwalimu, mwanasheria, mhasibu na hata mfanyabiashara. Swali la kujitafakari leo ni je, ahadi gani unawapa watu na (more…)

#TAFAKARI YA LEO; SIYO KINACHOFANYWA, BALI ANAYEKIFANYA…

By | February 10, 2021

Watu hufikiri kuna kazi au biashara ukizifanya mafanikio ni uhakika. Hilo siyo kweli, kwenye kila kazi na biashara, kuna waliofanikiwa na walioshindwa. Kinachowatofautisha watu hao ni sifa zao za ndani. Wale wanaofanikiwa wana sifa za tofauti kabisa na wanaoshindwa. Sifa za mtu zina nguvu na mchango mkubwa mno kwenye mafanikio (more…)

#TAFAKARI YA LEO; KUWA NA MAONI YAKO MWENYEWE…

By | February 9, 2021

Maoni ni kitu rahisi kila mtu kuwa nacho, lakini wengi walio na maoni hawajayatengeneza wao wenyewe, badala yake wamechukua ya wengine. Wachache wanaotengeneza maoni yenye maslahi kwao, huwa wanayasambaza kwa kasi kama propaganda kwa kuwa wanajua wengi ni wavivu wa kujifunza, kuujua ukweli na kuwa na maoni sahihi. Kwa kuwa (more…)

#TAFAKARI YA LEO; HAKUNA ANAYEKUFIKIRIA SANA…

By | February 8, 2021

Hakuna anayekosa usingizi kwa kukufikiria wewe, kila mtu anahangaika kujifikiria mwenyewe. Unafikiria wengine wanafikiri nini kuhusu wewe, kumbe na wao wanafikiria wewe unafikiri nini kuhusu wao. Unaweza kuacha kufanya baadhi ya vitu ili kuwaridhisha wengine kumbe hata hawana muda wa kufuatilia nini umefanya na kwa nini umefanya. Kila mtu ana (more…)

#TAFAKARI YA LEO; GUSA MAISHA YA WENGINE…

By | February 7, 2021

Ni rahisi kusema unatekeleza tu wajibu wako bila kujali nini kinatokea kwa wengine.Ni rahisi kujali maslahi yako bila ya kujali ya wengine. Inashawishi kupambana na hali yako na kuwaacha wengine wapambane na hali zao.Hayo yanaweza kukupa kile unachotaka, yanaweza kukufanya ubaki kwenye kazi yako, lakini hayatakufanya uache alama yoyote.Hakuna anayekumbukwa (more…)

#TAFAKARI YA LEO; FANYA KAMA UNAMSHAURI MWINGINE…

By | February 6, 2021

Inapokuja kwenye matatizo ya wengine, ni rahisi sana kuwashauri, huwa hatukuso chochote cha kuwaambia. Lakini inapokuja kwenye matatizo yetu wenyewe, tunajikuta tumekwama na hatujui nini cha kufanya. Hiyo ni kwa sababu tunakuwa tumeweka hisia zaidi kwenye matatizo yetu na hisia zinapokuwa juu, fikra zinakuwa chini. Unapokuwa kwenye matatizo yoyote yale, (more…)

#TAFAKARI YA LEO; NJIA YA KUZISHINDA MASHINE…

By | February 5, 2021

Mashine ya kwanza ya kushona nguo iliharibiwa vibaya na watu kwa sababu waliamini ni adui kwa ajira zao. Tangu kuanza kwa ugunduzi wa mashine za kurahisisha kazi, watu wamekuwa wanazihofia na kuzipinga, kwa sababu ni adui anayechukua ajira nyingi. Lakini kwa zama hizi hatuwezi tena vita hiyo, mashine zimeshakuwa sehemu (more…)

#TAFAKARI YA LEO; TATIZO LA MBIO ZA PANYA…

By | February 4, 2021

Watu huwa wanajaribu kukuweka kwenye mashindano ya kila aina. Na ndani yetu binadamu, huwa tuna roho ya kupenda kushindana. Ila tatizo kubwa la mashindano hayo ni hata ukishinda, hakuna unachonufaika nacho. Unaweza kubishana na watu na ukawashinda, lakini hutakuwa umewabadili. Unaweza kushindana kibiashara na kuona umeshinda, lakini kiuhalisia hujashinda. Tatizo (more…)

#TAFAKARI YA LEO; ANGALIA MASLAHI YAO…

By | February 3, 2021

Watu wanaweza kufanya vitu ambavyo vinatushangaza, tukashindwa kuelewa kwa nini wamefanya hivyo. Ipo njia rahisi ya kuwaelewa watu kwa yale wanayofanya, ambayo ni kuangalia maslahi yao kwenye kile wanachofanya. Kwa asili sisi binadamu ni wabinafsi, tunatanguliza maslahi yetu mbele kabla ya kingine chochote. Hivyo unapomuona mtu anafanya kitu, hata kama (more…)

#TAFAKARI YA LEO; JE NI UKWELI?

By | February 2, 2021

Hili ni swali la kwanza na muhimu kabisa kujiuliza kwenye jambo lolote lile. Ni rahisi sana kuamini yale ambayo watu wanatuambia hasa wanapoonekana kusema kutoka ndani ya mioyo yao na kwa ushawishi. Tunachosahau ni kwamba kila mtu huwa anadanganya, wapo wanaofanya hivyo kwa kujua, ambao hawa hufanya hivyo kulinda maslahi (more…)