Category Archives: #TAFAKARI YA LEO

#TAFAKARI YA LEO; UWEZO WA KUFIKIRI NDIYO CHANZO CHA MAKUBWA…

By | February 1, 2021

Uwezo wetu wanafamu wa kufikiri, ndiyo chanzo cha maendeleo yote duniani. Kila unachokiona kwa macho yako leo, kilianza kama fikra kwenye akili ya mtu. Na hazikuwa fikra za kawaida, kabla ya vitu hivyo kuwepo, wengi waliamini haviwezekani. Wale waliofikiri vitu hivyo, walionekana kama wamechanganyikiwa au wanaota tu. Lakini hawakukata tamaa, (more…)

#TAFAKARI YA LEO; UONGO NDIYO MSINGI WA MAOVU…

By | January 31, 2021

Kila uovu unaofanyika, huwa unaanzia kwenye uongo. Tena uongo unaanza kidogo, lakini unaendelea kukua ili kulinda uongo wa mwanzo. Lakini pia mtu anapotumia uongo na ukamfanikishia kile anachotaka, anashawishika zaidi kuendelea na uovu mwingine. Wengi huanza na uongo kidogo, wakijiambia hawataendelea hivyo, lakini uongo huo unapowapa wanachotaka, wanajikuta wakiendelea nao (more…)

#TAFAKARI YA LEO; UKWELI UNAHITAJI USHAHIDI…

By | January 30, 2021

Ukweli unahitaji ushahidi halisi, unaoonekana na kuweza kupimika na kila mtu. Ukweli unapaswa kuwa kweli kwa kila mtu na kila mahali. Ukweli ambao mtu analazimishwa kuamini bila ya ushahidi siyo ukweli huo. Kabla ya kukua kwa sayansi, watu waliamini mambo mengi ambayo siyo kweli. Dini na ushirikina viliwaweka watu kwenye (more…)

#TAFAKARI YA LEO; MUDA NI TIBA ISIYOSHINDWA…

By | January 29, 2021

Unaweza kuhangaika na jambo, ukaweka kila aina ya juhudi lakini bado usipate matokeo unayotaka. Hapo unapaswa kuuachia muda ufanye yake, kwa sababu muda ni tiba isiyoshindwa. Baada ya muda mrefu, suluhisho litajitokeza lenyewe au jambo unalohangaika nalo litapotea au kukosa umuhimu. Usijiumize au kukata tamaa pale juhudi unazoweka hazileti matokeo (more…)

#TAFAKARI YA LEO; MATOKEO HAYAHALALISHI NJIA…

By | January 28, 2021

Watu wamekuwa wanatumia njia zisizo sahihi ili tu kupata matokeo wanayoyataka. Wakiamini kilicho muhimu ni matokeo na siyo njia iliyoleta matokeo hayo. Wanaamini matokeo yakiwa mazuri basi njia itakuwa sahihi. Lakini hilo siyo kweli, tumeona wengi wakianguka baada ya kupata matokeo waliyotaka kwa sababu njia walizotumia hazikuwa sahihi. Hakikisha unaanza (more…)

#TAFAKARI YA LEO; WASHA MSHUMAA…

By | January 27, 2021

Kama kuna giza, kitu chenye manufaa unachoweza kufanya ni kuwasha mshumaa. Usihangaike kulaumu au kulaani giza, hilo halitabadili chochote. Lakini kwa kuwasha mshumaa, unaleta mwanga ambao unaliondoa giza. Kuna maeneo mengi yenye giza kwenye maisha yako na ya wengine, angalia ni mshumaa upi unaoweza kuwasha kisha fanya hivyo. Kuwa chanzo (more…)

#TAFAKARI YA LEO; ZIADA, UHABA NA KIASI…

By | January 26, 2021

Ziada ni mbaya, chochote unachofanya au kuwa nacho kwa ziada huwa kinakulevya na kukupa kiburi. Unaona tayari umeshapata kila kitu. Uhaba nao ni mbaya, kwa sababu unachokosa unakihofia na kukuweka kwenye hali ya kutawaliwa na wale wanaoweza kukupatia unachokosa. Mpango mzima ni kuwa na kiasi, kufikia kiasi. Kwa kiasi, huna (more…)

#TAFAKARI YA LEO; FAIDA ISIYO SAHIHI NI HASARA…

By | January 25, 2021

Ipo kauli maarufu kwamba hakuna kipya chini ya jua, tungekuwa tunaielewa kauli hii, tungejiepusha na mengi. Lakini huwa hatuielewi, huwa hatujifunzi kwa historia na hivyo kurudia makosa yale yale. Angalia kwenye utapeli, hakujawahi kuja utapeli mpya kabisa, utapeli wowote ule unatumia uongo au tamaa kuwanasa watu. Hii ina maana kama (more…)

#TAFAKARI YA LEO; KWA NJE NI RAHISI…

By | January 24, 2021

Kitu chochote kile ukikiangalia kwa nje, huwa kinaonekana ni rahisi kufanya na chenye manufaa makubwa. Ni mpaka uingie ndani ndiyo unakua ugumu na changamoto za kitu hicho. Hali hii ya kuona vitu ni rahisi imekuwa kikwazo kwa wengi kupiga hatua kwa sababu unapokutana na ugumu kwenye kile ulichochagua kufanya, ni (more…)

#TAFAKARI YA LEO; FURAHIA UNAPOSHINDWA…

By | January 23, 2021

Unajifunza mengi unaposhindwa kuliko unaposhinda. Kushindwa kunakuonesha ni maeneo yapi una udhaifu, wapi bado hujawa vizuri na hivyo kulazimika kujifunza na kukazana uwe bora zaidi. Kushinda kunakufanya ujione uko vizuri, unajua kila kitu na hilo linapelekea uwe na kiburi kinachokupelekea kuanguka na kushindwa. Mara kwa mara jiweke kwenye mazingira ya (more…)