Category Archives: #TAFAKARI YA LEO

#TAFAKARI YA LEO; UNAPOAHIRISHA JAMBO…

By | January 22, 2021

Jambo lolote unalokuwa umejipangia kufanya halafu ukaliahirisha, maana yake ni kwamba umejiambia una jambo jingine muhimu zaidi la kufanya. Sasa hebu angalia mwenyewe, pale unapoahirisha jambo, ni nini unaenda kufanya? Mara nyingi unajikuta ukifanya mambo ya hovyo na yasiyo na tija kabisa. Badala ya kukamilisha kazi muhimu, unakimbilia kufuatilia habari (more…)

#TAFAKARI YA LEO; KUWA BORA ZAIDI YA JANA…

By | January 21, 2021

Ni rahisi kujipima na kushindana na wengine, lakini unapoingia tu kwenye mashindano hayo, unakuwa umejipoteza. Mtu sahihi wa kushindana naye ni wewe mwenyewe, kila siku kuhakikisha unakuwa bora kuliko ulivyokuwa jana yake. Wewe ndiye unayejijua zaidi, wewe ndiye unajua unataka nini na ndani yako una nini. Kama hujajua hayo, utahangaika (more…)

#TAFAKARI YA LEO; MADHARA YA FIKRA CHANYA.

By | January 20, 2021

Tumeshajifunza sana manufaa ya fikra chanya, namna zinavyotuwezesha kuziona fursa zaidi na kutupa matumaini badala ya kukata tamaa. Lakini kila lenye faida huwa pia lina hasara zake. Fikra chanya pia zina madhara kama haziambatani na matendo chanya. Kuna watu wanakuwa na fikra chanya kweli kweli, lakini hakuna hatua zozote chanya (more…)

#TAFAKARI YA LEO; BADILI MAZINGIRA…

By | January 19, 2021

Kama kuna tabia yoyote unayotaka kubadili kwenye maisha yako, anza kwa kubadili mazingira yako. Mazingira yana nguvu kubwa kwenye kujenga na kuimarisha tabia. Angalia ni mazingira yapi unakuwepo wakati wa tabia husika. Mfano kama unasumbuka na hasira, angalia ni wakati gani huwa unapata zaidi hasira, utagundua kuna vitu ukifanya au (more…)

#TAFAKARI YA LEO; FURAHA SIYO RAHA MUDA WOTE…

By | January 18, 2021

Hadithi za utotoni zilikuwa zinamalizia na baada ya mateso wakaishi kwa raha mustarehe maisha yao yote. Hizo ni hadithi na siyo uhalisia. Hakuna maisha ya raha muda wote, kila wakati kuna ugumu au changamoto unakabiliana nayo na ukivuka inakuja nyingine. Furaha kwenye maisha ni kujua maana ya maisha yako, kujua (more…)

#TAFAKARI YA LEO; HESHIMU UNACHOJIFUNZA NA KUFANYA…

By | January 17, 2021

Kujifunza kitu mara moja haitoshi, unahitaji kurudia rudia. Kufanya kitu mara moja haikufikishi kwenye mafanikio makubwa, unapaswa kufanya mara kwa mara, kwa muda mrefu. Hapo ndipo inapokuja changamoto ya mazoea. Kwa sababu umekuwa unajifunza kitu kwa kurudia, unajiambia tayari unajua. Kwa sababu umekuwa unafanya kila siku, unajikuta ukifanya kwa mazoea. (more…)

#TAFAKARI YA LEO; KIKUTOKACHO KIPO NDANI YAKO…

By | January 16, 2021

Kama mtu amekukasirisha na kisha ukamtukana, tatizo siyo hasira ambayo umekuwa nayo, bali tatizo ni matusi yaliyo ndani yako. Huwezi kutoa kitu ambacho hakipo ndani yako. Kama hujui kuongea lugha ya kichina, hata ukasirishwe kiasi gani, hutaiongea, kwa sababu haipo ndani yako. Kwa mambo yote unayofanya au kusema na baadaye (more…)

#TAFAKARI YA LEO; KUJUA PEKEE HAITOSHI…

By | January 15, 2021

Hautafanikiwa na kuwa na maisha bora kwa sababu unajua vitu vingi. Bali utafanikiwa kwa kuweka kwenye matendo yale unayojua, hata kwa kiwango kidogo tu. Kujifunza kitu mara moja hakutoshi, unapaswa kurudia mara kwa mara mpaka kitu hicho kiwe sehemu yako, kiwe asili kwako. Chagua misingi utakayoendesha nayo maisha yako, iishi (more…)

#TAFAKARI YA LEO; HISIA NI KAMA MOTO…

By | January 14, 2021

Huwezi kufanya chochote bila hisia na huwezi kuwashawishi wengine bila kugusa hisia zao. Hisia ndiyo zinatoa msukumo kwa mtu kuchukua hatua fulani, lakini wengi wamekuwa wanazitumia kwa namna isiyo sahihi. Kwenye ukurasa wa 2205 unajifunza kwa kina namna sahihi ya kutumia hisia zako na za wengine, kwa namna ambayo zitaleta (more…)

#TAFAKARI YA LEO; NATAKA WEWE USHINDE…

By | January 13, 2021

Tunategemeana sana kwenye maisha, hakuna anayeweza kushinda peke yake. Ushindi wa mwalimu ni wanafunzi wanaofaulu, ushindi wa daktari ni wagonjwa wanaopona na ushindi wa mpishi ni watu wanaoshiba na kufurahia chakula. Chochote unachofanya, angalia wale unaowalenga wananufaikaje, wajibu wako ni kuhakikisha wanashinda, maana wakishinda hao, ndiyo na wewe unashinda pia. (more…)