Category Archives: #TAFAKARI YA LEO

#TAFAKARI YA LEO; NAIISHI LEO…

By | January 2, 2021

Wakati pekee ambao nina udhibiti nao ni wakati uliopo. Siku pekee ninayoweza kuitumia kufanya makubwa ni siku hii ya leo. Jana imeshapita, chochote nilochofanya au kushindwa kufanya siwezi kukibadili. Kesho bado haijafika, chochote ninachohofia kuhusu hiyo kesho siwezi kukiathiri. Lakini leo, iko kwenye mikono yangu, ipo ndani ya udhibiti wangu, (more…)

#TAFAKARI YA LEO; MAISHA YANGU NI JUKUMU LANGU…

By | January 1, 2021

Maisha yangu ndiyo jukumu langu kuu hapa duniani. Ndiyo wajibu wangu wa kwanza. Kama maisha yangu hayapo vile ninavyotaka, mimi ndiye wa kuwajibika. Sitamwachia mwingine jukumu hili, maana wengine nao wanapambana na maisha yao. Sitalalamika wala kumlaumu yeyote, badala yake nitachukua hatua sahihi kuyaboresha maisha yangu. Kama kuna jambo halipo (more…)

#TAFAKARI YA LEO; KULIPWA ZAIDI, TOA THAMANI ZAIDI…

By | December 31, 2020

Pesa ni zao la thamani. Kiasi cha pesa unachoingiza sasa ni matokeo ya thamani unayozalisha kwa wengine. Kama unataka kulipwa zaidi ya unavyolipwa sasa, toa thamani kubwa zaidi ya unayotoa sasa. Iwe ni kwenye ajira au biashara, zalisha thamani kubwa zaidi kwa wale wanaotegemea unachofanya. Fanya kwa namna ambayo hakuna (more…)

#TAFAKARI YA LEO; JIWEKEE VIWANGO VYAKO NA PAMBANA NAVYO.

By | December 30, 2020

Simba hata awe na njaa kiasi gani, huwa hawindi panya au wanyama wengine wadogo wadogo. Badala yake anapambana mpaka apate kitoweo sahihi kwake, ambacho ni mnyama mkubwa. Moja ya kikwazo cha mafanikio kwa wengi ni kushindwa kujiwekea viwango vya juu na kupambana kuvifikia. Kama unahangaika na kila kitu, hasa vitu (more…)

#TAFAKARI YA LEO; RAHISI HAINA THAMANI…

By | December 29, 2020

Watu wengi wanahangaika kutafuta njia rahisi na za mkato za kupata mafanikio makubwa. Na hilo huwapeleka kufanya vitu ambavyo ni rahisi na vinavyofanywa na kila mtu. Matokeo yake ni hawafanikiwi, kwa sababu kile kinachofanywa na kila mtu hakithaminiwi. Jamii itakuthamini kama unafanya kitu ambacho inakihitaji sana, lakini hakuna mwingine anaweza (more…)

#TAFAKARI YA LEO; FUATA USHAURI WAKO MWENYEWE…

By | December 28, 2020

Bila shaka umeshatoa ushauri kwa watu wengi kwenye hali mbalimbali wanazopitia. Labda ni mtu alipata msiba na kumpa ushauri kwamba aliyefariki amepumzika pema. Au ni mtu aliyepata hasara au kupoteza kitu na ukamshauri kwamba kwa kuwa bado yuko hai, basi anaweza kupoteza chochote alichopata. Cha kushangaza sasa, wewe ukiwa kwenye (more…)

#TAFAKARI YA LEO; JUKUMU LAKO KUU NI WATU…

By | December 27, 2020

“People are our proper occupation, our job is to do them good and put up with them.” – Marcus Aurelius Jukumu lako kuu kwenye maisha ni watu. Wajibu wako mkubwa ni kuwatendea vyema na kuweza kuendana nao bila ya kujali wakoje. Kila kazi au biashara unayofanya, inawalenga watu. Hivyo unapofanya (more…)

#TAFAKARI YA LEO; INAANZIA NYUMBANI…

By | December 25, 2020

“Virtue and charity start at home. If you have to go some where to display it, then it is not virtue.” – Leo Tolstoy Upendo, wema na msaada ni vitu ambavyo vinaanzia nyumbani. Kama unavifanya vitu hivi nje lakini huwezi kuvifanya nyumbani, siyo vya kweli. Chochote tunachofanya kinapaswa kuanzia nyumbani, (more…)

#TAFAKARI YA LEO; MAANA YA MAISHA NI KUKUA KIROHO…

By | December 24, 2020

“Grow spiritually and help others to do so; it is the meaning of life.” – Leo Tolstoy Maana ya maisha yetu na jukumu kubwa kabisa tulilonalo hapa duniani ni kukua kiroho. Changamoto nyingi tunazokutana nazo kwenye maisha na kutuyumbisha, ni kwa sababu ya uchanga wa kiroho. Unapokua kiroho, unaweza kukabiliana (more…)