Category Archives: #TAFAKARI YA LEO

#TAFAKARI YA LEO; KABLA HUJAWEKA JUHUDI…

By | December 23, 2020

“Speed is only useful if you are running in the right direction” – Joel Barker Kabla hujaweka juhudi kubwa kwenye kile unachofanya, hakikisha kwanza ndiyo kitu sahihi kwako kufanya. Maana kama unachofanya siyo sahihi, juhudi zote unazoweka unazipoteza. Kabla hujaweka kasi kubwa kwenye safari uliyonayo, Hakikisha kwanza uko kwenye uelekeo (more…)

#TAFAKARI YA LEO; MOTO HUMEZA KILA KINACHOWEKWA…

By | December 20, 2020

“What’s thrown on top of the conflagration is absorbed, consumed by it—and makes it burn still higher.” – Marcus Aurelius Moto mkubwa na unaowaka kwa ukali, huwa unageuza kila kinachowekwa kwenye moto huo kuwa nishati na kuwaka zaidi. Moto huo hauogopi chochote unachopokea, badala yake unakipokea na kukigeuza moto unaowaka (more…)

#TAFAKARI YA LEO; KURIDHIKA NA KUYAFURAHIA MAISHA…

By | December 18, 2020

“They who have decided to dedicate their lives to spiritual perfection will never be dissatisfied or unhappy, because, all that they want is in their power.” —Blaise Pascal Kama unataka kuridhika na kuyafurahia maisha yako, Basi jitoe kwa ajili ya ukuaji wa kiroho. Unapojitoa kwa ajili ya ukuaji wa kiroho, (more…)

#TAFAKARI YA LEO; MAANA HALISI YA UJASIRI…

By | December 17, 2020

“Courage is not having the strength to go on: it is going on when you don’t have the strength.” — Theodore Roosevelt Wengi hufikiri ujasiri ni kuwa na nguvu ya kuendelea na mapambano pale mambo yanapokuwa magumu. Lakini ukweli ni ujasiri ni kuweza kuendelea hata pale unapokuwa huna nguvu kabisa. (more…)

#TAFAKARI YA LEO; UKWELI HAUHITAJI KELELE NYINGI…

By | December 15, 2020

“Only misconceptions need to be supported by elaborate arguments. Truth can always stand alone.” – Leo Tolstoy Ukweli hauhitaji kelele nyingi, una nguvu ya kusimama wenyewe. Lakini uongo unahitaji kelele nyingi za kulazimisha ukubalike. Uongo unahitaji maelezo mengi ili kuwashawishi watu waukubali. Na uongo huwa unalazimisha watu waamini, tena bila (more…)

#TAFAKARI YA LEO; HAINA HARAKA LAKINI INAKAMILISHA…

By | December 14, 2020

“Nature does not hurry, yet everything is accomplished.” — Lao Tzu Asili huwa haina haraka, lakini huwa inakamilisha kila kitu. Asili huwa inafanya kila jambo kwa wakati wake na hivyo kukamilisha kila kitu. Lakini sisi na haraka zetu tunaacha mengi ambayo hatujakamilisha. Tuna mengi tunafanya na kuishia njiani. Pamoja na (more…)