Category Archives: #TAFAKARI YA LEO

#TAFAKARI YA LEO; KINACHOKUZUIA USIFAKIWE…

By | August 11, 2021

Ni ujuaji mwingi, kudhani unajua kila kitu na pale unaposhindwa basi unajipa kila aina ya visingizio. Hata pale wengine wanapokuwa wamefanikiwa kwenye kile ulichoshindwa bado hukubali kujifunza kwao, badala yake unawajibia kwa nini wao wamefanikiwa na wewe umeshibdwa. Usiendekeze tabia hiyo ya walioshindwa, kuwa mnyenyekevu na jifunze kwa wale waliopiga (more…)

#TAFAKARI YA LEO; MAISHA HAYASIMAMI…

By | August 10, 2021

Maisha huwa hayasimami, mara zote yanaenda mbele. Na wewe pia hupaswi kusimama, mara zote nenda mbele. Iwe utaruka, kukimbia, kutembea au kutambaa, wewe songa mbele. Hiyo ndiyo njia pekee ya kujisogeza karibu na kile unachotaka. Pambana usonge mbele, kila siku jifunze na fanya kitu kipya ambacho hujawahi kufanya huko nyuma. (more…)

#TAFAKARI YA LEO; UFUJAJI NI KIKWAZO…

By | August 9, 2021

Kutumia hovyo rasilimali ambazo zina uhaba mkubwa ni kikwazo kwako kuweza kupiga hatua na kufanikiwa. Kwa rasilimali hizo muhimu, unahitaji ubahili na ufanisi. Ubahili katika kutumia ili zitoshe na ufanisi katika kutumia ili zilete matokeo makubwa. Rasilimali ulizonazo tayari zinakutosha kupiga hatua kubwa, kama unaona hazitoshi ni kwa sababu huna (more…)

#TAFAKARI YA LEO; IGA HIKI…

By | August 8, 2021

Hufanani na wengine kwa chochote kile, hivyo mengi unayoiga kwao yanakupoteza kwa sababu hayaendani na wewe. Ila kuna kitu kimoja ambacho ukikiiga kwa wengine kinakuwa na manufaa makubwa sana kwako. Kitu hicho ni nidhamu. Kwa kila unayemuona amepiga hatua kuliko wewe, jua ni nidhamu zipi zimemwezesha kupiga hatua hizo, kisha (more…)

#TAFAKARI YA LEO; WABOBEZI WA KUANZA…

By | August 6, 2021

Watu wengi kwenye maisha huwa ni waanzaji wazuri wa mambo, ila huwa hawaendi mbali. Huwa hawana ung’ang’anizi kwenye kile wanachoanza mpaka wafike mwisho wake na kuona matokeo yake. Badala yake huwa wanakimbilia kuacha pale wanapokutana na ugumu au changamoto. Kama unayataka mafanikio makubwa, ondoka mara moja kwenye kundi hilo. Usiwe (more…)

#TAFAKARI YA LEO; RASILIMALI TAYARI UNAZO…

By | August 5, 2021

Hakuna ambaye hana rasilimali muhimu anazohitaji ili kufanikiwa. Kila siku tunakutana na rasilimali ambazo tukizitumia vizuri tutapata matokeo bora sana. Kila magumu, changamoto na majanga unayokutana nayo ni rasilimali. Kila unayekutana naye ni rasilimali. Na kila unachojifunza ni rasilimali. Usijiambie huna rasilimali, bali jiulize umezitumiaje mpaka sasa hizo ambazo tayari (more…)

#TAFAKARI YA LEO; MAJARIBU YANAPIMA MSIMAMO…

By | August 4, 2021

Majaribu huwa yanapima msimamo ambao mtu anao kwenye jambo lolote lile. Ambao hawajawahi kupitia majaribu makubwa kwenye kitu, wanaweza kudhani wana msimamo, kumbe siyo. Huwa tunawashangaa watu kwamba wamebadili msimamo wao, kwamba awali walikuwa na msimamo fulani, ila baada ya kupata fursa fulani wakabadilika. Hao hawakuwa na msimamo, ila tu (more…)

#TAFAKARI YA LEO; USIFANYE MAAMUZI KABLA YA KUONA HIKI…

By | August 3, 2021

Maamuzi mengi unayofanya kwenye maisha yako yanakuwa siyo sahihi kwa sababu unayafanya kwa kuangalia vitu kwa nje pekee. Usiwe mtu wa kufanya maamuzi kabla hujaangalia kitu kwa ndani, maana kwa kufanya hivyo ndiyo unaujua ukweli wenyewe. Kwa kuangalia kwa nje huoni ukweli ambao upo ndani. Kwa nje kila kitu ni (more…)

#TAFAKARI YA LEO; FOKASI NGUVU ZAKO…

By | August 2, 2021

Nguvu ulizonazo sasa tayari zinatosha kufanya makubwa kwenye maisha yako. Lakini namba unavyozitumia ni kikwazo kwako kuweza kufanya makubwa. Hiyo ni kwa sababu umekuwa unazitawanya sana nguvu zako. Unazitawanya kwenye mambo mengi yasiyo na tija kwako. Acha kufanya hivyo kama unataka kufanya makubwa, zikusanye nguvu zako kwenye machache muhimu kwa (more…)