Category Archives: #TAFAKARI YA LEO

#TAFAKARI YA LEO; TUMIA VIZURI KILA UNACHOKUTANA NACHO…

By | July 1, 2021

Kila kitu unachokutana nacho kwenye maisha, ni rasilimali muhimu kwako kufika kule unakotaka kufika. Usikipoteze wala kukitumia vibaya, badala yake kitumie kwa manufaa. Matumizi mazuri ya kitu ni kujiuliza namna ya kukitumia ili kufika kule unakotaka kufika. Matumizi mabaya ya kitu ni kulaumu au kulalamika kwa kukutana nacho. Kila unachokutana (more…)

#TAFAKARI YA LEO; UNAATHIRI WENGINE…

By | June 30, 2021

Kila maamuzi unayofanya kwenye maisha yako huwa yana athari kwenye maisha ya wengine. Hiyo ni kwa sababu sisi binadamu tunategemeana sana kwenye maisha. Na chochote unachotaka kwenye maisha yako wanacho wengine, hivyo unachohitaji ni kuweza kuwapa wanachotaka ili nao wakupe unachotaka. Huwezi kufanikiwa peke yako bila kuhusiana na wengine, hivyo (more…)

#TAFAKARI YA LEO; USIRIDHIKE…

By | June 29, 2021

Adui mkubwa wa mafanikio na maendeleo ni kuridhika na kile ambacho mtu ameshapata. Ugunduzi na hatua zote ambazo tumepiga kama wanadamu, ni kwa sababu watu hawakuridhika na kile walichokuwa nacho, japo kilikuwa bora. Iphone ya kwanza kutengenezwa yalikuwa mapinduzi makubwa mno, kila mtu alipenda namna teknolojia ilivyopiga hatua. Leo kuna (more…)

#TAFAKARI YA LEO; KWA NINI MAFANIKIO SIYO RAHISI?

By | June 28, 2021

Kwa sababu yanahitaji umakini mkubwa ambao wengi hawapo tayari kuuweka. Kwa sababu yanahitaji mtu afuatilie kwa kina kila anachofanya kitu ambacho wengi hawakitaki. Kwa sababu yanahitaji juhudi kubwa ambazo wengi hawapo tayari kuziweka. Na kwa sababu hayataki mazoea, kitu ambacho wengi wanakipenda sana. Huwezi kufanikiwa kwa kufanya vile unavyojisikia kufanya (more…)

#TAFAKARI YA LEO; KUFANYA MAAMUZI SAHIHI KWAKO…

By | June 27, 2021

Ili uweze kufanya maamuzi sahihi kwako, unapaswa kuondoa kila aina ya ushawishi wa watu wengine. Kuna kampeni za makusudi kabisa zinazoendeshwa na wengine ili kukushawishi wewe ufanye maamuzi ya aina fulani. Maamuzi hayo unayoshawishiwa kufanya yanakuwa na manufaa kwa watu wengine. Ili ufanikiwe, lazima uweze kufanya maamuzi yako mwenyewe. Kufanya (more…)

#TAFAKARI YA LEO; UHURU BILA NIDHAMU…

By | June 26, 2021

Uhuru bila ya nidhamu ni sawa na gari bila ya breki, linaweza kukupeleka kasi sana, lakini kasi hiyo itakupoteza kabisa, kwa sababu huna namna ya kulidhibiti gari. Watu wengi wamekuwa wanakimbilia kuwa huru kabla hawajajijengea nidhamu na kinachotokea ni wanapotezwa kabisa na uhuru wanaokuwa wamepata. Wewe pambana kujijengea kwanza nidhamu (more…)

#TAFAKARI YA LEO; HAKUNA KESHO….

By | June 25, 2021

Unapopanga kufanya kitu, chukuli kwamba hakuna kesho na pambana ukifanye kama ulivyopanga. Ni rahisi kujishawishi na kukisogeza mbele kile ulichopanga kufanya, lakini ukisharuhusu hilo, itakuwa vigumu kwako kufanya kitu hicho. Panga na fanya kama ulivyopanga na kama kutakuwa na usumbufu unaokuzuia usifanye, panga kufanya siku hiyo baada ya usumbufu kuisha (more…)

#TAFAKARI YA LEO; UNAHAKIKISHAJE UNAUPATA UKWELI…

By | June 24, 2021

Ukweli mara nyingi huwa unaumiza na wengi wanaokujali hawapo tayari kukuumiza, hivyo wanaweza kuuona ukweli ila wasikuambie. Watu wakishagundua hupendi ukweli unaokuumiza, wanakulisha uongo, ili tu ujisikie vizuri. Lakini uongo huo haukusaidii zaidi ya kukupoteza. Unachohitaji sana ni kuujua ukweli, hata kama unakuumiza, maana huo ndiyo unaokuweka huru. Tafuta watu (more…)

#TAFAKARI YA LEO; KAMA WENGI WANAFANYA, SIYO SAHIHI…

By | June 23, 2021

Ipo kauli ya kiswahili inayosema wengi wape, kauli hiyo ni sahihi kwenye mambo ya kawaida. Inapokuja kwenye mafanikio makubwa, wengi huwa hawapo sahihi. Kwa sababu njia ya kuelekea kwenye mafanikio ni ngumu na yenye vikwazo na changamoto nyingi, wengi huwa wanaikwepa. Hivyo ukikutana na kitu ambacho wengi wanakikubali na kukisifia, (more…)

#TAFAKARI YA LEO; UNAVYOWEZA KUACHA ALAMA HAPA DUNIANI.

By | June 22, 2021

Huhitaji kufanya ugunduzi mkubwa au mapinduzi fulani ndiyo uache alama hapa duniani. Ipo njia rahisi ambayo kila mmoja wetu anaweza kuitumia na akaacha alama kubwa. Njia hiyo ni kujifunza kwa kupata maarifa sahihi, kuyatumia maarifa hayo ili kuyafanya maisha yako kuwa bora kisha kuwafundisha wengine kile unachojia na uzoefu uliopata. (more…)