#TAFAKARI YA LEO; KAMA WEWE YAMEKUSHINDA, UNADHANI WENGINE WATAWEZA?
Wajibu wako wa kwanza kwenye maisha yako ni wewe mwenyewe. Hilo ndiyo jukumu lako kubwa unalopaswa kulipa kipaumbele kikubwa. Kitu chochote ambacho unataka watu wakupe, lazima uanze kujipa wewe mwenyewe. Ukitaka wakupende, jipende. Ukitaka wakukubali, jikubali. Na ukitaka wakuheshimu, jiheshimu. Kama wewe mwenyewe unashindwa kujipa vitu hivyo, unadhani wengine watawezaje (more…)