Category Archives: MAFANIKIO NA HAMASA

SIKU YA 3; Jinsi Ya Kuondo Kabisa Hofu Ya Kushindwa.

By | September 3, 2014

Ili uweze kupata chochote unachotaka kwenye maisha yako ni lazima uweze kuishinda hofu ya kushindwa. Kupata furaha, mapenzi, mafanikio, utajiri, ushawishi, umaarufu na hata chochote unachotaka hatua ya kwanza ni kuishinda hofu ya kushindwa. Hatua ya kwanza ya kushinda hofu ya kushindwa ni kuelewa kwamba kushindwa ni kitu ambacho kinatokea (more…)

TABIA ZA MAFANIKIO; Kujenga Tabia Ya NIDHAMU BINAFSI.

By | September 2, 2014

Mpenzi msomaji wa KISIMA CHA MAARIFA karibu tena kwenye kipengele cha TABIA ZA MAFANIKIO. Katika kipengele hiki kila mwezi tunajadili tabia moja muhimu itakayotuwezesha kufikia mafanikio makubwa. Mwezi wa tano tulijadili tabia ya matumizi mazuri ya muda, mwezi wa sita tukajadili tabia ya kujisomea, mwezi wa saba na wa nane (more…)

SIKU YA 2; Neno Moja Litakaloleta Maajabu Maishani Mwako.

By | September 2, 2014

Kuna neno moja ambalo linaweza kuleta maajabu makubwa sana kwenye maisha yako. Neno hili la maajabu ni siri ya kuwafanya wengine wafanye kile unachotaka. Neno hili la maajabu ni siri ya kupata chochote unachotaka. Neno hili la maajabu linafundishwa katika dini zote na linatumika katika kada zote za elimu, matibabu, (more…)

SIKU YA 1; Nguvu Ya Kujua Ni Nini Unataka Na Utakipataje.

By | September 1, 2014

Karibu sana kwenye SIKU 30 ZA MAFANIKIO MAKUBWA, katika siku hizi 30 utajifunza mambo yote muhimu unayohitaji kujua ili kuweza kufikia mafanikio makubwa kwenye maisha yako. Kumbuka kwamba unaweza kufikia mafanikio makubwa kwenye jambo lolote unalofanya au unalotaka kufanya. Kikubwa ni wewe kujua misingi unayotakiwa kufuata na kisha kuifuata na (more…)

Njia 30 Za Kufikia Mafanikio Makubwa Sana(World Class)

By | August 27, 2014

Kila mmoja wetu anapenda kupata mafanikio kwenye maisha. Tunataka kubobea kwenye kile tunachofanya na pia tunataka kupata fedha nyingi kwa kile tunachofanya. Lakini sio watu wote ambao wanafikia mafanikio makubwa katika mambo wanayofanya. Ni wachache sana wameweza kufikia mafanikio ya ngazi za kimataifa yaani world class. Ni kitu gani kinawafanya (more…)

FEDHA; Usiifanyie Kazi Fedha, Wacha Fedha Ikufanyie Kazi Wewe.

By | August 26, 2014

Kwa miezi miwili, kila wiki tumekuwa tukipata makala moja ya kujifunza jinsi ya kujenga tabia nzuri kwenye matumizi ya fedha. Pia tumejifunza jinsi ya kujenga tabia ya kujiwekea akiba na muhimu zaidi tumejifunza jinsi ya kuwekeza fedha ili kupata thamani zaidi. Kama umefuatilia makala zote hizi kwa makini na kuanza (more…)

Kuwa Tajiri Kwa Kufuata Sheria Hii Moja Rahisi Sana.

By | August 20, 2014

Kila mmoja wetu bila ya kujali kipato chake anaweza kuwa tajiri kama ataweza kufuata sheria hii moja ambayo ni rahisi sana. Japokuwa ukisikia neno kuwa tajiri unaona kama ni kitu ambacho sio kizuri, maisha yako yote unahangaika ili uwe tajiri au ufikie uhuru wa kifedha. Na kwa kuwa umeshachagua kuwa (more…)

FEDHA; Uwekezaji Wa Fedha Zako Kama Umeajiriwa Au Huna Muda Wa Kutosha.

By | August 19, 2014

Wiki iliyopita katika makala hizi za kujenga tabia za mafanikio, tuliona aina za uwekezaji ambazo mtu aliyejiajiri au anayefanya biashara anaweza kuzifanya. Aina hizo ni zile ambazo zinahitaji muda mwingi wa kufuatilia ili kuweza kufikia mafanikio makubwa. Kama hukupata nafasi ya kusoma makala ile isome kwa kubonyeza maneno haya. Leo (more…)

Hiki Ndio Kikwazo Kikubwa Kinachokuzuia Kufikia Mafanikio Makubwa.

By | August 13, 2014

Kila mmoja wetu anapenda kufikia mafanikio makubwa kwenye maisha yake. Na kila mmoja wetu anao uwezo mkubwa sana wa kufanya mambo makubwa zaidi ya anavyofanya sasa. Namaanisha hapo ulipo wewe bila ya kujali ni mambo mangapi umefanikiwa mpaka sasa bado una uwezo wa kufanikiwa zaidi na zaidi. Lakini cha kushangaza (more…)

FEDHA; Uwekezaji Wa Fedha Zako Kama Unafanya Biashara au Umejiajiri.

By | August 12, 2014

Wiki iliyopita katika tabia za mafanikio tulijadili umuhimu wa kuwekeza fedha baada ya kuweka akiba kwa muda fulani. Hii inatokana na thamani ya fedha kushuka haraka sana hivyo bila ya kuwekeza unaweza kujikuta unapoteza fedha kwa kuziweka tu benki au kwingine unakuweka. Leo tutaangalia aina mbalimbali za uwekezaji ambapo mtu (more…)