Category Archives: MAFANIKIO NA HAMASA

KUJISOMEA; Unapata Wapi Muda Wa Kujisomea Na Unapataje Vitabu Vya Kujisomea?

By | June 10, 2014

Habari za leo ndugu msomaji? Naamini unaendelea vizuri na harakati za kuboresha maisha yako. Hata kama huendelei vizuri, muda sio mzrefu mambo yako yatakuwa vizuri. Badili mtazamo wako na acha kujiona mwenye hatia. Wewe ni mshindi, ulizaliwa kuwa mshindi. Usikubali tena kuendelea kuwa mtumwa wa mawazo ya watu wengine. Karibu (more…)

KUJISOMEA; Jinsi Gani Unaweza Kujijengea Tabia Hii Muhimu.

By | June 3, 2014

Mpaka sasa unajua kuna umuhimu mkubwa wa wewe kujijengea tabia ya kujisomea. Na pia unajua kwa kujijengea tabia hii utaweza kuboresha maisha yako kwa kiwango kikubwa sana. Kama bado hujajua haya bonyeza hapa ili kujua umuhimu wa kujijengea tabia hii. Kwa kifupi ni muhimu sana kujijengea tabia ya kujisomea kwani (more…)

TABIA ZA MAFANIKIO; Tabia Ya Kujisomea.

By | June 3, 2014

Mpendwa msomaji na mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA karbu kwenye huu utaratibu wa kujijengea tabia za mafanikio. Katika utaratibu huu kila mwezi tunajadili tabia moja muhimu ili kuweza kufikia malengo tuliyojiwekea na kufanikiwa. Ni ukweli usiopingika kwamba mafanikio hayaji kwa bahati mbaya. Mafanikio yanatengenezwa kidogo kidogo kulingana na tabia za (more…)

Tabia Za Mafanikio; Jijengee Tabia Ya Kujisomea.

By | May 28, 2014

Katika dunia ya sasa hakuna kitu muhimu kama kujisomea na kujifunza mambo mapya kila wakati. Hii ni njia moja ya uhakika ya kuwekeza ndani yako na kujiweka katika nafasi nzuri ya kufanikiwa kwenye kile unachofanya. Kujisomea kunakupatia maarifa, kunakuongezea uwezo wa kufikiri na kunakuwezesha kupambana na changamoto unazokutana nazo kwenye (more…)

Muda; Mambo Muhimu Ya Kuzingati Ili Kuwa Na Matumizi Mazuri Ya Muda Wako.

By | May 27, 2014

Kwenye makala tatu zilizopita tumejifunza mambo mengi sana kuhusu muda, tunavyoupoteza na jinsi ya kupata muda wa ziada. Mpaka sasa unaelewa kwamba muda ni muhimu na adimu sana zaidi hata ya fedha, kwa sababu ukipoteza fedha unaweza kupata nyingine ila ukishapoteza muda ndio umepotea huwezi kuupata tena. Pamoja na umuhimu (more…)

MUDA; Ufanye nini kwenye muda wa ziada uliotengeneza?

By | May 20, 2014

Wiki iliyopita tuliona jinsi ya kuweza kupata masaa mawili ya ziada kila siku. Masaa haya tuliyapata sio kwa miujiza bali kwa kubadilisha vipaumbele vyetu. Mara nyingi unajikuta unafanya mambo ambayo hayana msaada wowote kwako ila ndio umeyapa kipaumbele kikubwa. Katika njia nyingi za kupata muda wa ziada kila siku kuna (more…)

Muda; Pata Masaa Mawili Ya Ziada Kila Siku.

By | May 13, 2014

Kwa wiki nzima kuanzia jumanne iliyopita nilikushauri unakili muda wa kila kitu unachokifanya unapoanza na unapomaliza. Kuna uwezekano umefanya au pia hukufanya. Kama ulifanya hivyo mpaka sasa utakuwa umeona muda wako mwingi unaupotezea wapi. Leo tutaangalia ni jinsi gani unaweza kupata masaa mawili ya ziada kila siku. Ninaposema utapata masaa (more…)

Unaendeleaje Na Zoezi La Kujua Matumizi Ya Muda Wako?

By | May 9, 2014

Wiki hii tuko kwenye zoezi la kujua matumizi ya muda wetu yakoje. Kama tulivyokubaliana ni kwamba tutaandika kwenye karatasi au kijitabu kidogo kila muda tunaotumia kufanya jambo lolote. Yaani utaandika muda ulioanza kufanya na muda ulipomaliza kufanya. Katika wiki hii fanya hivi bila ya kujilazimisha kurekebisha chochote, endelea kuishi maisha (more…)

MUDA; Nusu Ya Muda Wa Maisha Yako Unaipoteza Na Hujui Inapotelea Wapi.

By | May 6, 2014

Karibu sana kwenye kipengele cha TABIA ZA MAFANIKIO ewe msomaji na msafiri mwenzangu katika safari ya mafanikio makubwa sana. Kama nilivyoahidi kila mwezi tutakuwa tukijadili tabia moja ya mafanikio na kuona jinsi gani inatuzuia kufikia mafanikio na njia zipi tunaweza kutumia kuboresha tabia hiyo ili tuweze kufikia mafanikio makubwa. Kila (more…)

Mambo Mapya Na Mazuri Ndani Ya KISIMA CHA MAARIFA; Usikose.

By | May 5, 2014

Kupitia kisima cha maarifa sasa tutaanza kutoa mafunzo ya kubadili au kutengeneza tabia za mafanikio. Kwanzia mwezi wa tano kila mwezi tutakuwa tunaandika kuhusu tabia moja muhimu ya kukufikisha kwenye mafanikio. Kila siku ya jumanne ya kila wiki utapata makala moja kwenye kisima cha maarifa ikielezea umuhimu wa tabia tunayozungumzia (more…)