Category Archives: SHERIA ZA SIKU

#SheriaYaLeo (275/366); Sheria ya msingi ya asili ya binadamu.

By | August 2, 2022

#SheriaYaLeo (275/366); Sheria ya msingi ya asili ya binadamu. Sisi binadamu wote huwa tuna asili ya aina moja. Kwa ujumla sisi binadamu wote ni viumbe wa kihisia, ambao huwa tunafanya maamuzi yetu kwa kusukumwa na hisia. Lakini sheria ya msingi kabisa ya asili ya binadamu imekuwa ni kukataa asili yake. (more…)

#SheriaYaLeo (274/366); Usiende zaidi ya lengo.

By | August 1, 2022

#SheriaYaLeo (274/366); Usiende zaidi ya lengo. Kiini cha mkakati ni kudhibiti kile kinachofuata baada ya kufikia lengo. Maana ushindi huwa una hatari ya kuvuruga kile kinachofuata kwa njia mbili. Moja ni kutaka kurudia kufanya yale uliyofanya ukidhani yatakupa matokeo uliyopata. Unajikuta ukijenga mazoea bila hata kuangalia kama ni mazoea sahihi (more…)

#SheriaYaLeo (273/366); Kuwa tayari kubadilika.

By | July 31, 2022

#SheriaYaLeo (273/366); Kuwa tayari kubadilika. Kila kitu kwenye maisha huwa kinabadilika. Hivyo unapaswa kuchukulia kila kitu kwa kuendana na hali uliyonayo. Maji ndiyo kitu chenye nguvu zaidi duniani, kwa sababu huwa yapo tayari kubadilika. Maji huchukua nafasi kwenye chombo chochote ambacho yanawekwa. Hivyo kuwa tayari kubadilika kama maji ndiyo mkakati (more…)

#SheriaYaLeo (272/366); Pangilia mpaka mwisho.

By | July 30, 2022

#SheriaYaLeo (272/366); Pangilia mpaka mwisho. Hatari nyingi kwenye maisha, ambazo zipo mbele yetu, huwa zinaweza kuepukika kama tukiwa na mipango mizuri mpaka mwisho. Mara nyingi huwa tunachukua hatua ya kutatua tatizo dogo, lakini tunaishia kuzalisha tatizo kubwa zaidi. Kwenye mamlaka, nguvu kubwa ipo kwenye vitu unavyoacha kufanya kuliko vile unavyovifanya. (more…)

#SheriaYaLeo (271/366); Jipe nafasi ya kubadilika.

By | July 29, 2022

#SheriaYaLeo (271/366); Jipe nafasi ya kubadilika. Mradi wowote unaofanya, uwe ni sanaa, kazi au biashara ni sawa na kupigana vita. Lazima uwe na mkakati wa jinsi unavyokabili tatizo, kupangilia kazi yako na kukabiliana na tofauti ya matokeo na mategemeo. Watu wengi huwa wanaanza na wazo zuri, lakini katika kuweka mipango (more…)

#SheriaYaLeo (270/366); Achana na yaliyopita.

By | July 28, 2022

#SheriaYaLeo (270/366); Achana na yaliyopita. Kinachowakwamisha watu wengi ni kushindwa kuukabili uhalisia na kuona vitu jinsi vilivyo. Kadiri tunavyokua kiumri, ndivyo tunavyozidi kufanya vitu kwa mazoea. Tunatawaliwa zaidi na tabia. Kitu ambacho kilitupa matokeo mazuri huko nyuma kinakuwa ndiyo msingi wetu, tunarudia hicho hicho kila wakati. Marudio yanachukua sehemu ya (more…)

#SheriaYaLeo (269/366); Epuka kukaa kwenye kona.

By | July 27, 2022

#SheriaYaLeo (269/366); Epuka kukaa kwenye kona. Kwenye michezo mbalimbali, kukimbilia kukaa kwenye kona ni kujipeleka kwenye kushindwa na hata kufa kabisa. Hali hiyo pia ipo kwenye maeneo mengine ya maisha yetu. Pale unapokabiliana na jambo lolote lile, kukimbilia kwenye kona ni kujipeleka kwenye kushindwa. Kwenye kona kunaweza kuonekana kama ni (more…)

#SheriaYaLeo (268/366); Rudi nyuma kupata mtazamo mpya.

By | July 26, 2022

#SheriaYaLeo (268/366); Rudi nyuma kupata mtazamo mpya. Tatizo kubwa linalotukabili kwenye mikakati na maisha kwa ujumla ni kwamba kila mmoja wetu ni wa kipekee kwa haiba yake. Tunatofautiana sana na hata hali tunazopitia pia zinatofautiana. Changamoto kubwa ni kwamba huwa hatuwezi kujua tofauti walizonazo wengine. Mbaya zaidi ni tunashindwa hata (more…)

#SheriaYaLeo (267/366); Tumia machale yako.

By | July 25, 2022

#SheriaYaLeo (267/366); Tumia machale yako. Mara nyingi sana utahitajika kufanya maamuzi ya haraka kabla hujawa na taarifa za kutosha. Ni kwenye hali za aina hiyo ndiyo unapaswa kuyatumia vizuri machale yako. Kutumia hisia za ndani yako katika kufanya maamuzi sahihi. Kabla ya kutumia machale yako, lazima kwanza uyaendeleze. Na njia (more…)

#SheriaYaLeo (266/366); Wavuruge wasiweze kukusoma.

By | July 24, 2022

#SheriaYaLeo (266/366); Wavuruge wasiweze kukusoma. Nguvu ya maadui zako ipo kwenye uwezo wao wa kukusoma na kujua nia na mipango uliyonayo. Lengo la mikakati yako linapaswa kuwa ni kuwazuia maadui wasiweze kukusoma. Utaweza kukamilisha hilo kwa kuwavuruga maadui zako, kuwafanya wahangaike na mambo yasiyokuwa sahihi. Unachofanya ni kuigiza unafanya kitu (more…)