Category Archives: SHERIA ZA SIKU

#SheriaYaLeo (255/366); Imani ya shujaa.

By | July 13, 2022

#SheriaYaLeo (255/366); Imani ya shujaa. Asili huwa inaweka ukomo kwa kila kiumbe hai, ukomo wa mwisho ukiwa ni kifo. Huwa tuna ukomo kwenye kiasi cha nguvu tunachoweza kutumia kabla hatujachoka. Kadhalika kwenye muda na vipaji, tunavyo ila kwa ukomo mkubwa. Samaki hawezi kuruka angali na wala ndege hawezi kuishi ndani (more…)

#SheriaYaLeo (254/366); Puuza mambo kuyanyima nguvu.

By | July 12, 2022

#SheriaYaLeo (254/366); Puuza mambo kuyanyima nguvu. Jambo lolote lile huwa linakuwa na nguvu kwetu pale tunapolijali na kulipa umakini wetu. Hata watu huwa wanatusumbua kwenye mambo ambayo tunayajali sana. Lakini unapopuuza jambo lolote lile, unalinyima nguvu na hivyo halikusumbui. Hata watu wanapotaka kukusumbua, ukiwapuuza usumbufu wao unakosa nguvu kwako. Kupuuza (more…)

#SheriaYaLeo (253/366); Ona hatari kubwa iliyo mbele yako.

By | July 11, 2022

#SheriaYaLeo (253/366); Ona hatari kubwa iliyo mbele yako. Changamoto kubwa ambayo watu wengi wanayo ni kunasa kwenye wakati uliopo na kushindwa kabisa kupangilia yale yanayokuja. Matokeo yake ni mambo yanakuja kwao kwa mshangao mkubwa, wakiwa hawana maandalizi yoyote, kitu ambacho kinawaathiri sana. Wewe usiwe kama walio wengi, usikubali kuvurugwa na (more…)

#SheriaYaLeo (252/366); Tumia vizuri machafuko.

By | July 10, 2022

#SheriaYaLeo (252/366); Tumia vizuri machafuko. Fikiria akili yako kama jeshi. Jeshi linapaswa kuweza kuendana na ugumu na machafuko yanayoendelea kwa kutumia njia isiyotabirika. Kama ilivyo kwenye vita vya msitumi, adui hatumii mkakati wote mazoea, badala yake kila wakati anakuwa kwenye mwendo. Hali hiyo inafanya kuwa vigumu sana kumshambulia adui huyo. (more…)

#SheriaYaLeo (251/366); Gawa ili kushinda.

By | July 9, 2022

#SheriaYaLeo (251/366); Gawa ili kushinda. Pale tunapokabiliana na kitu chochote kikubwa, iwe ni adui, jukumu au changamoto, huwa tunahofia. Ukubwa wa kile kinachotukabili unatuogopesha kwa kuona hatuwezi kukishinda. Lakini huo siyo ukweli, hakuna chochote kikubwa ambacho hatuwezi kukishinda kama tutatumia njia sahihi. Na moja ya njia bora kabisa ya kushinda (more…)

#SheriaYaLeo (250/366); Usimshambulie adui kwenye uimara wake.

By | July 8, 2022

#SheriaYaLeo (250/366); Usimshambulie adui kwenye uimara wake. Kile ambacho adui anakionyesha wazi wazi ndiyo uimara wake. Ukimshambulia kwenye hicho huwezi kumshinda, bali utamfanya azidi kuwa imara. Njia pekee ya kumshinda adui yeyote yule ni kumshambulia kwenye madhaifu yake. Kila mtu ana madhaifu, ambayo huwa anajaribu kuyaficha. Hivyo chochote anachokionyesha mtu (more…)

#SheriaYaLeo (249/366); Kuwa na machaguo mengi.

By | July 7, 2022

#SheriaYaLeo (249/366); Kuwa na machaguo mengi. Ili kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kupata ushindi kwenye pambano lolote lile, unachohitaji siyo mkakati bora unaofuatwa hatua kwa hatua, bali mkakati wako unapaswa kuwa na machaguo mengi kuliko aliyonayo adui yako. Badala ya kuwa na chaguo moja sahihi ambalo ndiyo unalikumbatia, mkakati bora (more…)

#SheriaYaLeo (248/366); Epuka vita zisizo na manufaa.

By | July 6, 2022

#SheriaYaLeo (248/366); Epuka vita zisizo na manufaa. Siyo kila vita ni ya wewe kupigana. Siyo kila pambano lazima ushinde. Na siyo kila anayekukabili unapaswa kujibizana naye. Wengi wanakutega uingie kwenye mitego yao ili kukuvuruga usiendelee na mikakati yako mikubwa. Wanakuchosha na mapambano yasiyo na tija kitu kinachoondoa nguvu zako kwenye (more…)

#SheriaYaLeo (247/366); Piga kwenye mhimili.

By | July 5, 2022

#SheriaYaLeo (247/366); Piga kwenye mhimili. Ni kawaida ya mamlaka kuonyesha uimara wake kwa lengo la kutisha au kuhadaa wengine. Hakuna mamlaka inayopenda kuonyesha udhaifu wake, japo kila mamlaka ina udhaifu. Kila mamlaka huwa ina mhimili wake, ambapo ndiyo uimara na nguvu za mamlaka hiyo vimejikusanya. Huo ndiyo mhimili ambao unakuwa (more…)

#SheriaYaLeo (246/366); Dhibiti mchezo mzima.

By | July 4, 2022

#SheriaYaLeo (246/366); Dhibiti mchezo mzima. Maisha ni kama mchezo wa drafti. Anayefanikiwa ni yule anayekuwa na udhibiti kwenye mchezo mzima. Kila kete inachezwa kwa kusudi maalumu, ambalo ni kupata ushindi mkubwa baadaye. Hivyo ndivyo maisha yanavyokuwa. Hakun hatua yoyote inayochukuliwa kwa kubahatisha. Badala yake kila hatua inakuwa imepimwa na kupangiliwa (more…)