Category Archives: SHERIA ZA SIKU

#SheriaYaLeo (245/366); Fikiria zaidi ya pale ulipo sasa.

By | July 3, 2022

#SheriaYaLeo (245/366); Fikiria zaidi ya pale ulipo sasa. Kwenye vita, mkakati ni sanaa ya kudhibiti mpango mzima wa kivita. Wakati mbinu ni ujuzi wa kukabiliana na pambano lililo mbele yako. Wengi wetu kwenye maisha ni watu wa mbinu badala ya mikakati. Tunavurugwa na yale yanayoendelea kwa wakati huo kiasi kwamba (more…)

#SheriaYaLeo (244/366); Yatambue maoni yako mwenyewe.

By | July 2, 2022

#SheriaYaLeo (244/366); Yatambue maoni yako mwenyewe. Tambua ya kwamba hata wewe una maoni yako mwenyewe. Tambua jinsi maoni hayo yanafanya kazi ndani yako. Kubali kwamba haupo huru kama unavyodhani. Umekuwa unashawishiwa na wengine kwa namna mbalimbali. Lazima pia utambue ya kwamba siyo mjanja kama unavyojichukulia. Unaweza kulaghaiwa na kushawishiwa kwenye (more…)

#SheriaYaLeo (243/366); Wachukulie kwa mtazamo sahihi.

By | July 1, 2022

#SheriaYaLeo (243/366); Wachukulie kwa mtazamo sahihi. Jinsi unavyowachukulia watu, ndivyo pia wanavyokuwa. Matarajio uliyonayo kwa watu ndiyo matokeo utakayoyapata hata kama hutawaambia moja kwa moja. Tegemea watu watafanya vizuri au kuwa vizuri na hilo ndiyo litatokea. Na kama utategemea watu wafanye vibaya au kuwa wabaya ndivyo watakavyokuwa. Matarajio yetu kwa (more…)

#SheriaYaLeo (242/366); Waambukize hisia sahihi.

By | June 30, 2022

#SheriaYaLeo (242/366); Waambukize hisia sahihi. Sisi binadamu ni viumbe wa kihisia ambapo maamuzi yetu huwa tunayafanya kwa kusukumwa na hisia. Kama unataka kuwashawishi watu, itakuwa rahisi kwako kama utaanza kwa kugusa hisia zao. Na njia rahisi ya kugusa hisia ni kwa kuziambukiza. Anza kwa kuwa na zile hisia ambazo unataka (more…)

#SheriaYaLeo (241/366); Wajengee Kujiamini.

By | June 29, 2022

#SheriaYaLeo (241/366); Wajengee Kujiamini. Unapojaribu kuwashawishi watu kwenye kitu chochote, moja kati ya haya matatu litatokea. Moja unaweza kukosoa na kupinga maoni yao. Kitu ambacho kitawafanya wayalinde na kutatetea maoni yao na hapo watakuwa wagumu kushawishika. Mbili unaweza usiguse kabisa maoni yao, usiyapinge wala kuyaunga mkono, kitu ambacho hakigusi hisia (more…)

#SheriaYaLeo (240/366); Jifunze kusikiliza kwa kina.

By | June 28, 2022

#SheriaYaLeo (240/366); Jifunze kusikiliza kwa kina. Chochote unachofikiria ni ambacho tayari unakijua. Na yale unayojua ni machache mno ukilinganisha na mengi ambayo huyajui. Unapokuwa unazungumza au kufikiria, akili yako ina tabia ya kuzunguka kwenye mambo yale yale ambayo tayari unayajua. Lakini unapokutana na watu wengine, wanakuwa na vitu vya tofauti (more…)

#SheriaYaLeo (239/366); Tumia ndoto kubwa ambazo hawajazifikia.

By | June 27, 2022

#SheriaYaLeo (239/366); Tumia ndoto kubwa ambazo hawajazifikia. Watu wengi huwa wanaamini wana uwezo mkubwa ndani yao kuliko ule unaoonekana kwa nje. Kila mtu ana ndoto kubwa sana ambazo bado hajazifikia. Inaweza kuwa ni mafanikio makubwa wanayotaka kufikia na ngazi za juu zaidi wanazotaka kupanda. Bado wanakuwa hawajafika kule wanakotaka kufika (more…)

#SheriaYaLeo (238/366); Tengeneza jicho la tatu.

By | June 26, 2022

#SheriaYaLeo (238/366); Tengeneza jicho la tatu. Watu wengi huwa wamekwama kwenye wakati uliopo, kwa kuvurugwa na yale yanayoendelea kwenye wakati huo. Wanayafikiria zaidi mambo hayo kitu kinachowapelekea kupata taharuki na kufanya maamuzi ambayo siyo bora sana. Wanashindwa kuona zaidi ya kile kilichopo sasa au mbadala wake. Wachache ambao wanaweza kufikiri (more…)

#SheriaYaLeo (237/366); Changanya ukali na wema.

By | June 25, 2022

#SheriaYaLeo (237/366); Changanya ukali na wema. Unapokuwa kiongozi unahitaji sana kuwa na ushawishi mkubwa kwa wengine ili kuweza kuwaongoza vizuri na kufanya makubwa. Njia bora ya kufanya hivyo ni kuchanganya ukali na wema. Na hilo unalifanya kupitia zawadi na adhabu unazozitoa. Kama kiongozi unapaswa kueleza taratibu za watu wako kufuata. (more…)

#SheriaYaLeo (236/366); Jua na tumia udhaifu wa watu.

By | June 24, 2022

#SheriaYaLeo (236/366); Jua na tumia udhaifu wa watu. Sisi binadamu huwa tuna upinzani. Huwa hatupendi kupangiwa nini tufanye na nini tusifanye. Tunapenda kuona tukifanya maamuzi yetu wenyewe. Huwa tunapinga na kukataa mabadiliko yoyote tunayopendekezewa na wengine. Katika kuwashawishi watu, kukabiliana nao kwenye upinzani wao huwa siyo njia sahihi. Utatumia nguvu (more…)