Category Archives: SHERIA ZA SIKU

#SheriaYaLeo (235/366); Wape ambacho hawajakizoea.

By | June 23, 2022

#SheriaYaLeo (235/366); Wape ambacho hawajakizoea. Ni asili yetu binadamu kupenda kile ambacho hatuna. Huwa tunaona maisha ya wengine ni bora kuliko yetu pale wanapokuwa na vitu ambavyo sisi hatuna. Huwa tunaona kazi au biashara za wengine ni nzuri kuliko zetu. Tunaona maisha yao ni mazuri kuliko yetu. Mara zote tunatamani (more…)

#SheriaYaLeo (234/366); Mhamasishaji mkuu.

By | June 22, 2022

#SheriaYaLeo (234/366); Mhamasishaji mkuu. Watu wengi huwa wanapenda kuhamasisha kwa kutumia maneno. Lakini maneno pekee huwa hayana nguvu ya ushawishi. Na pia huwa yanasahaulika haraka. Kama unataka kuwa na ushawishi mkubwa kwa wengine, kuna mambo mawili muhimu unapaswa kuyazingatia. La kwanza ni kuonyesha kwa vitendo. Watu wanaelewa, kuhamasika na kukumbuka (more…)

#SheriaYaLeo (233/366); Jinsi ya kuwakabili wasumbufu.

By | June 21, 2022

#SheriaYaLeo (233/366); Jinsi ya kuwakabili wasumbufu. Kwenye maisha utakutana na watu wasumbufu. Watu ambao kwa kuwa wana uwezo mkubwa kuliko wengine, huona kama hawahitaji kufuata taratibu wanazozifuata wengine. Watu hao hufanya tofauti na wanavyofanya wengine na wanapoulizwa huomba radhi na kuahidi kufanya kwa usahihi. Lakini bado wakati mwingine hawafanyi kwa (more…)

#SheriaYaLeo (232/366); Wape ushindi kwenye mambo madogo.

By | June 20, 2022

#SheriaYaLeo (232/366); Wape ushindi kwenye mambo madogo. Kama unataka kuwashawishi watu wakubaliane na wewe kwenye jambo kubwa unalotaka, wape kwanza ushindi kwenye mambo madogo. Angalia mambo madogo ambayo hayana athari kwenye lile kubwa unalotaka, kisha kubaliana nao kwenye mambo hayo. Katika kukubaliana nao kwenye mambo hayo madogo unakuwa umewaweka kwenye (more…)

#SheriaYaLeo (231/360); Tumia hisia kueleweka.

By | June 19, 2022

#SheriaYaLeo (231/360); Tumia hisia kueleweka. Unapotumia maneno pekee kuelezea kitu, inakuwa vigumu kueleweka. Na pia unaishia kuibua ubishi ndani ya watu ambao hawatakubaliana na maelezo yako kirahisi. Lakini ukitumia hisia ambazo zinawanasa wengine, wanakuelewa kwa urahisi zaidi bila hata ya kuleta ubishi. Kwa kuwafanya watu wajisikie vile unavyojisikia wewe, unakuwa (more…)

#SheriaYaLeo (230/366); Tumia utani kushawishi.

By | June 18, 2022

#SheriaYaLeo (230/366); Tumia utani kushawishi. Mabishano ni sumu kubwa kwenye ushawishi. Ukishaingia kwenye ubishani unaishia kutengeneza adui na hivyo inakuwa vigumu kumshawishi mtu. Ipo njia bora ya kuwashawishi watu ambayo ni kutumia utani. Pale watu wanapotoa shutuma kuhusu wewe, badala ya kuanza kwa kuwashambulia, unaanza na utani kwanza. Utani huo (more…)

#SheriaYaLeo (229/366); Tumia ubishi wao kuwashawishi.

By | June 17, 2022

#SheriaYaLeo (229/366); Tumia ubishi wao kuwashawishi. Kijana wa mfanyabiashara ya mikopo alienda kwa kiongozi wa dini akilalamika jinsi amejaribu kumshawishi baba yake azingatie misingi ya dini kama kusali lakini baba yake huyo alidai hana muda wa hayo mambo ya dini. Kiongozi huyo wa dini alikuwa anajua tabia za baba wa (more…)

#SheriaYaLeo (228/366); Tumia maigizo na siyo maneno.

By | June 16, 2022

#SheriaYaLeo (228/366); Tumia maigizo na siyo maneno. Kutumia maneno kuwashawishi watu ni jambo hatari sana. Kwani watu huishia kuelewa kinyume na kile ambacho tumemaanisha. Maneno huwa yana nafasi kubwa ya kueleweka vibaya. Lakini pia maneno huwa ni rahisi kuwaumiza watu na kuleta hali ya kutokuelewana. Lakini maigizo huwa yanaeleweka moja (more…)

#SheriaYaLeo (227/366); Waachie watu hisia.

By | June 15, 2022

#SheriaYaLeo (227/366); Waachie watu hisia. Watu wengi huwa wanakazana kutumia maneno kuwashawishi watu. Iwe ni kupitia mazungumzo au maandiko. Wanasema mengi wakiamini baadhi yatakuwa na ushawishi kwa watu hao. Lakini maneno matupu huwa hayana ushawishi mkubwa. Badala yake yanawaacha watu wakiwa na wasiwasi. Kwa sababu watu wanaweza kuondoka na maana (more…)

#SheriaYaLeo (226/366); Penyeza kwenye akili zao.

By | June 14, 2022

#SheriaYaLeo (226/366); Penyeza kwenye akili zao. Ili uweze kuwa na ushawishi kwa watu, lazima kwanza uweze kupenyeza kwenye akili zao. Mara nyingi watu ambao wana madaraka makubwa huwa hawapo tayari kusikiliza ushauri, hasa wa walio chini yao. Huku wale wasio na madaraka wakiona hawahitaji ushauri huo. Ili kuvuka ukinzani huo, (more…)