Category Archives: SHERIA ZA SIKU

#SheriaYaLeo (306/366); Tumaini kwa ajili yetu wote.

By | September 2, 2022

#SheriaYaLeo (306/366); Tumaini kwa ajili yetu wote. Tumeshaona jinsi ambavyo sisi binadamu ni viumbe wa kihisia. Huwa tunafanya maamuzi yetu kwa kusukumwa na hisia badala ya mantiki. Na hilo ndiyo limekuwa chanzo cha matatizo ambayo tumekuwa tunakutana nayo kwenye maisha. Lakini pamoja na hayo, bado lipo tumaini kwa ajili yetu (more…)

#SheriaYaLeo (305/366); Wewe ndiyo kikwazo kwako.

By | September 1, 2022

#SheriaYaLeo (305/366); Wewe ndiyo kikwazo kwako. Maisha ni vita na mapambano, kila wakati unajikuta ukikabiliana na hali mbaya, mahusiano mabovu na mashirikiano hatari. Jinsi unavyokabiliana na hali hizo ndiyo itaamua hatima yako. Kama utajiona umepotea, kama utapoteza mwelekeo, kama huwezi kutofautisha rafiki na adui, unapaswa kujilaumu mwenyewe. Kila kitu kwenye (more…)

#SheriaYaLeo (304/366); Asili ya binadamu haibadiliki.

By | August 31, 2022

#SheriaYaLeo (304/366); Asili ya binadamu haibadiliki. Dunia inaendelea kupiga hatua. Maendeleo ya sayansi na teknolojia yanaleta ufahamu kwenye mambo mengi ambayo huko nyuma hayakujulikana. Kwa sababu hiyo tunaweza kudhani pia kwamba binadamu nao wanabadilika. Lakini ukweli ni kwamba asili ya binadamu huwa haibadiliki. Bado watu wanafanya maamuzi kwa hisia badala (more…)

#SheriaYaLeo (302/366); Sogelea unachokionea wivu.

By | August 29, 2022

#SheriaYaLeo (302/366);Sogelea unachokionea wivu. Watu huwa wana tabia ya kuficha matatizo yao na kuonyesha nyuso zenye furaha. Tunachoona na kusikia kwa watu ni habari njema na ushindi. Hilo huwa linajenga hali ya wivu kwetu, kwa kuona wengine wapo pazuri kuliko pale tulipo sisi. Lakini kama tutawasogelea karibu hao tunaowaonea wivu, (more…)

#SheriaYaLeo (301/366); Ona kivuli chako.

By | August 28, 2022

#SheriaYaLeo (301/366); Ona kivuli chako. Kila mtu huwa ana pande mbili. Upande mzuri ambao ndiyo anauonyesha kwa wengine. Na upande mbaya ambao anauficha. Wengi wakiwa hadharani hufanya mambo mazuri na ya kupendeza. Lakini wakiwa faraghani hufanya mambo mabaya na yasiyo ya kupendeza. Na mara nyingi, wale wanaojionyesha ni wema sana (more…)

#SheriaYaLeo (300/366); Kataa maelezo rahisi.

By | August 27, 2022

#SheriaYaLeo (300/366); Kataa maelezo rahisi. Sisi binadamu huwa tuna ukomo fulani kwenye uwezo wetu wa kufikiri ambao ndiyo chanzo cha matatizo mengi tunayokutana nayo. Tunapofikiria kuhusu watu au kitu ambacho kimetokea, huwa tunakimbilia kwenye maelezo rahisi kwetu kuelewa. Huwa tunakimbilia kwenye kuangalia kama mtu au kitu ni kizuri au kibaya, (more…)

#SheriaYaLeo (299/366); Chunguza mizizi ya hisia zako.

By | August 26, 2022

#SheriaYaLeo (299/366); Chunguza mizizi ya hisia zako. Kila hisia unazokuwa nazo, huwa zinakuwa na mizizi yake ambayo huwa haionekani wazi. Ni mpaka uchunguze kwa kina ndiyo utaweza kujua chanzo halisi cha hisia unazokuwa nazo. Kwa mfano umepatwa na hasira, unapaswa kuacha hisia hizo zitulie, kisha kuchunguza nini kimezisababisha. Kama zimesababishwa (more…)

#SheriaYaLeo (298/366); Jua hujui.

By | August 25, 2022

#SheriaYaLeo (298/366); Jua hujui. Huwa tunapenda kuwabeza watu wa zama zilizopita jinsi ambavyo hawakuwa wanajua yale ambayo tunajua sasa. Tunaona kama walikuwa watu wajinga na walioshindwa kujua yale ya msingi. Hebu fikiria ni kwa namna gani watu wa vizazi vijavyo watatushangaa na kutubeza kwa mambo tunayofanya sasa. Kuna mengi tunajua, (more…)

#SheriaYaLeo (297/366); Nafsi iliyopotea.

By | August 24, 2022

#SheriaYaLeo (297/366); Nafsi iliyopotea. Kila mtu huwa ana nafsi yake ambayo ameipoteza. Hilo linatokana na mtu kuchagua kuwa kama vile ambavyo watu wanataka awe na siyo kama anavyosukumwa kuwa kutoka ndani yake. Wajibu wako mkubwa kwenye maisha ni kuondokana na hali ya mgando unayokuwa nayo, vile unavyojiweka ili kuwaridhisha wengine. (more…)

#SheriaYaLeo (296/366); Usipotezwe na vitu visivyo na tija.

By | August 23, 2022

#SheriaYaLeo (296/366); Usipotezwe na vitu visivyo na tija. Kuna wakati unajikuta umezidiwa na majukumu ambayo unapaswa kuyatekeleza. Unajikuta ukiwa na mambo mengi ya kufanya, lakini muda wa kuyafanya unakuwa mdogo. Ni katika wakati huo ndiyo unapata hali ya kuvurugwa, kwa kuona kuna mambo unapoteza au unayakosa kwa sababu umepoteza udhibiti. (more…)