Category Archives: SHERIA ZA SIKU

#SheriaYaLeo (295/366); Tambua msukumo wako wa shari.

By | August 22, 2022

#SheriaYaLeo (295/366); Tambua msukumo wako wa shari. Sisi binadamu tuna asili ya ushari. Na hilo siyo jambo baya mara zote. Maana ni ushari huo ndiyo unaotupa msukumo wa kufanya makubwa na kufanikiwa. Lakini pale ushari huo unaposhindwa kudhibitiwa vizuri, unakuwa chanzo cha machafuko makubwa. Wizi, utapeli, uhasama na vita yote (more…)

#SheriaYaLeo (294/366); Ona zaidi ya wakati uliopo.

By | August 21, 2022

#SheriaYaLeo (294/366); Ona zaidi ya wakati uliopo. Sisi binadamu huwa tuna tabia ya kuishi kwenye wakati uliopo. Hii ni sehemu kubwa ya asili yetu, ambayo tumeipata kutoka kwa wanyama. Mara nyingi huwa tunakimbilia kujibu kile kilicho mbele yetu kwa wakati husika, ambacho kinanasa umakini wetu zaidi. Lakini sisi siyo tu (more…)

#SheriaYaLeo (293/366); Wakubali watu kama walivyo.

By | August 20, 2022

#SheriaYaLeo (293/366); Wakubali watu kama walivyo. Kuchangamana na watu wengine ndiyo moja ya chanzo kikuu cha matatizo ya kihisia, lakini haipaswi kuwa hivyo. Tatizo ni kwamba huwa tunawahukumu watu mara zote, tukitamani wangekuwa tofauti na walivyo. Huwa tunataka kuwabadili watu, tukitaka wafikiri na kufanya kama sisi. Lakini hilo huwa haliwezekani, (more…)

#SheriaYaLeo (292/366); Fikiria kama mwandishi.

By | August 19, 2022

#SheriaYaLeo (292/366); Fikiria kama mwandishi. Waandishi huwa wanachunguza kitu kwa ndani ili kuweza kujua uhalisia wake. Huwa hawachukulii kitu juu juu kama wanavyofanya watu wengine. Kwanza kabisa wanajizuia wasihukumu kitu chochote kile wanachofanya watu, hata kama ni kibaya kiasi gani. Huchukulia kwamba watu wana sababu ya kila wanachofanya, sababu inayoonekana (more…)

#SheriaYaLeo (291/366); Nenda na wakati.

By | August 18, 2022

#SheriaYaLeo (291/366); Nenda na wakati. Huwa tunapenda kwenda na mazoea, kufanya yale ambayo yamekuwa yakifanyika na matokeo yake kutabirika. Kwenda na mazoea ni kutumia mambo yaliyopita kufanya maamuzi kwenye mambo ya sasa, kitu ambacho kinakuwa siyo sahihi. Ili kufanya maamuzi sahihi na kupata matokeo bora, unapaswa kwenda na wakati. Unapaswa (more…)

#SheriaYaLeo (290/366); Pima watu kama wana wivu.

By | August 17, 2022

#SheriaYaLeo (290/366); Pima watu kama wana wivu. Wivu ni moja ya hisia ambazo binadamu huwa tunakuwa nazo. Ni hisia inayochochewa na hali ya mtu kujilinganisha na wengine na kutokupenda pale wengine wanapokuwa wamemzidi. Wivu huweza kumsukuma mtu kufanya mabaya na kuwadhuru wengine kwa kutokupendezwa na namna walivyowazidi. Katika mahusiano na (more…)

#SheriaYaLeo (289/366); Epuka nguvu ya kubadilishwa na kundi.

By | August 16, 2022

#SheriaYaLeo (289/366); Epuka nguvu ya kubadilishwa na kundi. Sisi binadamu ni viumbe wa kijamii, huwa tunapenda sana kuwa ndani ya makundi ya watu wengine. Lakini makundi hayo huwa yana nguvu kubwa ya kutubadili kwa namna tunavyofikiri, kusema na kufanya. Ndani ya kundi tunajikuta tukijilinganisha na wengine na kujali wanatuchukuliaje. Bila (more…)

#SheriaYaLeo (288/366); Kabili upande wako mbaya.

By | August 15, 2022

#SheriaYaLeo (288/366); Kabili upande wako mbaya. Kila mmoja wetu ana upande wake ambao ni mbaya. Kuna tabia fulani na madhaifu ambayo mtu unakuwa nazo ambazo umekuwa unajaribu kuvificha kwa sababu havikubaliki kijamii. Kwa nje umejenga tabia na mwonekano ambao unafanya ukubalike na wengine na kuonekana mtu mzuri. Ule upande wako (more…)

#SheriaYaLeo (287/366); Kubadili matokeo badili mtazamo wako.

By | August 14, 2022

#SheriaYaLeo (287/366); Kubadili matokeo badili mtazamo wako. Jinsi ambavyo unaona na kuchukulia vitu, siyo jinsi ambavyo vilivyo, bali ni jinsi wewe mwenyewe ulivyo, mtazamo ambao unao. Hiyo ndiyo maana unaweza kuwakuta watu wawili wako kwenye eneo moja, wakifanya kitu kinachofanana, mmoja akawa amefanikiwa na mwenye furaha huku mwingine akiwa ameshindwa (more…)

#SheriaYaLeo (286/366); Ona vitu kama vilivyo na siyo kama hisia zako zinavyokusukuma.

By | August 13, 2022

#SheriaYaLeo (286/366); Ona vitu kama vilivyo na siyo kama hisia zako zinavyokusukuma. Unapaswa kujua pale unaposukumwa na hisia katika maamuzi na kujidhibiti ili usilete madhara. Hiyo ni kwa sababu hisia huwa zinatuzuia tusione vitu kama vilivyo. Hofu inakufanya umkuze zaidi adui na kukimbilia kujihami haraka. Hasira zinakufanya ukimbilie kuchukua hatua (more…)