Category Archives: SHERIA ZA SIKU

#SheriaYaLeo (285/366); Jihadhari na wivu.

By | August 12, 2022

#SheriaYaLeo (285/366); Jihadhari na wivu. Katika hisia zote za binadamu, hakuna ambayo ni mbaya na yenye madhara kama wivu. Hisia kwamba wengine wametuzidi kwenye yale ambayo tunayataka sana kama mali, umaarufu na mamlaka. Huwa tunaona tunastahili kupata kwa wingi kama hao wengine, lakini tatizo linakuja kwamba tunakuwa hatuna namna ya (more…)

#SheriaYaLeo (284/366); Fikiri kwa ajili yako mwenyewe.

By | August 11, 2022

#SheriaYaLeo (284/366); Fikiri kwa ajili yako mwenyewe. Sisi binadamu huwa tunapenda sana vitu ambavyo ni rahisi na tumeshavizoea. Tunayapata mawazo yetu kutoka kwa wazazi, shule na jamii inayotuzunguka. Na mitandao ya kijamii imezidisha sana hali hiyo ya kutegemea fikra za wengine. Hivyo ndivyo tunavyoishia kufikiri kuhusu dunia na maisha kwa (more…)

#SheriaYaLeo (283/366); Nguvu ya ushirikiano.

By | August 10, 2022

#SheriaYaLeo (283/366); Nguvu ya ushirikiano. Sisi binadamu huwa tunaathiriwa sana na fikra na hisia za watu ambao tunashirikiana nao. Huwa tunaishia kuwa kama wale ambao tunakaa nao kwa muda mrefu. Wale waliotawaliwa na hisia hasi, wasio na furaha na wenye kisirani huwa wana nguvu kubwa ya kushwishi kwa sababu hisia (more…)

#SheriaYaLeo (282/366); Wazimu wa kundi.

By | August 9, 2022

#SheriaYaLeo (282/366); Wazimu wa kundi. Wewe peke yako, ukiwa na wazo au mpango ambao ni wa kijinga, watu watakutahadharisha mara moja na kukurudisha kwenye uhalisia. Lakini hilo linapokuwa kwenye kundi, kinyume chake hutokea. Hata kama wazo au mpango ni wa kijinga kiasi gani, kama umekubalika na kundi, kila mtu anakubaliana (more…)

#SheriaYaLeo (281/366); Tofauti ya hisia na mantiki.

By | August 8, 2022

#SheriaYaLeo (281/366); Tofauti ya hisia na mantiki. Watu wengi hutumia maneno hisia na mantiki bila kuelewa maana yake halisi. Watu huona wale wasiokubaliana nao kama wanatumia hisia badala ya mantiki. Tunachopaswa kujua ni kwamba sisi binadamu wote ni viumbe wa kihisia. Huwa tunaathiriwa na hisia mbalimbali ambazo zinachochea fikra zinazotufanya (more…)

#SheriaYaLeo (280/366); Ielewe Asili Yako.

By | August 7, 2022

#SheriaYaLeo (280/366); Ielewe Asili Yako. Sisi binadamu tuna mambo mengi. Hatujui mawazo yetu yanatoka wapi. Wala hatujui hisia zetu zinatokea wapi. Lakini tunaweza kuelewa vyanzo vya hayo kama tukiwa na udadisi na kuhoji maswali mengi. Na hayo ndiyo matumaini pekee unayoweza kuwa nayo, kwa sababu ni vigumu kujua pale unapokuwa (more…)

#SheriaYaLeo (279/366); Usiruhusu mafanikio yawe sumu kwako.

By | August 6, 2022

#SheriaYaLeo (279/366); Usiruhusu mafanikio yawe sumu kwako. Sisi binadamu huwa tuna udhaifu ambao upo ndani ya kila mmoja wetu. Udhaifu huo huwa unapelekea tujione na kujichukulia kwa namna ambayo siyo sahihi. Udhaifu huo unatokana na asili yetu ya kupenda kujisifia na kukuza chochote tulichonacho. Huwa tunaona tuna uwezo mkubwa kuliko (more…)

#SheriaYaLeo (278/366); Chambua, chunguza na hoji.

By | August 5, 2022

#SheriaYaLeo (278/366); Chambua, chunguza na hoji. Ili kujenga uwezo mkubwa wa ndani unaoweza kufanya maamuzi sahihi, unapaswa kutafuta njia ya kutawala hisia zako. Hisia huwa zinatuondoa kwenye uwezo wetu mkubwa wa kufikiri. Hisia hizo zinatuteka na kuathiri mtazamo tunaokuwa nao. Tunapokuwa tumetawaliwa na hisia, hatuvioni vitu kama vilivyo kwa uhalisia (more…)

#SheriaYaLeo (277/366); Uwezo Mkubwa Wa Ndani.

By | August 4, 2022

#SheriaYaLeo (277/366); Uwezo Mkubwa Wa Ndani. Kila binadamu huwa ana kitu anachokiabudu. Huwa kuna kitu cha juu ambacho mtu anakijeshimu na kukitukuza zaidi. Kwa baadhi ya watu ni ufahari wao wa ndani. Wengine ni familia zao, dini zao au jamii zao. Wanafalsafa wa kale waliamini na kuabudu uwezo mkubwa ulio (more…)

#SheriaYaLeo (276/366); Hakuna chenye nguvu kuzidi asili ya mwanadamu.

By | August 3, 2022

#SheriaYaLeo (276/366); Hakuna chenye nguvu kuzidi asili ya mwanadamu. Watu wengi hudhani ujuzi wa asili ya binadamu umepitwa na wakati. Huona kwa maendeleo ya teknolojia tuliyonayo, tunepiga hatua kuondoka kwenye asili yetu binadamu na kuwa bora zaidi. Lakini hilo siyo kweli. Pamoja na mabadiliko makubwa ambayo yameendelea kwenye kila eneo (more…)