Category Archives: TABIA ZA MAFANIKIO

FEDHA; Ufanye Nini Na Fedha Zako Baada ya Kuweka Akiba?

By | August 5, 2014

Mpaka sasa tumeshajifunza mengi kwenye tabia za mafanikio na mwezi wa saba na wa nane tunaendelea kujadili jinsi ya kujenga tabia nzuri kwenye matumizi na uhufadhi wa fedha. Kitu kikubwa ambacho mpaka sasa umeshakifanya kama unafuatilia mafunzo haya kwa ukaribu ni kupunguza matumizi yasiyo ya lazima na kuanza kujijengea tabia (more…)

FEDHA; Tabia Kumi Mbaya Kuhusu Fedha Zinazokufanya Uendelee Kuwa Masikini.

By | July 29, 2014

Kila mmoja wetu anapenda kuwa na fedha zitakazomtosheleza mahitaji yake na kuweza kumuondoa kwenye umasikini. Pamoja na kupenda fedha na kuuchukia umasikini bado matendo yako hayaonyehi hivyo. Matendo yako yanakwenda kinyume kabisa na mapenzi au mawazo yako. Matendo yako yanaonesha kwamba hupendi fedha na hutaki kuondoka kwenye umasikini. Ni vipi (more…)

FEDHA; Utaratibu Mzuri Wa Kujiwekea Akiba.

By | July 22, 2014

Hakuna kitu kizuri kwenye maisha yako kama pale ambapo unaweza kudhibiti mzunguko wako wa fedha. Yaani kama unaweza kujua kiasi gani unapata na kinatoka wapi na ni kiasi gani unatumia na unakitumia wapi unakuwa na uhuru, furaha na maisha yako yanakuwa ya uhakika. Hii ndio sababu kubwa iliyofanya tuanze na (more…)

FEDHA; Anza Kujenga Tabia Ya Kujiwekea Akiba.

By | July 15, 2014

Kama umefanya zoezi la wiki iliyopita mpaka sasa utakuwa unajua ni wapi fedha zako zinatoka na muhimu zaidi ni wapi fedha zako zinakwenda. Kama ulikuwa mwaminifu kwenye kuandika vizuri mapato na matumizi yako utakuwa umeanza kupata picha ni kiasi gani cha fedha unapoteza kila siku. Kama hukupata nafasi ya kufanya (more…)

FEDHA; Tatizo Sio Fedha, Tatizo Ni Wewe.

By | July 1, 2014

Karibu sana msomaji kwenye kipengele cha TABIA ZA MAFANIKIO ambapo tunashauriana jinsi ya kujenga tabia za kutusaidia kufikia mafanikio tunayotazamia. Kila mwezi tunajadili tabia moja muhimu ya kufikia mafanikio. Mwezi huu wa saba tunazungumzia fedha, upatikanaji wake na jinsi ya kuzitunza. Kutokana na umuhimu na upana wa somo hili tutajadili (more…)

TABIA ZA MAFANIKIO; Tabia Ya Utunzaji Na Matumizi Mazuri Ya Fedha.

By | June 27, 2014

Kila mwezi ndani ya KISIMA CHA MAARIFA tunajadili tabia moja muhimu ya kujenga ili kuweza kufikia mafanikio makubwa katika maisha. Sehemu kubwa ya mafanikio yetu inatokana na tabia zetu ambazo zinatokana na matendo yetu ambayo ni zao la mawazo yetu. Kupitia sehemu hii ya TABIA ZA MAFANIKIO tunajadili jinsi ya (more…)

KUJISOMEA; Mambo Muhimu Ya Kuzingatia Ili Kujenga Tabia Imara Ya Kujisomea.

By | June 24, 2014

Habari za leo msomaji wa KISIMA CHA MAARIFA, natumaini wewe ni mzima wa afya na unaendelea vizuri na mpango huu wa kutengeneza tabia za mafanikio. Mpaka sasa utakuwa umeshaanza kuwa na utaratibu wa kujisomea kama umefuatilia makala hizi kwa umakini. Leo tutazungumzia mambo muhimu ya kuzingatia ili uweze kujenga tabia (more…)

KUJISOMEA; Jinsi Unavyoweza Kusoma Vitabu Vingi Ndani Ya Muda Mfupi Na Kuelewa Zaidi.

By | June 17, 2014

Mimi huwa nasoma angalau kitabu kimoja kila wiki na wakati mwingine nasoma vitabu viwili au zaidi ndani ya wiki moja. Sitaki kurudia ni faida gani naipata kwenye kusoma vitabu hivi kwa sababu nilishaeleza sana kwenye makala; hivi ndivyo tabia ya kupenda kujisomea ilivyoninufaisha, inawezekana hata kwako pia. Watu wengi huwa (more…)

KUJISOMEA; Unapata Wapi Muda Wa Kujisomea Na Unapataje Vitabu Vya Kujisomea?

By | June 10, 2014

Habari za leo ndugu msomaji? Naamini unaendelea vizuri na harakati za kuboresha maisha yako. Hata kama huendelei vizuri, muda sio mzrefu mambo yako yatakuwa vizuri. Badili mtazamo wako na acha kujiona mwenye hatia. Wewe ni mshindi, ulizaliwa kuwa mshindi. Usikubali tena kuendelea kuwa mtumwa wa mawazo ya watu wengine. Karibu (more…)