Category Archives: #KURASA_KUMI ZA KITABU KILA SIKU

#KURASA_KUMI ZA KITABU LEO; Maswali Chanya Hubadili Mtazamo Wako…

By | October 11, 2017

KITABU; Socrates ’ way : seven master keys to using your mind to the utmost / Ronald Gross. UKURASA; 71 – 80. Maswali tunayojiuliza na hata kuwauliza wengine, yanachangia sana kwenye mtazamo ambao mtu unakuwa nao. Ukijiuliza maswali chanya unajenga mtazamo chanya, kadhalika maswali hasi yanajenga mtazamo hasi. Kwa mfano (more…)

#KURASA_KUMI ZA KITABU LEO; Swali Moja Muhimu Litakalo boresha Mahusiano yako.

By | October 10, 2017

KITABU; Socrates ’ way : seven master keys to using your mind to the utmost / Ronald Gross. UKURASA; 61 – 70. Socrates anatuasa kuuliza maswali bora ili kuweza kupata ukweli wa mambo na hata kujijua sisi wenyewe kwa kina. Watu walioishi falsafa ya Socrates wamekuwa watu wa kuhoji wengine (more…)

#KURASA_KUMI ZA KITABU LEO; Uliza Maswali Makuu.

By | October 9, 2017

KITABU; Socrates’ way : seven master keys to using your mind to tje utmost / Ronald Gross. UKURASA 51 – 60 Socrates alisifika kwa kuwa mtu wa kuhoji. Hakuwa mtu wa kukubali chochote anachoambiwa na kukipokea kama ndiyo kitu kamili. Badala yake alihoji zaidi na zaidi kuhakikisha anaupata ukweli wenyewe. (more…)

#KURASA_KUMI ZA KITABU LEO; Kujua imani yako hasa, jiulize kwa nini mara nyingi.

By | October 8, 2017

KITABU; Socrates ’ way : seven master keys to using your mind to the utmost / Ronald Gross. UKURASA; 37 – 50. Socrates alikuwa akishangaa sana jinsi gani watu hawapendi kufikiri. Alisema watu wengi wanapenda kuamini kile walichopokea na wasikihoji. Pale mtu anapojaribu kuhiji na kuona imani yake inatikiswa, anaacha (more…)

#KURASA_KUMI ZA KITABU LEO; Jijue Wewe Mwenyewe…

By | October 7, 2017

KITABU; Socrates ’ way : seven master keys to using your mind to the utmost / Ronald Gross. UKURASA; 27 – 36. Kupitia mtindo wake wa mijadala, Socrates anatufundisha ya kwamba, zoezi muhimu sana ambalo kila mtu anapaswa kufanya ni kujijua yeye mwenyewe kwanza. Anasema watu wengi hukimbilia kuomba ushauri (more…)

#KURASA_KUMI ZA KITABU LEO; Mtindo wa kufundisha wa Socrates na kwa nini hakuandika kitabu.

By | October 6, 2017

KITABU; Socrates ’ way : seven master keys to using your mind to the utmost / Ronald Gross. Ukurasa; 17 – 26. Pamoja na ushawishi mkubwa ambao Socrates amekuwa nao kwenye falsafa zote duniani, Socrates hakuwahi kuandika kitabu chochote. Hakuna kitabu chochote ambacho kimeandikwa na Socrates. Socrates aliamini kwamba, njia (more…)

#KURASA_KUMI ZA KITABU LEO; SOCRATES; Menta wa mamenta…

By | October 5, 2017

KITABU; Socrates’ way : seven master keys to using your mind to the utmost / Ronald Gross. UKURASA; 6 – 16. Ukiangalia kwa undani falsafa zote za kale, kuanzia Ugiriki mpaka Roma, zina misingi yake kutoka kwa mwanafalsafa Socrates. Socrates anaweza kuchukuliwa kama mwasisi wa misingi mingi ambayo falsafa nyingi (more…)

#KURASA_KUMI ZA KITABU LEO; Ndani yetu tuna kitu kikubwa, tumekamilika na tuna kila tunachohitaji.

By | October 4, 2017

KITABU; Philosophy for life and other dangerous situations : ancient philosophy for modern problems / Jules Evans UKurasa 227 – 236. Falsafa zote na hata imani za kidini, zinaweka mkazo kwenye kitu kimoja, kwamba sisi ni zaidi ya hii miili tunayoiona. Ndani yetu kuna kitu kikubwa sana, ambacho ndiyo kinabeba (more…)

#KURASA_KUMI ZA KITABU LEO; Je kuna kifo kizuri?

By | October 2, 2017

KITABU; Philosophy for life and other dangerous situations : ancient philosophy for modern problems / Jules Evans UKurasa 217 – 226… Wanafalsafa wa kigiriki waliamini kwamba kifo ni zoezi la kiimani. Waliamini maisha yote tunayoishi, ni kujiandaa na zoezi kuu ambalo ni kifo. Socrates alisema falsafa ni kujiandaa na kifo. (more…)

#KURASA_KUMI ZA KITABU LEO; Hakuna jibu moja la maisha mazuri kwa wote.

By | October 1, 2017

KITABU; Philosophy for life and other dangerous situations : ancient philosophy for modern problems / Jules Evans UKurasa; 207 – 216… Kupitia kitabu hicho, tumeona falsafa mbalimbali ambazo kila moja ilikuwa na msingi wa maisha mazuri. Lakini falsafa zote hizi zina chimbuko lake kutoka kwa mwanafalsafa Socrates ambaye aliamini sisi (more…)