Category Archives: UCHAMBUZI VITABU

THINK AND GROW RICH: Hatua Ya Nne Ya Kufikia Utajiri; Maarifa, Uzoefu Na Uchunguzi – 1.

By | February 5, 2015

Tunaendelea na uchambuzi wa kitabu THINK AND GROW RICH kama hukusoma makala za uchambuzi uliopita bonyeza maandishi haya THINK AND GROW RICH. Kuna aina mbili za maarifa, maarifa ya kawaida na maarifa ya kitaalamu. Maarifa ya kawaida hata ungekuwa nayo mengi kiasi gani, hayawezi kukusaidia kufikia utajiri. Haya ni maarifa (more…)

THINK AND GROW RICH; Hatua Ya Tatu Ya Kufikia Utajiri; Kufikia Akili yako ya ndani – 2

By | January 30, 2015

Kwa wewe kuwa tayari kusoma na kujifunza kupitia kitabu hiki ina maana kwamba unahitaji elimu hii muhimu itakayoboresha maisha yako. Na ili uweze kupata elimu hii na iweze kukusaidia ni lazima uwe tayari kuvpokea vile unavyojifunz ana kuvifanyia kazi. Pia ni lazima ufuate maelekezo yote unayojifunza. Ukichagua kufuata baadhi na (more…)

THINK AND GROW RICH; Hatua ya Tatu Ya Kufikia Utajiri; Kufikia akili yako ya ndani – 1

By | January 29, 2015

Akili ya binadamu imegawanyika katika sehemu tatu, kuna akili inayofikiri na kufanya maamuzi (conscious mind), kuna akili isiyofikiri wala kufanya maamuzi ila inapokea kila taarifa inayoingizwa(subconscious mind) na kuna akili ya juu kabisa inayotawala akili hizi(superconscious mind). Akili ya ndani ambayo haifanyi maamuzi ina nguvu kubwa sana ya kuwez akupokea (more…)

THINK AND GROW RICH; Hatua Ya Pili Ya Kuelekea Kwenye Utajiri, IMANI–2.

By | January 23, 2015

Tunaendele ana sehemu ya pili ya uchambuzi huu wa hatua ya pili ya kuelekea kwenye utajiri. Hatua hii ni imani, katika makala iliyopita tumeweza kuona jinsi imani inavyoweza kukuletea mambo makubwa. Huu hapa ndio ukweli kuhusu imani na mafanikio; Mawazo ambayo yamechanganywa na hisia na imani yanatengeneza nguvu ya sumaku (more…)

THINK AND GROW RICH; Hatua Ya Pili Ya Kuelekea Kwenye Utajiri, IMANI – 1

By | January 22, 2015

Imani ndio kiungo kikuu cha akili. Pale imani inapochanganywa na mawazo yenye hamasa, akili inachukua mawazo hayo na kuyafanyia kazi. Kwa njia hii inakuwezesha wewe kufikia kile unachotaka. Hisia za IMANI, UPENDO na MAPENZI ni hisia zenye nguvu kubwa sana kwa binadamu. Hisia hizo tatu zinapochanganywa pamoja, zinamwezesha mtu kuweza (more…)

THINK AND GROW RICH; Hatua Ya Kwanza Ya Kuelekea Kwenye Mafanikio. – 2

By | January 16, 2015

Karibu kwenye sehemu hii ya uchambuzi wa vitabu na sasa tunachambua kitabu THINK AND GROW RICH. Katika sehemu iliyopita ya uchambuzi tuliona hatua sita za kufikia lengo lolote la kifedha au utajiri unaotaka. Naamini umeshatengeneza hatua zile, kama bado tafadhali rudia tena kusoma makala ile na utengeneze maelezo mafupi kwa (more…)

THINK AND GROW RICH; Hatua Ya Kwanza Ya Kuelekea Kwenye Mafanikio. – 1

By | January 15, 2015

Hatua ya kwanza kabisa ya kuelekea kwenye mafanikio ni kuwa na hamu au shauku kubwa sana ya kufanikiwa. Katika hadithi ya Edwin tuliyoona kwenye uchambuzi uliopita, kilichomfanya akamtafute Edson ni hamu yake kubwa ya kutaka kufanikiwa. Hakukubali kurudishwa nyuma na kikwazo chochote. Edwin alikuwa na hamu kubwa sana ya kufanikiwa, (more…)

THINK AND GROW RICH; SURA YA KWANZA

By | January 9, 2015

Mtu aliyetamani kuingia kwenye ubia na Thomas A. Edison. Ni kweli kwamba mawazo ni vitu ambavyo kama vikichanganywa na malengo, uvumilivu na shauku kubwa lazima yatamfikisha mtu kwenye utajiri wa mali. Edwin C Barnes alitamani sana kuingia kwenye ybia naThomas Edison(Thomas Edison alikuwa mwanasayansi na mgunduzi mkubwa sana wa enzi (more…)

THINK AND GROW RICH; SURA YA KWANZA

By | January 9, 2015

Mtu aliyetamani kuingia kwenye ubia na Thomas A. Edison. Ni kweli kwamba mawazo ni vitu ambavyo kama vikichanganywa na malengo, uvumilivu na shauku kubwa lazima yatamfikisha mtu kwenye utajiri wa mali. Edwin C Barnes alitamani sana kuingia kwenye ybia naThomas Edison(Thomas Edison alikuwa mwanasayansi na mgunduzi mkubwa sana wa enzi (more…)

UCHAMBUZI WA KITABU; THINK AND GROW RICH.

By | January 8, 2015

Habari za leo mpenzi msomaji wa KISIMA CHA MAARIFA, karibu kwenye kipengele hiki cha uchambuzi wa vitabu ambapo tunapata nafasi ya kujifunza mambo mazuri yanayopatikana kwenye vitabu mbalimbali. Kwa mwaka jana tulifanikiwa kufanya uchambuzi wa kitabu RICH DAD POOR DAD na uchambuzi wa kitabu THE RICHEST MAN IN BABYLON. Katika (more…)