Category Archives: UCHAMBUZI VITABU

Utangulizi Wa Kitabu Cha Ustoa; A GUIDE TO GOOD LIFE.

By | March 18, 2017

Mambo muhimu niliyojifunza kwenye utangulizi wa kitabu A GUIDE TO GOOD LIFE. Hichi ni kitabu kilichoandikwa na mwandishi na mwanafalsafa Willium ambaye alikuwa akitafiti kuhusu Tamaa. Baada ya kuangalia dini zinasemaje kuhus tamaa, hakupata maarifa ya kutosha, ndipo alipogeukia falsafa na kukutana na falsafa ya ustoa, ambayo imeelezea kwa kina (more…)

UCHAMBUZI WA KITABU; Getting Results The Agile Way (Mbinu Za Kuwa Na Matumizi Mazuri Ya Muda Na Kupata Ufanisi Mkubwa.)

By | June 15, 2016

Kama kuna kitu kimoja ambacho kila mtu anapigania kwenye maisha haya ni kuweza kutumia muda vizuri na kupata matokeo bora, kuwa na ufanisi mkubwa kwenye shughuli mbalimbali. Matumizi mazuri ya muda kwa sasa imekuwa ni changamoto kutokana na kuongezeka kwa mambo yanayohitaji muda wetu huku muda ukibaki ule ule. Kumekuwa (more…)

UCHAMBUZI WA KITABU; FAIL FORWARD (Hatua 15 Za Kufikia Mafanikio Kupitia Kushindwa).

By | May 25, 2016

Ni rahisi sana kuona watu waliofanikiwa na kusema na wewe unataka ufanikiwe kama wao. Lakini unapoianza safari ya mafanikio ndipo unapogundua kuna mengi hukuyajua. Kuna mengi sana ambayo utayashindwa kwenye safari yako hiyo na kama utakuwa hujajiandaa vizuri hutafika mbali. Watu waliofanikiwa hawakufika walipo kwa mara moja tu, bali wamevuka (more…)

UCHAMBUZI WA KITABU; DEEP WORK (Mbinu Za Kufanya Kazi Yenye Maana Kwenye Zama Hizi Za Usumbufu).

By | May 18, 2016

Ukweli ni kwamba tunaishi kwenye zama ambazo kuna usumbufu wa hali ya juu sana. Sasa hivi mtu yeyote anaweza kukusumbua muda wowote anaoamua wewe. Ukuaji wa teknolijia na mtandao na ujio wa mitandao ya kijamii pamoja na simu janja (smartphone) umefanya iwe rahisi sana kusumbuliwa. Tunasumbuliwa kwa simu zisizokuwa muhimu, (more…)

UCHAMBUZI WA KITABU; THE 50TH LAW (Mbinu Za Kuondokana Na Hofu)

By | May 11, 2016

The 50th law ni kitabu kilichoandikwa na mwandishi Robert Green ambapo amefuatilia maisha ya mwanamuziki 50 Cent ambaye ameweza kufanikiwa sana kwenye muziki. Mwandishi alifuatilia kwa makini maisha ya mwanamuziki huyu ambaye amepitia maisha magumu sana lakini bado akaweza kufikia mafanikio makubwa. katika uchambuzi wake, mwandishi aliweza kuona falsafa moja (more…)

UCHAMBUZI WA KITABU; The Essentials Of Business Etiquette. (Tabia Muhimu Za Kuzingatia Kwenye Mahusiano Ya Kibiashara)

By | May 4, 2016

Tabia zetu zina athari kwenye biashara au kazi tunazofanya. Kuna baadhi ya mambo tunaweza kuwa tunafanya na yakawa yanaharibu sana sifa zetu kwenye biashara na hata kazi. Mwandishi na mshauri Barbara Pachter anatushirikisha tabia za kuzingatia kwenye maeneo yetu ya kazi na hata biashara katika kitabu chake The Essentials Of (more…)

UCHAMBUZI WA KITABU; THE SEVEN HABITS OF HIGHLY EFFECTIVE PEOPLE (Tabia Saba Za Watu Wenye Ufanisi Wa Hali Ya Juu).

By | April 20, 2016

Ufanisi ni moja ya vitu vyenye mchango mkubwa sana kwenye maisha ya mafanikio. Ufanisi ndio unawawezesha baadhi ya watu kuweza kufanya mambo makubwa huku wengine wakiishia kushindwa kufikia ndoto za maisha yao. Wale ambao wana ufanisi mkubwa kwenye maisha yao ndio wanaokuwa na maisha ya furaha na yenye mafanikio makubwa. (more…)

UCHAMBUZI WA KITABU; The Longevity Project (Ugunduzi Wa Kushangaza Kuhusu Afya Na Kuishi Miaka Mingi)

By | April 13, 2016

Ukweli ni kwamba kila mmoja wetu anapenda kuwa na maisha ya mafanikio, na maisha yoyote ya mafanikio yanaanza na mtu kuwa na afya bora. Na kitu kingine muhimu sana ni kwamba kila mmoja wetu anapenda kuishi miaka mingi, kila mtu anapenda kuwa na maisha marefu zaidi hapa duniani. Lakini hivyo (more…)

UCHAMBUZI WA KITABU; DIFFICULT CONVERATIONS (Mbinu Za Kujadili Mambo Magumu Na Muhimu Kwako)

By | April 6, 2016

Kuna mazungumzo ambayo ni muhimu sana kwa kila mmoja wetu, ila mazungumzo haya yanakuwa magumu kufanya kutokana na unyeti wake na umuhimu wake pia. Katika hali kama hii watu wengi hushindwa kutoa kile walichonacho mioyoni mwao na hivyo kubaki wanaumia au kuzikosa fursa muhimu kwao. Mazungumzo kati yako na mwenza (more…)

Mambo 54 Ya Kuzingatia Ili Kufanikiwa Kwenye Ajira.

By | March 30, 2016

Pamoja na kwamba nafasi za ajira zimekuwa chache sana kwenye zama hizi, bado kuna tatizo kubwa hata kwa wale ambao wanazipata nafasi hizi za ajira. Maeneo mengi ya kazi yamekuwa na changamoto kubwa sana ambazo zinawazuia watu kuweza kufanya kazi zao kwa furaha na uzalishaji mkubwa. Na changamoto kubwa kwenye (more…)