3225; Raha.

By | October 30, 2023

3225; Raha. Rafiki yangu mpendwa,Raha huwa ina msukumo mkubwa sana kwetu.Mambo mengi tunayoyafanya ni kwa msukumo wa raha.Tunayafanya kwa sababu yanatupa raha. Kufanya mambo kwa sababu ya kupata raha inaweza kuwa kichocheo au kikwazo cha mafanikio yetu. Raha inakuwa kichocheo cha mafanikio pale mchakato mzima wa mafanikio unapokuwa unatupa raha. (more…)

3224; Wakikuonyesha usiwakatalie.

By | October 29, 2023

3224; Wakikuonyesha usiwakatalie. Rafiki yangu mpendwa,Tunawahitaji sana watu kwenye maisha yetu.Na kadiri tunavyokuwa tunawahitaji watu fulani, ndivyo tunavyotamani wangekuwa vile tunavyotaka wawe. Mwanzoni watu huwa wanaweza kudanganya na kuigiza vile tunavyotaka.Na huwa tunahadaika na hilo.Na kufurahi kwa sababu tunaona tumewapata watu sahihi. Lakini uongo na maigizo huwa hayadumu kwa muda (more…)

3223; Jipe dakika tano.

By | October 28, 2023

3223; Jipe dakika tano. Rafiki yangu mpendwa,Huwa ni kawaida kwetu binadamu tunaposikia kitu kipya kwa mara ya kwanza kukikataa na kukipinga kwamba hakifai au hakiwezekani.Lakini mara nyingi hayo huwa ni maamuzi ya haraka ambayo pia siyo sahihi.Unakuwa umefikia hitimisho la haraka kabla hata ya kutafakari kwa kina. Kuepuka hali hiyo (more…)

Karibu kwenye jamii ya tofauti ya Kisima Cha Maarifa.

By | October 27, 2023

⭐️KARIBU KWENYE JAMII YA KISIMA CHA MAARIFA. Habari Rafiki, Napenda kuchukua nafasi hii kukukaribisha kwenye jamii ya tofauti ya KISIMA CHA MAARIFA. Hii ni jamii ya watu walioamua kushika hatamu ya maisha yao na kujenga maisha ya mafanikio makubwa. Kupitia jamii hii, watu wanajifunza kwa kupata maarifa sahihi na kuchukua (more…)

3222; Haya matatu yanakushindaje ukiwa hai?

By | October 27, 2023

3222; Haya matatu yanakushindaje ukiwa hai? Rafiki yangu mpendwa,Kuna mambo mengi unayowajibika nayo kwenye maisha yako.Mambo hayo ni mengi na yote yanakutegemea wewe moja kwa moja bila kujali wingi na ukubwa wake. Katika hayo mengi, kuna mambo matatu ambayo kwa namna yoyote ile hupaswi kukubali yakakushinda.Mambo hayo matatu unapaswa kuyafikia (more…)

3221; Nani anamiliki nani?

By | October 26, 2023

3221; Nani anamiliki nani? Rafiki yangu mpendwa, Huwa kuna utani kwenye mabenki kwamba mtu akiwa anadaiwa bilioni na benki, basi mtu huyo anakuwa anamilikiwa na benki.Lakini mtu akiwa anadaiwa trilioni na benki, mtu huyo anakuwa anaimiliki benki. Hivyo pia ndivyo ilivyo kwa wateja na biashara. Pale mteja mmoja anapokuwa anachangia (more…)

3220; Unayasababisha mwenyewe.

By | October 25, 2023

3220; Unayasababisha mwenyewe. Rafiki yangu mpendwa,Kuna mambo mengi yanayokuvuruga na yanayokuwa kikwazo kwako kupiga hatua kubwa kwenye maisha yako.Unaweza kuona wengine ndiyo wanaosababisha mambo hayo, lakini kiuhalisia, wewe ndiye umekuwa unayasababisha mwenyewe. Kuna nyakati unapatwa na hasira sana kwenye maisha yako, ambazo zinapelekea ufanye maamuzi yasiyokuwa sahihi. Unaweza kuona hasira (more…)

3219; Ubora na Mafanikio makubwa.

By | October 24, 2023

3219; Ubora na Mafanikio makubwa. Rafiki yangu mpendwa,Watu wengi wanayapenda mafanikio makubwa.Lakini wengi hawayapati, siyo kwa sababu hawawezi kuyapata, bali kwa sababu hawajui namna sahihi ya kuyapata. Tunajua umuhimu wa kuweka kazi kwa msimamo na muda mrefu ili kufanikiwa.Na wapo wengi wanaoweka sana kazi na kwa muda mrefu bila kuacha, (more…)

3218; Upotevu mkubwa wa muda.

By | October 23, 2023

3218; Upotevu mkubwa wa muda. Rafiki yangu mpendwa,Kuna muda ambao huwa tunaupoteza tukiwa tunajua kabisa ya kwamba tunapoteza muda.Hapa ni pale ambapo unakuwa unafanya vitu ambavyo havina mchango wa wewe kufika kule unakotaka kufika.Upotevu huu wa muda huwa unaweza kujishtukia na kuacha kupoteza muda. Halafu sasa, kuna muda ambao huwa (more…)

3217; Nyenzo ya juu kabisa.

By | October 22, 2023

3217; Nyenzo ya juu kabisa. Rafiki yangu mpendwa,Kuanza biashara na kuikuza ni vitu viwili tofauti kabisa.Hapo ndipo watu wengi sana wanapokwama kwenye safari zao za kibiashara. Wengi wanapoanza biashara huwa wanakuwa wapo peke yao na hivyo kila kitu kufanya wao.Wanapokuwa wanashindwa kufanya kitu, wanaona ni kitu ambacho hakiwezi kufanyika kibiashara. (more…)