3208; Unajua lakini hufanyi.

By | October 13, 2023

3208; Unajua lakini hufanyi. Rafiki yangu mpendwa, Kwenye ukurasa uliopita wa 3207 tumejifunza umuhimu wa kuchukua hatua ili kuzalisha matokeo tunayotaka badala ya kusubiri matokeo yajizalishe yenyewe. Hilo ni jambo ambalo kila anayetaka mafanikio makubwa analijua, kwamba matokeo makubwa hayatokei tu, bali yanasababishwa. Tukiendelea na mfano wa ukurasa huo, kwenye (more…)

3207; Simu ziite sasa.

By | October 12, 2023

3207; Simu ziite sasa. Rafiki yangu mpendwa,Nimekuwa naona watu wakiweka picha za bidhaa mbalimbali wanazouza kwenye mtandao (wasap status) pamoja na bei zake.Kisha wanaweka maelezo; simu ziite sasa.Nimekuwa nachukulia kauli hiyo kama utani tu na kuona hakuna muuzaji aliye makini anayekuwa anategemea kweli kwamba simu zitaita. Siku moja nilikuwa namfanyia (more…)

3206; Raha ya ukuaji.

By | October 11, 2023

3206; Raha ya ukuaji. Rafiki yangu mpendwa,Viumbe wote hai huwa wana sifa ya ukuaji.Na sisi sote huwa tunafurahia sana ukuaji kwenye viumbe wote hai wanaotuzunguka. Ukiwa na wanyama unaowafuga au mimea uliyopanda, ukuaji ndiyo kitu ambacho unakifuatilia sana.Unakuwa unajua kila hatua ambapo kitu kipo na hatua gani inayofuata kwenye ukuaji. (more…)

3205; Chini ya hapo unatafuta matatizo.

By | October 10, 2023

3205; Chini ya hapo unatafuta matatizo. Rafiki yangu mpendwa,Kwenye kitabu cha ujumbe kwenda kwa Garcia, tumejifunza madaraja matano ya watu.Na tukaona tunahitaji kufanya kazi na watu wa daraja la kwanza ambao wanafanya kitu sahihi bila kuambiwa na daraja la pili ambao wanafanya kitu sahihi baada ya kuambiwa mara moja.Kufanya kazi (more…)

3204; Usimwache akapoa.

By | October 9, 2023

3204; Usimwache akapoa. Rafiki yangu mpendwa,Mara baada ya mteja kununua kwako, nini huwa kinafuata?Kwa walio wengi, mteja anaponunua muuzaji anafurahia hayo mauzo kisha kumshukuru na kumwacha aende zake. Hili ni kosa kubwa ambalo limekuwa linawanyima wauzaji fursa ya kufanya mauzo mengi zaidi.Mara baada ya mteja kununua, huwa anakuwa kwenye moto (more…)

3203; Inachukua muda.

By | October 8, 2023

3203; Inachukua muda. Rafiki yangu mpendwa,Sehemu kubwa ya mambo tunayojifunza kwenye maisha siyo mapya.Bali tunakuwa tunarudia mambo yale yale kwa namna tofauti tofauti. Na hiyo ni kwa sababu sisi binadamu huwa tunazoea na kusahau mambo haraka sana.Tunakuwa tunajua kabisa, lakini kwa mazoea na usahaulifu, tunapotezea na mwishowe tunapata madhara. Kitu (more…)

3202; Asilimia 100.

By | October 7, 2023

3202; Asilimia 100. Rafiki yangu mpendwa,Kuna namna ya kufikiri tuliyonayo ambayo imekuwa ni kikwazo kwetu kuweza kupiga hatua kubwa. Namna hiyo ni kutaka uhakika kwenye kila jambo ndiyo tulifanye.Na siyo tu uhakika, bali uhakika wa asilimia 100.Yaani tunataka kitu kiwe cha uhakika kabisa ndiyo tukifanye. Madhara ya hilo ni pale (more…)

Fadhila Yenye Nguvu Na Mafanikio Makubwa Kwenye Maisha Yako

By | October 6, 2023

Mpendwa mstoa mwenzangu, Sina uhakika kama itakufaa lakini wewe ni mtu mwenye bahati sana na ujasiri mkubwa mpaka hapa ulipofikia. Kwa sababu kuishi ni ujasiri mkubwa mno, mpaka hapa ulipo umeshavuka vikwazo vingi na umevipita. Pata picha changamoto mbalimbali ulizoweza kukabiliana nazo. Ni wangapi walioshindwa kufikia hapo wewe ulipo? Unaona (more…)

3201; Madhara ya kutokusikiliza.

By | October 6, 2023

3201; Madhara ya kutokusikiliza. Rafiki yangu mpendwa,Mtu mmoja amewahi kuandika kwamba unapochagua menta au kocha kwenye maisha yako, unatakiwa umsikilize kile anachokuambia. Hiyo ni kwa sababu lengo la kuwa na menta au kocha ni kupunguza urefu wa safari, kwa kuepuka kurudia makosa ambayo yeye amewahi kufanya au alishajifunza. Lakini huwa (more…)