3200; Kushindwa ni kuacha.

By | October 5, 2023

3200; Kushindwa ni kuacha. Rafiki yangu mpendwa,Karibu kila mtu kwenye maisha anataka kupata mafanikio makubwa. Lakini kwenye uhalisia ni wachache sana ambao wamefanikiwa.Wengi sana wameshindwa. Na unapoangalia kwa karibu wale walioshindwa,Unagundua siyo kwa sababu ya kukosea au kukutana na ugumu.Bali ni kwa sababu waliacha kufanya. Iko hivi, wanaofanikiwa na wanaoshindwa (more…)

3199; Mauzo ya Kibabe.

By | October 4, 2023

3199; Mauzo ya Kibabe. Rafiki yangu mpendwa,Niwe mkweli kwamba huwa napenda sana mambo ya kibabe.Hasa pale ubabe huo unapomwezesha mtu kuvuka hofu na kuchukua hatua.Naamini bila ya shaka yoyote kwamba kwenye hii dunia bila ubabe wa aina fulani, huwezi kupata makubwa unayotaka.Maana kila kitu ni cha kupambania na hakuna nafasi (more…)

3198; Siyo kilema.

By | October 3, 2023

3198; Siyo kilema. Rafiki yangu mpendwa,Ni mara ngapi umewahi kuwaambia watu kwamba lengo lako ni kujenga utajiri mkubwa kwenye maisha yako, halafu watu hao wakaanza kukuonyesha lengo lako siyo sahihi?Wanakuambia kuweka lengo la utajiri ni tamaa na hata hivyo pesa huwa hazileti furaha! Sasa hebu niambie kitu kimoja, hao watu (more…)

Utalivuka Daraja Pale Utakapolikuta

By | September 30, 2023

Habari njema mstoa mwenzangu, Huwa tunahofia sana vitu vya mbele yetu. Kabla hata hatujalifikia jambo, tayari tumeshajipa presha juu ya kitu hicho kitakuwaje. Kufikiria mambo yajayo kabla hata hatujalifikia huwa linatukosesha kuishi katika hali yetu ya uwepo wa hali ya sasa. Tunafikiria yajayo na tunaacha kuishi leo na matokeo yake (more…)

3195; Kuwa mchezaji hatari kwenye mashindano.

By | September 30, 2023

3195; Kuwa mchezaji hatari kwenye mashindano. Rafiki yangu mpendwa,Kama tukiyachukulia maisha kama mchezo na wewe kama mchezaji, unaweza kuwa mchezaji hatari sana kwenye hayo mashindano.Utakuwa na hatari pale unapokuwa unaanzia chini kabisa na huna chochote cha kupoteza. Kwenye mashindano ya aina yoyote ile ni wachezaji wanaoanzia chini kabisa na hawana (more…)

XXII; Kuhusu ubatili wa kuwa njia panda.

By | September 29, 2023

XXII; Kuhusu ubatili wa kuwa njia panda. Rafiki yangu Mstoa, Kufanya maamuzi na kuyasimamia kwenye utekelezaji ni kitu ambacho kimekuwa changamoto kwa watu wengi.Kwa kutaka matokeo fulani, watu hufanya maamuzi sahihi.Lakini inapokuja kwenye utekelezaji, huwa wanasita kuchukua hatua zinazopaswa kuchukuliwa kulingana na maamuzi waliyofanya.Hapo watu wanakuwa njia panda, kwa sababu (more…)

3194; Sehemu ngumu zaidi kwenye mipango.

By | September 29, 2023

3194; Sehemu ngumu zaidi kwenye mipango. Rafiki yangu mpendwa,Watu wengi huwa hawapati mafanikio makubwa kwenye maisha yao.Na siyo kwa sababu hawataki kufanikiwa, wanakuwa wanataka sana.Pia siyo kwa sababu hawaweki mipango ya kufanikiwa, wanaiweka sana tu.Na pia siyo kwamba hawaanzi kufanyia kazi mipango yao, huwa wanaanza wakiwa na shauku kubwa.Lakini sasa, (more…)

3193; Ndiyo sababu ya kufanya.

By | September 28, 2023

3193; Ndiyo sababu ya kufanya. Rafiki yangu mpendwa,Karibu kila mtu anajua nini hasa anachotaka kwenye maisha yake.Na pia wengi wanajua nini wanapaswa kufanya ili kupata wanachotaka.Lakini cha kushangaza, inapokuja kwenye kufanya, wengi huwa hawachukui hatua. Tunaweza kushangaa kwa nje, iweje watu washindwe kufanya kile wanachojua kabisa kwamba wanapaswa kufanya ili (more…)