3184; Haina Mjadala.

By | September 19, 2023

3184; Haina Mjadala. Rafiki yangu mpendwa,Kwenye safari ya kujenga mafanikio makubwa kwenye maisha, lazima uwe na mchakato ambao unaufuata mara zote bila kuacha.Unapaswa kuwa na mambo ambayo utayafanya bila ya kuruhusu hofu au sababu zozote zile kukuzuia.Hii ni dhana inayoitwa Haina Mjadala (Non Negotiable). Kwenye mambo hayo, hupotezi muda kujiuliza (more…)

3183; Nini naweza kupenda kwake?

By | September 18, 2023

3183; Nini naweza kupenda kwake? Rafiki yangu mpendwa,Wateja tulionao kwenye kile tunachouza ni watu muhimu sana kwetu.Hao ndiyo wanaotuwezesha kulipa gharama mbalimbali kwenye maisha yetu. Ni kupitia wao kununua kwetu ndiyo tunapata fedha za kuyaendesha maisha yetu.Wateja wanaonunua kwetu ni watu muhimu sana kwetu. Swali ni je tunawafanyaje ili waweze (more…)

3182; Suuza kisha rudia.

By | September 17, 2023

3182; Suuza kisha rudia. Rafiki yangu mpendwa,Japokuwa safari ya kupata mafanikio makubwa kwenye maisha ni ngumu, watu wamekuwa wanazidisha ugumu huo kwa kuamua kuacha kufanya yale ya msingi kwenye hiyo safari. Kwenye kila eneo la maisha, huwa kuna mambo mengi ya kufanya.Lakini yapo ya msingi kabisa ambayo ni lazima yafanywe (more…)

Hiki Ndiyo Chanzo Cha Matatizo Mengi Zama Hizi

By | September 16, 2023

Mpendwa mstoa mwenzangu, Tunaishi katika zama za kelele. Na ni ngumu katika zama hizi mtu kuonekana kuwa mpweke, kukaa bila kuwa na kitu cha kufanya. Zama hizi mtu anayekaa kimya bila kupiga kelele kwenye mitandao ya kijamii au kuchangia kwenye hoja mbalimbali anaonekana kama vile amepitwa na wakati. Kwa lugha (more…)

3181; Tuko hapa kwa ajili ya utekelezaji.

By | September 16, 2023

3181; Tuko hapa kwa ajili ya utekelezaji. Rafiki yangu mpendwa,Kipindi cha nyuma, maarifa yalikuwa adimu sana kiasi cha watu kuwa tayari kuwa tayari kulipa gharama kubwa ili kuyapata na kuyatumia kupiga hatua kubwa.Kadhalika kwa mawazo mazuri ya biashara na miradi mingine.Kuna watu waliweza kuingiza kipato kikubwa kwa kuuza tu mawazo (more…)

Barua ya XX; Kuhusu kuishi yale unayohubiri.

By | September 15, 2023

Barua ya XX; Kuhusu kuishi yale unayohubiri. Rafiki yangu Mstoa,Kusema huwa ni rahisi sana, kila mtu ni msemaji mzuri. Lakini inapokuja kwenye kutenda, wengi siyo wazuri. Kushauri wengine pia ni rahisi sana, na wengi ni washauri wazuri. Lakini mara nyingi unakuta anayetoa ushauri ndiye anauhitaji zaidi huo ushauri anaotoa, ila (more…)

3180; Sitaki upate amani.

By | September 15, 2023

3180; Sitaki upate amani. Rafiki yangu mpendwa,Siku za karibuni nilikuwa nampigia mmoja wetu hapa simu.Akaniambia nikiona simu yako nakosa amani.Nikamwambia hivyo ni vizuri kabisa, kwa sababu hicho ni kiashiria kwamba programu inafanya kazi. Japokuwa jina langu ni Amani, hicho ndiyo kitu ambacho sitataka ukipate kabisa.Kwa sababu kupitia kujifunza kwa usomaji (more…)

3179; Ndoto na Juhudi.

By | September 14, 2023

3179; Ndoto na Juhudi. Rafiki yangu mpendwa,Kwenye programu ya CHUO CHA MAUZO ambayo tunaiendesha, tupo kwenye ngazi ya washiriki kufundisha masomo mbalimbali ya programu hiyo. Hivi karibuni washiriki wameshirikisha mambo waliyojifunza kwenye kijitabu kidogo nilichoandikws kinachoitwa; JINSI YA KUPATA CHOCHOTE UNACHOTAKA (A MESSAGE TO GARCIA). Kwenye kijitabu hicho, watu wanagawanyika (more…)

3178; Sijali, Naweka Kazi.

By | September 13, 2023

3178; Sijali, Naweka Kazi. Rafiki yangu mpendwa,Kwenye michezo, hasa mpira wa miguu, mashindano ambayo yanafanyika kwa njia ya ligi, timu inaweza kuwa imeshashinda kwa pointi ambazo imejikusanyia kabla hata ya ligi kuisha.Lakini lazima timu hiyo ikamilishe michezo yote iliyobaki kwenye mzunguko wa ligi.Ushindi unaweza kuwa umeshapatikana kabisa, lakini lazima muda (more…)

3177; Nidhamu na hamasa.

By | September 12, 2023

3177; Nidhamu na hamasa. Rafiki yangu mpendwa,Watu wengi kwenye maisha wamekuwa wanahangaika sana na hamasa.Wamekuwa wanatafuta vitu vya kuwapa hamasa ili kuendelea na safari yao ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa. Kwa bahati mbaya sana, hamasa haijawahi kuwa na manufaa makubwa kwa mtu, hasa kwenye safari ya mafanikio makubwa. Hiyo ni (more…)