3176; Kuza mauzo kwa macho na masikio.

By | September 11, 2023

3176; Kuza mauzo kwa macho na masikio. Rafiki yangu mpendwa,Mauzo ndiyo moyo wa biashara.Matatizo mengi ya biashara huwa yanaanzia kwenye mauzo.Pale mauzo yanapokuwa chini, changamoto nyingi hujitokeza kwenye biashara. Kwa maana hiyo basi, mahali pa kuanzia kutatua changamoto nyingi za kibiashara ni kukuza mauzo.Zipo njia nyingi za kukuza mauzo kama (more…)

3175; Muda kama silaha.

By | September 10, 2023

3175; Muda kama silaha. Rafiki yangu mpendwa,Siyo kila tatizo au changamoto unayokutana nayo kwenye maisha unahitaji kuishambulia kwa ukali.Zipo nyingine ambazo silaha yake sahihi ni muda.Kwa kuvipa vitu muda, vinajitatua vyenyewe bila ya wewe kupoteza muda kwenye kuvitatua. Mfano mzuri ni pale watu wanapoiga kile unachofanya.Ni hali inayoweza kukuumiza.Kwa sababu (more…)

Kataa Hisia Za Maumivu Na Maumivu Yataondoka Yenyewe

By | September 9, 2023

Mpendwa mstoa mwenzangu, Mchezo mzima wa maisha yetu huwa unaanzia kwenye akili. Akili yetu inatupa kile ambacho kimetawala mara nyingi kwenye akili yetu. Ukiwa na hisia za kushindwa utapata matokeo ya kushindwa. Ukiwa na hisia za kupata zaidi utashangaa na akili yako inakuletea matokeo ya ushindi kwako. Ukiwa na hisia (more…)

3174; Kitakachokufanya uache.

By | September 9, 2023

3174; Kitakachokufanya uache. Rafiki yangu mpendwa, Hadithi ambazo huwa tunajiambia sisi wenyewe, kuhusu sisi, zina nguvu kubwa sana kwenye maisha yetu.Na hadithi hizo huwa zinatokana na ushahidi wa yale ambayo huwa tunayafanya, hasa tunapokuwa peke yetu. Iko hivi rafiki, kitakachoamua mafanikio kwenye maisha yako siyo kile unachofanya mbele ya wengine, (more…)

Barua ya XIX; Kuhusu mambo ya kidunia na kustaafu.

By | September 8, 2023

Barua ya XIX; Kuhusu mambo ya kidunia na kustaafu. Rafiki yangu Mstoa, Maisha yetu hapa duniani ni ya mahangaiko, tangu tunazaliwa mpaka tunakufa.Kwenye kila hatua ya maisha kunakuwa na mambo ambayo tunayahangaikia.Na hilo limekuwa halina mwisho. Kwa watu wengi wasiokuwa na uelewa au falsafa wanayoiishi, maisha yao yote huwa ya (more…)

3173; Ufunguliwe au uvunje.

By | September 8, 2023

3173; Ufunguliwe au uvunje. Rafiki yangu mpendwa,Kama unapita mahali usiku, ambapo pana wanyama hatari na ghafla ukasikia mnyama mkali anakujia.Ukakimbia mpaka ukakutana na nyumba, ambayo mlango umefungwa.Unadhani ni nini utafanya ili uweze kujitoa kwenye hatari uliyopo? Bila shaka ni utagonga huo mlango ili uweze kufunguliwa na uondokane na hatari inayokuwa (more…)

3172; Uhuru na Raha.

By | September 7, 2023

3172; Uhuru na Raha. Rafiki yangu mpendwa,Watu wengi huwa wanachagua kuingia kwenye biashara na ujasiriamali ili kupata uhuru na raha.Wanataka uhuru wa kuyaendesha maisha yao kwa namna wanavyotaka wao na raha ya kufanya mambo yao kwa namna wanavyojisikia. Kitu ambacho wanakuwa hawakijui ni kwamba uhuru na raha huwa haviendi pamoja.Kufanya (more…)

3171; Usilipie unachoweza kupata bure.

By | September 6, 2023

3171; Usilipie unachoweza kupata bure. Rafiki yangu mpendwa,Kwenye ukurasa uliopita wa 3170, tumejifunza kuhusu kulipa ada kupitia makosa mbalimbali tunayofanya kwenye maisha yetu.Pia tukaona hekima ni kujifunza kupitia makosa ya wengine ili usiyarudie. Kwenye ukurasa huu tunakwenda kuangalia zaidi kuhusu kujenga hekima kupitia makosa ya wengine.Ndiyo maana ukurasa unaitwa usilipie (more…)

3170; Umelipa ada.

By | September 5, 2023

3170; Umelipa ada. Rafiki yangu mpendwa,Hakuna kitu ambacho kinauma kwenye maisha kama kufanya makosa.Na hilo huwa linaumiza zaidi pale makosa yanayofanyika yanapokuwa ya kifedha.Yaani pale unapokosea na kuingia gharama kwenye makosa hayo huwa linaumiza sana. Mwenzetu mmoja hapa amekuwa na safari ya kwenda nje ya nchi kwa ajili ya kukuza (more…)

3169; Msukumo wa kufanya maamuzi.

By | September 4, 2023

3169; Msukumo wa kufanya maamuzi. Rafiki yangu mpendwa,Kama kuna kitu ambacho watu huwa wanakikwepa sana ni kufanya maamuzi.Kama kuna nafasi ya watu kusubiri kufanya maanuzi, wataitumia kusubiri. Unaweza kuona ni jambo la kistaarabu kuwaacha watu mpaka wawe tayari kufanya maamuzi wao wenyewe.Lakini inapokuja kwenye mambo muhimu, hupaswi kuwa hivyo. Kwa (more…)