3168; Lugha pekee tunayoielewa hapa.

By | September 3, 2023

3168; Lugha pekee tunayoielewa hapa. Rafiki yangu mpendwa,Kuna lugha nyingi ambazo huwa zinaongelewa na wengi.Lakini hapa kwenye programu yetu ya Bilionea Mafunzoni, tunaielewa lugha moja pekee. Ni lugha ambayo sote tumeikubali na ndiyo tunaipambania katika mambo yote tunayoyafanya.Ni lugha ambayo inatuwajibisha kwenye kila kitu tunachokifanya kwenye hii safari. Ndiyo lugha (more…)

Jinsi Ya Kumjibu Mtu Anayekuletea Umbea

By | September 2, 2023

Rafiki yangu katika Ustoa, Tunaishi kwenye jamii yenye maneno, karibu kila siku tunasikia maneno yakisemwa juu yetu sisi wenyewe na hata watu wengine. Kuna wakati tunayasikia maneno mabaya na kuna wakati tunasikia maneno mazuri yakisemwa. Hatuwezi kuwazuia wengine wasituseme kwani hakuna mtu ambaye hasemwi, kama maiti inasemwa sembuse wewe uliye (more…)

3167; Msukumo sahihi.

By | September 2, 2023

3167; Msukumo sahihi. Rafiki yangu mpendwa,Sisi binadamu huwa hatufanyi maamuzi na kuchukua hatua kama hakuna msukumo ndani yetu.Ni lazima kuwe na msukumo kwanza, tena ambao unagusa hisia ndiyo tuweze kuamua na kuchukua hatua.Kadiri maamuzi na hatua tunazochukua zinavyokuwa kubwa, ndivyo msukumo unavyopaswa kuwa mkubwa pia. Kabla ya kuendelea nitakupa mfano (more…)

Barua ya XVIII; Kuhusu sherehe na kufunga.

By | September 1, 2023

Barua ya XVIII; Kuhusu sherehe na kufunga. Rafiki yangu Mstoa, Kwenye mwaka huwa kuna miezi ambayo huwa ina sherehe nyingi.Ni miezi ambayo watu hupumzika kabisa kazi zao na kusherekea.Katika kipindi hicho, watu hula na kunywa mpaka kusaza.Hiyo huwa ni miezi ambayo watu hushindwa kujizuia hasa kwenye nidhamu walizokuwa wanajijengea.Mfano mtu (more…)

3166; Bakiza moja.

By | September 1, 2023

3166; Bakiza moja. Rafiki yangu mpendwa,Kwenye harakati za kujitafuta, nimewahi kufanya kilimo cha matikiti maji.Nilishirikiana na rafiki yangu mmoja na tulijipanga vyema kuhakikisha tunapata matokeo mazuri. Baada ya kuandaa shamba, kupanda na miche kuanza kutoa matunda, tulitafuta mtaalamu wa kilimo na kwenda naye shambani ili aangalie na kutushauri zaidi mambo (more…)

3165; Huruma

By | August 31, 2023

3165; Huruma Rafiki yangu mpendwa,Huwa kuna taratibu mbalimbali ambazo huwa tumejiwekea kwenye kushirikiana na watu wengine.Kwa taratibu hizo, huwa tuna hatua za kuchukua pale mtu anapokwenda tofauti na anavyopaswa kwenda. Kuna watu ambao wanakuwa wameenda tofauti kabisa na taratibu ambazo tumeweka.Lakini inapokuja kwenye kuchukua hatua zinazopaswa kuchukuliwa, huruma inatuingia.Tunawaonea watu (more…)

3164; Uchumi wa biashara.

By | August 30, 2023

3164; Uchumi wa biashara. Rafiki yangu mpendwa,Biashara nyingi sana zinazoanzishwa huwa zinaishia kufa ndani ya muda mfupi tangu kuanzishwa kwake.Na hata zile ambazo hazifi, nyingi zimekuwa hazipati ukuaji mkubwa, badala yake zinabaki kuwa ndogo. Sababu nyingi zimekuwa zinatolewa juu ya biashara kufa.Na ya kwanza kabisa ambayo imekuwa inasemwa sana ni (more…)

3163; Mazoea na Kujisahau.

By | August 29, 2023

3163; Mazoea na Kujisahau. Rafiki yangu mpendwa,Sisi binadamu tumeumbiwa kusahau.Kusahau kumekuwa na manufaa makubwa sana kwetu kwani kumewezesha kuendelea na maisha licha ya mambo mbalimbali tunayoyapitia. Kama tungekuwa tunakumbuka kila ambacho tumepitia kwenye maisha, tusingeweza kuwa na maisha tulivu.Uzito wa kumbukumbu tunazokuwa nazo ungetuelemea sana kiasi cha kushindwa kufanya maamuzi (more…)

3162; Kufanya na kutokufanya.

By | August 28, 2023

3162; Kufanya na kutokufanya. Rafiki yangu mpendwa,Kila mtu huwa anakosea kwenye maisha.Hayupo hata mmoja ambaye anapatia mara zote.Tunachotofautiana ni aina ya makosa, ukubwa na madhara. Hapa tutaangalia aina ya makosa na jinsi yanavyowatofautisha watu kwenye matokeo wanayopata. Kuna aina mbili za makosa.Aina ya kwanza ni makosa ya kufanya. Hapa ni (more…)

3161; Nipe nikupe haitoshi.

By | August 27, 2023

3161; Nipe nikupe haitoshi. Rafiki yangu mpendwa,Sehemu kubwa ya mahusiano yetu sisi binadamu yamejengwa kwenye msingi wa nipe nikupe.Kwa sababu kwa asili watu ni wabinafsi, ambao wanajali zaidi maslahi yao kuliko maslahi ya watu wengine. Kupitia hilo la watu kujali zaidi maslahi yao binafsi, ndiyo kanuni kuu ya ushirikiano na (more…)