3146; Hujifunzi, una ahirisha.

By | August 12, 2023

3146; Hujifunzi, una ahirisha. Rafiki yangu mpendwa,Tunaishi kwenye zama za maarifa na taarifa.Hizi ni zama ambazo maarifa na taarifa zinapatikana kwa wingi na urahisi sana.Kila mtu anaweza kujifunza chochote kile anachotaka bure kabisa au kwa gharama ndogo sana. Tungetegemea kwenye zama kama hizi watu wajifunze kwa wingi sana na waweze (more…)

Barua ya XV; Kujenga afya ya akili na roho.

By | August 11, 2023

Barua ya XV; Kujenga afya ya akili na roho. Rafiki yangu Mstoa, Sisi binadamu tuna mwili, akili, roho na hisia. Lakini inapokuja kwenye kujenga afya zetu, huwa tunahangaika zaidi na afya ya mwili na kusahau hizo afya nyingine.Angalia gharama ambazo watu huwa wanaingia kwenye kujenga afya ya mwili, kuanzia ulaji, (more…)

3145; Ni wewe.

By | August 11, 2023

3145; Ni wewe. Rafiki yangu mpendwa,Huwa kuna usemi maarufu kwenye tasnia ya mafunzo ya maendeleo binafsi kwamba kama unataka kumwona mtu anayekuzuia wewe kufanikiwa basi simama mbele ya kioo.Ikimaanisha kwamba wewe ndiye kikwazo cha kwanza kwako kufanikiwa. Hicho ni kitu ambacho watu wengi wanakichukulia poa sana. Wengi wakiwa hawakiamini kweli (more…)

3143; Kikosi cha kwanza.

By | August 9, 2023

3143; Kikosi cha kwanza. Rafiki yangu mpendwa,Kila kocha wa mchezo, huwa ana wachezaji wengi kuliko inavyohitajika.Kwenye wachezaji hao wengi anaokuwa nao, huwa ana kikosi chake cha kwanza. Kikosi cha kwanza huwa kinakuwa na wale wachezaji bora kabisa ambao kocha anakuwa na imani nao kwamba wanaweza kumpa ushindi mkubwa.Hicho ndiyo kikosi (more…)

3142; Sikosi hela ya kula.

By | August 8, 2023

3142; Sikosi hela ya kula. Rafiki yangu mpendwa,Matokeo yoyote ambayo mtu unayapata yanalingana na fikra ambazo mtu unakuwa nazo.Unachopata ni sawa sawa kabisa na picha uliyonayo kwenye fikra zako. Kwa mfano kama kwenye fikra zako unajisifu kwamba kwenye shughuli zako hukosi hela ya kula, hicho ndiyo utakachoishia kupata, hela ya (more…)

3141; Kwa nini hufanyi?

By | August 7, 2023

3141; Kwa nini hufanyi? Rafiki yangu mpendwa,Unajua unachotaka kwenye maisha yako, wapi unapotaka kufika.Pia unajua nini unapaswa kufanya ili uweze kupata unachotaka.Lakini sasa, kwa nini hufanyi yale unayopaswa kufanya ili kupata unachotaka kupata? Na hata pale inapotokea unaanza kufanya, kwa nini huna mwendelezo?Kwa nini unaanza kufanya na kuishia njiani?Nini kinakukosesha (more…)

3140; Chukua picha nyingi zaidi.

By | August 6, 2023

3140; Chukua picha nyingi zaidi. Rafiki yangu mpendwa,Siku moja ya tarehe 10 Disemba mwaka 1914, Thomas Edison akiwa nyumbani kwake alipata taarifa kwamba maabara yake kubwa ilikuwa inaungua moto.Aliongozana na kijana wake kwenda kuangalia hilo na kukuta kweli maabara ikiteketea kwa moto.Baada ya kuona kinachoendelea, Edison aligeuka na kumwambia kijana (more…)

3139; Dola.

By | August 5, 2023

3139; Dola. Rafiki yangu mpendwa,Kwa zama tunazoishi sasa, sifa za utajiri huwa zinapimwa kwa thamani ya dola za Kimarekani.Huenda hilo likaja kubadilika kwa zama zijazo, ila kwa sasa hicho ndiyo kipimo. Hivyo basi, inapokuja kwenye kiwango cha utajiri ambacho mtu amefikia, thamani inayotumika ni ya dola.Na kinachopimwa ni thamani ya (more…)