3091; Tumwombee akue.

By | June 18, 2023

3091; Tumwombee akue. Rafiki yangu mpendwa,Mtoto anapozaliwa, huwa hatuwi na wasiwasi kama atakua au la.Tunachojua ni kadiri muda utakavyokuwa unaenda, kuna mabadiliko ya ukuaji ambayo tutayaona kwake.Hatuhitaji kuwa na wasiwasi wala kumwombea mtoto ndiyo akue.Ukuaji tayari upo ndani yake, kinachohitajika ni muda na mazingira sahihi ili ukuaji huo uweze kupatikana. (more…)

3090; Nipe namba, nikupe hadithi.

By | June 17, 2023

3090; Nipe namba, nikupe hadithi. Rafiki yangu mpendwa,Watu huwa wanapenda sana kuongea.Hiyo ni kwa sababu kupitia maongezi ni rahisi kuficha mambo ambayo wameshindwa kuyakamilisha.Ukiwa mtu wa kusikiliza kila sababu unazopewa na kuziamini, utapewa sababu nyingi sana ila kamwe hutapewa matokeo.Kama unataka watu waache kukupa sababu na wakupe matokeo, anza kwa (more…)

3089; Pumua, kula, fanya kazi.

By | June 16, 2023

3089; Pumua, kula, fanya kazi. Rafiki yangu mpendwa,Kuna mambo mengi sana ambayo tumekuwa tunahangaika nayo kwenye maisha yetu.Na kwa kuwa muda wetu ni wenye ukomo na mambo ya kufanya kuwa mengi, huwa ni rahisi kuahirisha baadhi ya mambo. Kuna mengi sana ambayo huwa tunayaahirisha, kwa sababu ya muda.Lakini kuna ambayo (more…)

3088; Usielezeke kirahisi.

By | June 15, 2023

3088; Usielezeke kirahisi. Rafiki yangu mpendwa,Matokeo unayoyapata sasa kwenye maisha yako, ni zao la hatua ulizochukua huko nyuma.Na matokeo utakayoyapata kesho, yatakuwa zao la hatua unazochukua leo. Watu wengi huwa wanahangaika sana na matokeo wanayoyapata na kusahau hatua wanazochukua.Matokeo yake ni kujikuta wanaendelea kupata matoke yale yale. Kile ambacho watu (more…)

3086; Uhakika wa ushindi.

By | June 13, 2023

3086; Uhakika wa ushindi. Rafiki yangu mpendwa,Maisha ni mchezo mkubwa ambapo kila mtu anapambana kupata ushindi ambao ni mafanikio. Pamoja na kila mtu kuwa kwenye mapambano hayo, ni wachache sana ambao wanapata ushindi mkubwa wanaokuwa wanautaka. Wengine wengi sana hawaupati ushindi huo, licha ya kukazana sana kuiga yale ambayo wachache (more…)

3085; Hamasa na kufanya.

By | June 12, 2023

3085; Hamasa na kufanya. Rafiki yangu mpendwa,Kuna kitendawili kikali sana kwenye hamasa na kufanya kama ilivyo kwenye yai na kuku.Watu huwa wanatumia muda mwingi kujadiliana kipi kilianza kati ya yai au kuku.Inakuwa kitendawili kikali kwa sababu ukisema yai lilianza, utaulizwa lilitagwa na kuku yupi?Na ukisema kuku alianza, utaulizwa kutoka kwenye (more…)

3084; Kila mtu anaongea, sisi tufanye.

By | June 11, 2023

3084; Kila mtu anaongea, sisi tufanye. Rafiki yangu mpendwa,Watu wanaongea sana,Wanaongea jinsi ambavyo wanataka kufanya makubwa.Wanaongea jinsi ambavyo wengi siyo waaminifu wala wachapa kazi.Wanaongea jinsi ambavyo mambo ni magumu na vikwazo vinavyowazuia.Wanaongea jinsi walivyoshindwa kutimiza yale waliyoahidi wao wenyewe. Lakini yote hayo wanayoongea hayana uzito kama ufanyaji.Kuongea kunafurahisha na kuridhisha, (more…)