3076; Kubadilika na kutokubadilika.

By | June 3, 2023

3076; Kubadilika na kutokubadilika. Rafiki yangu mpendwa,Hendry Ford, aliyekuwa mwanzilishi wa magari, alikuwa mtu mbishi sana kubadilika.Baada ya kuja na gari ambalo lilipendwa sana na watu, hakutaka kubadili chochote, badala yake aliendelea kuzalisha gari hilo hilo kwa muundo ule ule.Licha ya kushauriwa sana kubadilika, aliendelea kubaki kwenye kile alichoamini ndiyo (more…)

Barua ya V; Kuhusu Kuishi Kwa Falsafa Na Maisha Ya Mafanikio.

By | June 2, 2023

Barua ya V; Kuhusu Kuishi Kwa Falsafa Na Maisha Ya Mafanikio. Rafiki yangu Mstoa,Moja ya vitu vinavyofanya watu wengi wasiyafurahie maisha ni kutokuishi maisha halisi kwao.Wengi wanaishi maisha ya kuiga na kuwaridhisha wengine.Wengi sana wanaishi maisha ya maigizo kwa nje, huku ndani yao wakiwa tofauti kabisa. Tumekuwa tukiona watu ambao (more…)

3075; Mapenzi na pesa.

By | June 2, 2023

3075; Mapenzi na pesa. Rafiki yangu mpendwa,Watu huwa wanasema kwamba pesa haiwezi kununua mapenzi,Sijui kuhusu hilo kwenye mahusiano, lakini kwenye biashara, mapenzi na pesa haviwezi kutenganishwa. Tukianzia kwenye msingi mkuu, utafanikiwa zaidi kwenye biashara ambayo unapenda kuifanya.Ile ambayo kwako siyo kazi, bali kama mchezo, ambayo inahusisha kusudi la maisha yako (more…)

3074; Utekelezaji ni muhimu zaidi.

By | June 1, 2023

3074; Utekelezaji ni muhimu zaidi. Rafiki yangu mpendwa,Kuna watu wanadhani kwamba kinachowazuia wasifanikiwe ni hawajawa na wazo bora kabisa linaloweza kuwapa mafanikio makubwa. Wengine wengi wanadhani kinachowakwamisha ni hawajapata mtaji kwa ajili ya kuanzisha au kukuza biashara.Wengine ni ujuzi, koneksheni au kukosa rasilimali muhimu ambazo wanahitaji. Kuna mengi watu wanaweza (more…)

3073; Faida, Hasara au Mshahara?

By | May 31, 2023

3073; Faida, Hasara au Mshahara? Rafiki yangu mpendwa,Jim Rohn aliwahi kunukuliwa akisema; unalipwa kulingana na thamani unayoipeleka sokoni.Hiyo ina maana kwamba kiasi cha fedha unachopata, kinategemea sana kile unachofanya na jinsi unavyofanya vitu hivyo. Kanuni ya msingi ya uchumi pia inaeleza wazi juu ya mahitaji (demand) na upatikanaji (supply) wa (more…)

3072; Usilale.

By | May 30, 2023

3072; Usilale. Rafiki yangu mpendwa,Tuna maadui wengi sana ambao wanapambana kwa kila namna kutuzuia tusipate mafanikio makubwa tunayoyataka. Maadui wanaokuwa na nguvu sana siyo wa nje, bali wale wa ndani yetu.Hao ni maadui wanaokuwa na nguvu kwa sababu wanatujua kiundani. Uvivu, uzembe na mazoea ni maadui ambao wengi hawajui madhara (more…)

3071; Maamuzi na utekelezaji.

By | May 29, 2023

3071; Maamuzi na utekelezaji. Rafiki yangu mpendwa,Tunajua jinsi ambavyo wanaoyataka mafanikio ni wengi, lakini wanaoyapata wakiwa wachache sana. Tumeshajifunza sababu nyingi zinazowatofautisha wanaofanikiwa na wanaoshindwa. Hapa tunakwenda kuangalia eneo moja ambalo siyo kwamba halifanyiki kabisa, bali halifanyiki kwa usahihi. Eneo hilo ni kufanya maamuzi na utekelezaji wa maamuzi hayo. Watu (more…)

Jinsi Ya Kuvuka Hofu Na Wasiwasi

By | May 27, 2023

Huwa tunatengeneza picha ya hofu ambayo hata haipo kiuhalisia, tunatengeneza hofu na wasiwasi kisha hofu na wasiwasi vinatutengeneza na kuwa na wasiwasi na hofu katika akili zetu. Wakati mwingine huwa tunafikiria tutalivukaje daraja kabla hata hatujalifikia, huwa tunaanza kuwa na hofu ya mambo yajayo, kwa kujiuliza maswali kama vile, vipi (more…)

3069; Kesho itakuwa ngumu zaidi.

By | May 27, 2023

3069; Kesho itakuwa ngumu zaidi. Rafiki yangu mpendwa,Sisi binadamu huwa tupo vizuri sana kwenye kujidanganya.Huwa tunapanga mambo yetu wenyewe, tukiwa na shauku kubwa.Lakini wakati wa kufanya mambo hayo unapofika, tunaahirisha.Tunajiambia tutafanya kesho. Kama kuna kaburi ambalo lina ndoto nyingi zilizoshindwa kutimia basi ni hiyo kesho.Hebu anza tu kwa kujiuliza wewe (more…)