3037; Uwajibikaji haukwepeki.

By | April 25, 2023

3037; Uwajibikaji haukwepeki. Rafiki yangu mpendwa,Mafanikio ya aina yoyote ile kwenye maisha huwa yanaambatana na uwajibikaji.Ni uwajibikaji wa hali ya juu sana ndiyo unaozalisha mafanikio makubwa ambayo watu wanayapata kwenye maisha yao. Mafanikio pia yanategemea sana watu ambao mtu anaambatana nao.Kwa sababu hakuna mtu anayeweza kufanya kila kitu peke yake, (more…)

3036; Ndiyo ni Hapana kubwa.

By | April 24, 2023

3036; Ndiyo ni Hapana kubwa. Rafiki yangu mpendwa,Wakati tupo kwenye msimu wa HAPANA, tukumbushane jambo muhimu sana kuhusu NDIYO na HAPANA. Unaposema HAPANA kwenye kitu kimoja, unakuwa umekikataa kitu hicho kimoja tu.Hilo linakupa fursa ya kuweza kuangalia mambo mengine mazuri yanayoendana na kile unachofanya na kuweza kuyasemea NDIYO.Kwa maana hiyo (more…)

3035; Huwajibiki kumridhisha yeyote.

By | April 23, 2023

3035; Huwajibiki kumridhisha yeyote. Rafiki yangu mpendwa,Moja ya vitu vinavyotuchelewesha kufanikiwa kwenye maisha ni kujipa wajibu mwingi usiotuhusu. Na moja ya wajibu tuliojipa ambao unatutesa bure ni kutaka kumridhisha kila mtu.Huu ni wajibu unaotuchosha na usio na tija yoyote kwetu, kwa sababu hauna mchango kwetu kufikia mafanikio makubwa tunayoyataka. Tumekuzwa (more…)

Jinsi Ya Kukabiliana Na Hasira

By | April 22, 2023

Hasira ni miongoni mwa hisia hasi ambayo imekuwa ikiwagharimu watu wengi. Mpaka sasa hakuna mtu ambaye anaweza kusema hajawahi kufanya maamuzi ya hasira ambayo yalipelekea kuharibu kazi, biashara na hata kuvunja mahusiano yetu. Tatizo la hasira ni ukichaa wa muda na Mwanafalsafa Seneca anafananisha hasira na ukichaa wa muda. Kwa (more…)

3034; Fanya kwa ajili yako.

By | April 22, 2023

3034; Fanya kwa ajili yako. Rafiki yangu mpendwa,Huenda umewahi kutumia muda na nguvu zako kufanya kitu kwa ajili ya wengine.Ukitegemea kwamba watakushukuru kwa namna ulivyojitoa.Au watakulipa fadhila kwa uliyowafanyia. Lakini matokeo yanakuwa ni tofauti kabisa.Watu unaokuwa umejitoa kufanya vitu kwa ajili yao hawajali kabisa.Hawakushukuru kwa namna ulivyojitoa.Lakini pia hata pale (more…)

Misingi Mikuu Kumi Ya Falsafa Ya Ustoa.

By | April 21, 2023

Misingi Mikuu Kumi Ya Falsafa Ya Ustoa. Ustoa ni falsafa ya vitendo iliyoanzia Ugiriki ya kale na baadaye kuhamia Roma ya kale.Falsafa hii ilianzishwa na Zeno ambaye alikuwa mfanyabiashara na kwenye moja ya safari zake za kibiashara meli yake iliharibika na kupata hasara kubwa. Ni katika kutafuta namna ya kujiliwaza (more…)

3033; Wasiwe na pengine pa kwenda.

By | April 21, 2023

3033; Wasiwe na pengine pa kwenda. Rafiki yangu mpendwa,Mafanikio makubwa unayoyataka kwenye maisha yako, yatatokana na watu.Unahitaji sana watu ili kuweza kufikia ndoto kubwa ulizonazo.Na kadiri ndoto zako zinavyokuwa kubwa, ndivyo unavyowahitaji watu wengi na kwa muda mrefu. Lakini changamoto moja kubwa kwenye watu ni huwa hawaeleweki. Unaweza kuwapata watu (more…)

3031; Muda wa kutosha kwenye kazi.

By | April 19, 2023

3031; Muda wa kutosha kwenye kazi. Rafiki yangu mpendwa,Tupo kwenye msimu wa HAPANA, kipindi cha kusema HAPANA kwa mengine yote isipokuwa kujenga biashara zetu kuu na kufanya uwekezaji. Lengo kuu la kuingia kwenye msimu huu wa HAPANA ni kuondokana na mambo ambayo huwa yanakuwa usumbufu kwetu na kupunguza muda wetu (more…)

3030; Unafanya ambavyo hawafanyi.

By | April 18, 2023

3030; Unafanya ambavyo hawafanyi. Rafiki yangu mpendwa,Imezoeleka kwamba, kama unataka kufanikiwa, angalia yale ambayo waliofanikiwa wanayafanya kisha na wewe uyafanye. Kwamba mafanikio huwa yanaacha alama, kama utaangalia waliyofanya waliofanikiwa na wewe ukayafanya, utafanikiwa sana. Ni kweli kwamba mafanikio huwa yanaacha alama.Lakini kwenye kufanya yale ambayo waliofanikiwa wanayafanya, kuna ugumu mkubwa.Hiyo (more…)