3029; Msimu wa HAPANA.

By | April 17, 2023

3029; Msimu wa HAPANA. Rafiki yangu mpendwa,Hakuna neno moja lenye nguvu kubwa sana kwenye safari yako ya mafanikio kama neno HAPANA.Hapana siyo tu neno, bali ni sentensi inayojitosheleza. Ili uweze kupata mafanikio makubwa kwenye maisha yako na kufika kule unakotaka kufika, lazima useme HAPANA kwa mambo mengi sana. Kusema HAPANA (more…)

3028; Maamuzi ya mtu mmoja.

By | April 16, 2023

3028; Maamuzi ya mtu mmoja. Rafiki yangu mpendwa,Makosa mengi kwenye maisha huwa yanafanyika wakati wa kufanya maamuzi.Na kadiri watu wengi wanavyohusika kwenye kufanya maamuzi, ndivyo nafasi za kufanya makosa zinavyokuwa nyingi. Maamuzi bora ni yale yanayofanywa na mtu mmoja, ambaye ana uelewa wa kina kuhusu kile anachokiamulia.Mtu huyo anaweza kuchukua (more…)

3027; Watu wa aina yako.

By | April 15, 2023

3027; Watu wa aina yako. Rafiki yangu mpendwa,Kuna vitatu muhimu sana nilivyojifunza wakati naanza kwenye hii safari ya kujenga mafanikio makubwa kwenye maisha yako. Kimoja ni kutoka kwa aliyekuwa maandishi na mnenaji Jim Rhon ambaye alisema; maisha yako ni wastani wa maisha ya watu watano wanaokuzunguka. Akimaanisha unakuwa kama wale (more…)

3025; MIMI ni…

By | April 13, 2023

3025; MIMI ni… Rafiki yangu mpendwa,Wakati wa sikukuu ya Pasaka, kuna jumbe nyingi ambazo watu walikuwa wanatumiana.Mtu mmoja alinitumia ujumbe wa picha ambao ulinasa umakini wangu na kunifikirisha kwa kina. Ujumbe huo ni kauli saba za Yesu akisema MIMI NI…Kuna ujumbe mkubwa sana kwenye kujitamkia maneno hayo, kitu ambacho nimeona (more…)

3024; Kazi itakayokulipa vizuri wakati wote.

By | April 12, 2023

3024; Kazi itakayokulipa vizuri wakati wote. Rafiki yangu mpendwa,Ukitaka upotee na kukosa kabisa mafanikio kwenye hizi zama tunazoishi, sikiliza na fanyia kazi kila aina ya ushauri unaopewa na kila mtu. Kumekuwa na ushauri mwingi kinzani ambao umekuwa unatolewa na watu wengi kwenye mambo mbalimbali. Na sehemu kubwa ya ushauri huo (more…)

3023; Tatizo na suluhisho.

By | April 11, 2023

3023; Tatizo na suluhisho. Rafiki yangu mpendwa,Huwa kuna kauli inayosema, ukiwa na nyundo, kila kitu kinaonekana kama msumari ambao utashawishika kuugonga na nyundo hiyo. Hiyo ina maana kwamba unapokuwa na suluhisho fulani ambalo unalikubali na kulipenda sana, ni rahisi kuona kila tatizo linaweza kutatuliwa na suluhisho hilo. Unapokuwa unapenda suluhisho (more…)

3022; Kushindwa kabla ya kuanza.

By | April 10, 2023

3022; Kushindwa kabla ya kuanza. Rafiki yangu mpendwa,Kufanya jambo lolote jipya na kubwa kwenye maisha yako, huwa kunaambatana na hatari ya kushindwa. Hatari ya kushindwa huwa inakuwa kubwa pale mtu unapokuwa unafanya kwa mara ya kwanza.Kukosa uzoefu kunapelekea mtu kufanya makosa mengi yanayomuathiri. Lakini kushindwa huwa kunakuwa ni kwa uhakika, (more…)

3021; Haina mjadala.

By | April 9, 2023

3021; Haina mjadala. Rafiki yangu mpendwa,Kwenye maisha yangu sijawahi kusikia mtu anasema amekuwa bize sana kiasi kwamba amekosa muda wa kupumua.Au mtu kusema ametingwa sana kiasi cha kushindwa kula chochote kwa siku nzima. Kuna vitu ambavyo hata iweje lazima uvifanye kwenye kila siku yako.Hata iwe umebanwa kiasi gani, lazima utapumua, (more…)

3020; Nionyeshe orodha yako.

By | April 8, 2023

3020; Nionyeshe orodha yako. Rafiki yangu mpendwa,Hakuna kipindi ambacho binadamu tumevurugwa kama nyakati tunazoishi sasa.Tunaishi kwenye usumbufu mkubwa sana ambao unawinda umakini wetu.Kuna mambo mengi sana ambayo yanaonekana tunapaswa kuyafanya, lakini siyo yote ni muhimu. Njia pekee ya kutoka kwenye mtego huo wa kuwa na mambo mengi ya kufanya lakini (more…)