3019; Kwani namba zinasemaje?

By | April 7, 2023

3019; Kwani namba zinasemaje? Rafiki yangu mpendwa,Unapokuwa na ndoto kubwa unazotaka kuzifikia kwenye maisha yako, utasikia ujinga mwingi sana. Utashauriwa mambo mengi sana unayoweza kufanya ili kufikia ndoto hizo.Lakini mengi katika hayo unayoshauriwa, yanakuwa ni ujinga mtupu. Utashauriwa kutumia njia mbalimbali za mkato, ambazo huishia kuwa njia ndefu na zinazokugharimu (more…)

3018; Ushindi wa kiongozi.

By | April 6, 2023

3018; Ushindi wa kiongozi. Rafiki yangu mpendwa.Ushindi wa kiongozi yeyote yule huwa unapimwa kwa matokeo anayozalisha.Viongozi wote bora huwa wanazalisha matokeo makubwa. Unaweza kuwa kiongozi mwenye huruma, anayejali na maarufu kwa wengi, lakini kama biashara yako itashindwa, hayo yote hayatakuwa na maana. Kama biashara yako itashindwa, hakuna atakayejali wala kusikiliza (more…)

3016; Usiwe wa kawaida.

By | April 4, 2023

3016; Usiwe wa kawaida. Rafiki yangu mpendwa,Kwa chochote unachofanya kwenye maisha yako, usikubali kuwa mtu wa kawaida.Watu wa kawaida huwa wanaweza kuonekana ni wema kwenye jamii, lakini huwa hawapati mafanikio makubwa. Mafanikio makubwa huwa yanapatikana kwa kufanya mambo kwa utofauti na ukubwa kuliko ilivyozoeleka.Mafanikio makubwa ni zao la kwenda kinyume (more…)

3015; Simba na kondoo.

By | April 3, 2023

3015; Simba na kondoo. Rafiki yangu mpendwa,Mtu mmoja amewahi kusema unapaswa kuhofia zaidi kundi la kondoo 100 wanaoongozwa na simba mmoja kuliko unavyohofia kundi la simba 100 wanaoongozwa na kondoo mmoja. Hiyo ni kauli iliyobeba ujumbe mzito sana inapokuja kwenye uongozi na timu kwenye biashara.Ubora na ufanisi wa timu inayoendesha (more…)

3014; Kama hushindwi, unashindwa.

By | April 2, 2023

3014; Kama hushindwi, unashindwa. Rafiki yangu mpendwa,Sisi binadamu huwa tunaepuka sana kushindwa.Hiyo ni kwa sababu tumekuzwa tukiaminishwa kwamba kushindwa ni kubaya.Tumeaminishwa anayeshindwa anakuwa na matatizo fulani. Tangu utotoni, kushindwa kumekuwa kukiadhibiwa kwa namna mbalimbali.Hilo limetujengea hofu kubwa kwenye kushindwa.Na hofu hiyo imepelekea tusiwe tayari kujaribu vitu vipya, kwa kuwa hatutaki (more…)

3013; Muda na biashara.

By | April 1, 2023

3013; Muda na biashara. Rafiki yangu mpendwa,Mtu mmoja aliwahi kunukuliwa akisema, kama umewapenda watu wawili na unatakiwa kubaki na mmoja, unatakiwa kumchagua wa pili, kwa sababu kama ungekuwa unampenda kweli wa kwanza, usingeenda kwa wa pili. Kwa kuhamishia msingi huo kwenye biashara nakwenda kukuambia; kama kuna kitu chochote unachokipa muda (more…)

3012; Kama hakuna tatizo ni tatizo.

By | March 31, 2023

3012; Kama hakuna tatizo ni tatizo. Rafiki yangu mpendwa,Kama unaiendesha biashara yako kwa kasi na mabadiliko tunayoenda nayo, kuna matatizo mengi ambayo utayatengeneza. Mabadiliko yoyote unayofanya, lazima yazalishe matatizo mbalimbali. Kadhalika pale unapokwenda kwa kasi kubwa, lazima ufanye baadhi ya makosa ambayo yanaleta matatizo. Kama unaendesha biashara yako na hakuna (more…)

3011; Unaweza kufanya zaidi.

By | March 30, 2023

3011; Unaweza kufanya zaidi. Rafiki yangu mpendwa,Ukiwa ardhini na ukatazama angani, unaona anga au mawingu kama ndiyo ukomo.Lakini ukipata njia ya kupanda juu zaidi, unagundua ukomo ulioona ukiwa chini siyo mwisho, bali unaweza kwenda zaidi na zaidi. Hivyo ndivyo ilivyo kwenye mambo mengi ya maisha, ukomo unaokuwa unauona siyo halisi, (more…)