3009; Umasikini na uaminifu.

By | March 28, 2023

3009; Umasikini na uaminifu. Rafiki yangu mpendwa,Kwenye makala ya ukurasa wa 3008 uliopita niliandika;‘Hakuna kitu kama masikini mwenye furaha,Au masikini mwaminifu.Furaha na uaminifu haviwezi kukaa pamoja na umasikini.’ Kila mtu alikubaliana na upande kwamba hakuna masikini mwenye furaha.Na hilo liko wazi kwamba huwezi kuwa na furaha kama huna uhakika wa (more…)

3008; Shughuli muhimu zaidi.

By | March 27, 2023

3008; Shughuli muhimu zaidi. Rafiki yangu mpendwa,Kuna shughuli nyingi sana unazojihusisha nazo kwenye maisha yako ya kila siku.Lakini shughuli iliyo muhimu zaidi kuliko zote ni ile ya kujiingizia kipato.Hiyo ndiyo shughuli muhimu kwa sababu ndiyo msingi mkuu wa maisha yako. Kuingiza kipato ndiyo msingi wa kuyaendesha maisha yako. Ndiyo kunakuwezesha (more…)

3007; Jaribio.

By | March 26, 2023

3007; Jaribio. Rafiki yangu mpendwa,Moja ya vikwazo vikubwa kwa watu kufanikiwa ni tabia ya kughairisha mambo. Mtu anakuwa anajua kabisa nini anatakiwa kufanya, lakini hafanyi. Na mara nyingi sana kinachowafanya watu waghairishe mambo ni kuyaona ni makubwa na kuhofia kushindwa.Mambo yanayoghairishwa zaidi ni yale ambayo ni mapya na makubwa. Yanaghairishwa (more…)

3006; Haifanyiki.

By | March 25, 2023

3006; Haifanyiki. Rafiki yangu mpendwa,Asili ina kanuni ya visababishi na matokeo.Kanuni hiyo inasema kwa kila matokeo unayoyaona, kuna visababishi vyake.Hivyo basi, kama kuna matokeo ulitegemea kuyaona ila hayaonekani, ni kwamba hakuna visababishi. Waswahili wanasema ukiona vyaelea ujue vimeundwa.Mambo hayatokei tu kwa bahati au ajali, bali huwa yanasababishwa. Na hapo ndipo (more…)

3005; Wewe na biashara.

By | March 24, 2023

3005; Wewe na biashara. Rafiki yangu mpendwa,Changamoto nyingi ambazo watu wanakutana nazo kwenye biashara, chanzo chake ni watu kushindwa kujitofautisha na biashara zao.Kwa sababu wanamiliki biashara, basi wanadhani biashara hizo ni wao na hivyo kufanya chochote wanachojisikia kwenye biashara hizo. Hizo fikra kwamba wao ndiyo biashara na wanaweza kufanya chochote (more…)

3004; Malengo na sababu.

By | March 23, 2023

3004; Malengo na sababu. Rafiki yangu mpendwa, Huwa tunachukulia wanaoshindwa kwenye maisha kama watu ambao hawana malengo yoyote.Na wanaofanikiwa kwenye maisha tunaona ndiyo wenye malengo. Kwa kifupi tunachodhani ni tofauti ya wanaoshindwa na wanaofanikiwa ni malengo.Lakini huo siyo ukweli, karibu kila mtu ana malengo fulani. Malengo hayo yanaweza kuwa madogo (more…)

3003; Piga makofi tafadhali.

By | March 22, 2023

3003; Piga makofi tafadhali. Rafiki yangu mpendwa,Wengi wetu tumelelewa kwenye mazingira ambayo hatujafundishwa kutambua, kuthamini na kusifia juhudi na hatua wanazopiga wengine. Pale tunapoona kuna wengine wamefanikiwa kuliko sisi kwenye jambo lolote lile, tunatafuta sababu ya kubeza uwezo ambao mtu ametumia kupata alichopata. Na hapo ndipo chuki zote dhidi ya (more…)

3002; Unajiangusha mwenyewe.

By | March 21, 2023

3002; Unajiangusha mwenyewe. Rafiki yangu mpendwa,Hakuna mtu yeyote anayeweza kukuangusha kwenye maisha yako isipokuwa wewe mwenyewe. Chochote unachotaka kwenye maisha na hujakipata, hakuna aliyekunyima ila wewe mwenyewe.Ni wewe ndiye unayejizuia kupata yale yote unayoyataka kwenye maisha yako. Na picha linaanzia pale unachotaka hakiendani na kile unachofanya.Unakuwa unataka makubwa sana, lakini (more…)

3001; Wape ushindi.

By | March 20, 2023

3001; Wape ushindi. Rafiki yangu mpendwa,Falsafa kuu ambayo ndiyo huwa naendesha nayo huduma zangu, ambayo nilijifunza kutoka kwa Zig Zigler inasema; unaweza kupata chochote unachotaka kwenye maisha yako, kama utawasaidia watu wengi zaidi kupata kile wanachotaka. Swali ni watu wengi wanataka nini ili uweze kuwapatia na wewe upate unachotaka?Jibu ni (more…)