2999; Mlango wa kutokea.

By | March 18, 2023

2999; Mlango wa kutokea. Rafiki yangu mpendwa,Kazi ya kujenga timu ambayo ndiyo kipaumbele chetu kikubwa kwa sasa siyo kazi rahisi.Ina changamoto za kila aina.Kuna makosa madogo madogo ambayo ukiyafanya yanakuwa kikwazo kikubwa kwako kujenga timu bora. Ili kuepuka makosa hayo kwenye kujenga timu, ni muhimu kuwa na hatua unazozifuata kwenye (more…)

2998; Amini.

By | March 17, 2023

2998; Amini. Rafiki yangu mpendwa,Kujenga timu bora ya kuendesha biashara kunahitaji watu.Na watu huwa wanapenda kumfuata mtu anayejua wapi anakwenda na ana amini atafika kule anakokwenda. Ili uweze kuwavuta watu sahihi kuja kwako, lazima uwe kiongozi mzuri, ambaye unajua unakokwenda na unaamini utafika unakokwenda.Watu wanataka uwe na imani isiyoyumba kuhusu (more…)

2997; Wingi na ubora.

By | March 16, 2023

2997; Wingi na ubora. Rafiki yangu mpendwa,Kwenye kila kitu tunachofanya, kuna njia mbili za kukiendea; wingi na ubora. Kwenye wingi unaangalia namba.Na kadiri namba inavyokuwa kubwa, ndivyo matokeo yanavyokuwa mazuri pia. Kwenye ubora unaangalia viwango.Kadiri viwango vinavyokuwa vya juu, ndivyo matokeo yanavyokuwa mazuri. Kwa bahati mbaya sana wingi na ubora (more…)

2996; Fanya vitu vya maana.

By | March 15, 2023

2996; Fanya vitu vya maana. Rafiki yangu mpendwa,Sisi binadamu tuna rasilimali tatu ambazo zina uhaba mkubwa sana. Rasilimali hizo ni muda, nguvu na umakini.Hizo ni rasilimali ambazo ukishaziweka kwenye kitu kimoja, huwezi kuziweka tena kwenye kitu kingine. Chochote unachofanya kwenye maisha yako, lazima utahusisha rasilimali hizo tatu, utaweka muda wako, (more…)

2995; Ongoza.

By | March 14, 2023

2995; Ongoza. Rafiki yangu mpendwa,Viongozi huwa wana kazi kuu moja, ambayo ni kuongoza.Na ili kuongoza vyema, huwa wanaondoa kila aina ya mashaka wanayokuwa nayo.Wanajitoa kweli kweli kwenye kile ambacho wanakifanya. Viongozi bora misimamo yao huwa inajulikana wazi.Kama wapo ndani basi wapo ndani moja kwa moja.Hawawi mguu mmoja ndani na nguu (more…)

2993; Ukiondoka, siyo kwa sababu hizi mbili.

By | March 12, 2023

2993; Ukiondoka, siyo kwa sababu hizi mbili. Rafiki yangu mpendwa,Tangu nimeanza huduma hii ya ukocha, kuna watu wengi sana ambao wameshapita na kuondoka.Wapo ambao niliwaondoa mimi mwenyewe na wapo ambao waliondoka wao wenyewe. Niliowaondoa sababu kuu ni moja tu, kushindwa kukaa kwenye mchakato ambao tumekubaliana, licha ya kuelekezwa kwa kila (more…)

2992; Ukomo wa watu wengine.

By | March 11, 2023

2992; Ukomo wa watu wengine. Rafiki yangu mpendwa,Watu wengi hawafanikiwi kwenye maisha yao kwa sababu wana ukomo ambao wamejiwekea kwenye fikra zao. Wanakuwa wamefunga fikra zao kwa nini kinachowezekana na nini hakiwezekani. Wanapokuona wewe ukiwa na fikra za kufanya makubwa, wanakuambia haiwezekani. Kukuambia kwao haiwezekani, siyo kwamba haiwezekani kweli, bali (more…)

2991; Tutashinda.

By | March 10, 2023

2991; Tutashinda. Rafiki yangu mpendwa,Kwenye hii safari ya ubilionea, ni lazima tupate ushindi.Na hilo litawezekana kama tu tutaufanya mchakato wa safari hii kuwa kipaumbele cha kwanza kwenye maisha yetu.Safari yenyewe siyo rahisi, lakini kwa kuifanya kuwa kipaumbele cha kwanza, tunajiweka kwenye nafasi ya kushinda. Kuna mambo mengi yanayotaka muda, nguvu (more…)

2990; Usalama na Uhuru.

By | March 9, 2023

2990; Usalama na Uhuru. Rafiki yangu mpendwa,Sisi binadamu huwa tuna mahitaji mbalimbali kwenye ngazi mbalimbali za maisha yetu. Hitaji la chini na la msingi kabisa huwa ni usalama.Huwa tunapenda kuwa na uhakika kwamba maisha yetu yanaweza kuendelea bila ya kikwazo chochote. Hitaji la juu kabisa ni uhuru.Huwa tunapenda kuwa huru, (more…)