2979; Hofu ya mafanikio.

By | February 26, 2023

2979; Hofu ya mafanikio. Rafiki yangu mpendwa,Kwa kipindi kirefu ambacho nimekuwa najifunza kuhusu mafanikio, nimekuwa na kutana na sababu mbalimbali zinazowazuia watu kufanikiwa.Moja ya sababu hizo ni hofu ya mafanikio. Nilikuwa sielewi iweje mtu anayeyataka mafanikio awe pia anayahofia mafanikio?Sikuwa nalipa sana uzito hilo kwenye sababu za watu kutokufanikiwa. Ni (more…)

2978; Biashara rahisi kufanya.

By | February 25, 2023

2978; Biashara rahisi kufanya. Rafiki yangu mpendwa,Swali la ni biashara gani rahisi kwa mtu kufanya ni swali ambalo nimekuwa naulizwa kila mara na watu.Kipindi cha nyuma nilikuwa nakazana kuwaelewesha watu ni biashara gani zinaweza kuwafaa watu kulingana na hali wanazokuwa nazo. Lakini kwa uzoefu ambao nimeshajijengea mpaka sasa kwenye biashara, (more…)

2977; Furahia kushindwa.

By | February 24, 2023

2977; Furahia kushindwa. Rafiki yangu mpendwa,Kwenye safari ya mafanikio ambayo tupo, hakuna kitu kizuri ambacho kila mmoja anakitaka kama ushindi. Tunapenda sana ushindi, uwe ni mdogo mdogo au mkubwa, kwa sababu ni kiashiria kizuri kwamba tunaelekea kule tunakotaka kufika. Japokuwa kushinda kunaleta hali ya kujisikia vizuri wakati huo wa ushindi, (more…)

2976; Muda na usumbufu.

By | February 23, 2023

2976; Muda na usumbufu. Rafiki yangu mpendwa,Inapokuja kwenye muda, msimamo wangu uko wazi mara zote, tatizo letu siyo muda, bali kile tunachofanya na muda tulionao.Ninaamini, bila ya shaka yoyote kwamba muda tunao mwingi, ila tu tunautumia vibaya.Kwamba tatizo kubwa la muda tulilonalo, siyo kwamba muda ni wa uhaba, bali tunao (more…)

2975; Huu ndiyo ushindi.

By | February 22, 2023

2975; Huu ndiyo ushindi. Rafiki yangu mpendwa,Wote tulio hapa tuna lengo kubwa moja ambalo ni kufikia ubilionea.Hilo ndiyo lengo kuu ambalo kila mmoja wetu analipambania.Ni lengo ambalo tunaamini bila ya shaka yoyote kwamba tutakifikia.Kwa sababu tupo tayari kulipambania bila ya kuchoka wala kukata tamaa. Katika kufikia lengo hilo la ubilionea, (more…)

2974; Umekufa au hutaki.

By | February 21, 2023

2974; Umekufa au hutaki. Rafiki yangu mpendwa,Moja ya vitu muhimu unavyohitaji sana kwenye safari yako ya mafanikio ni msimamo usioyumbishwa.Na msimamo huo haupaswi tu kuwa kwenye yale unayotaka, bali pia kwenye yale unayoahidi. Unapaswa kufanya neno lako kuwa sheria.Kwamba ukiahidi unatekeleza kama ulivyoahidi na siyo kuanza kuleta sababu. Unahitaji kuwa (more…)

2973; Wape sababu ya kukuheshimu.

By | February 20, 2023

2973; Wape sababu ya kukuheshimu. Rafiki yangu mpendwa,Tunajifunza mambo mengi kwenye biashara na mauzo.Na mengi sana tunayojifunza yameegemea kwenye kuwajali sana wateja na kuweka maslahi yao mbele.Hayo ni mambo yenye nguvu na ushawishi mkubwa kwa wateja. Lakini pia kuna wateja wanachukulia kujali kwetu kama sehemu ya kutaka kutunyanyasa.Kwa kuwa tumechagua (more…)

2972; Hatari umeibeba wewe.

By | February 19, 2023

2972; Hatari umeibeba wewe. Rafiki yangu mpendwa,Kuendesha biashara kuna changamoto nyingi sana.Kila wakati kuna kitu unakuwa unapambana nacho. Kama hiyo haitoshi, kuna hatari kubwa unayokuwa umeibeba kila siku kibiashara.Changamoto unazokabiliana nazo kibiashara zinakuwa na hatari ya kuweza kupelekea biashara kufa. Tatizo zaidi ni kwamba hatari yote ya biashara yako umeibeba (more…)

2971; Uongozi, usimamizi na ufuatiliaji.

By | February 18, 2023

2971; Uongozi, usimamizi na ufuatiliaji. Rafiki yangu mpendwa,Kila mtu ambaye anaajiri watu wa kumsaidia majukumu ya kibiashara, anajua changamoto nyingi ambazo anakutana nazo. Imekuwa ni changamoto kubwa sana kupata wafanyakazi sahihi na kuweza kukaa nao kwenye biashara kwa muda mrefu. Kumekuwa na maumivu, malalamiko, kukatishwa tamaa na kuvurugwa kwa wengi (more…)

2970; Kosa la uzururaji.

By | February 17, 2023

2970; Kosa la uzururaji. Rafiki yangu mpendwa,Kipindi nikiwa mdogo, nilikuwa nashangaa sana pale niliposikia kuna watu wamekamatwa na posili kwa kosa la uzururaji.Nilikuwa nashangaa mtu mzima anazururaje.Maana nilizoea unapoambiwa acha kuzurura, maana yake ni uache kwenda kila mahali na kutulia sehemu moja. Baadaye nilikuja kujifunza kwamba kumbe uzururaji siyo tu (more…)