2969; Tegemeo lako.

By | February 16, 2023

2969; Tegemeo lako. Rafiki yangu mpendwa,Hakuna kipindi kizuri kwenye kujenga biashara kama kipindi ambacho biashara ina wateja wachache. Wengi hukihofia kipindi hiki na kukimbilia kufafuta wateja wengi zaidi kabla hawajawajua vizuri wateja wachache walionao. Hakuna tatizo lolote kwenye kutaka kufikia wateja wengi zaidi. Lakini itapendeza sana kama utawatumia vizuri wateja (more…)

2968; Sizitaki mbichi hizi.

By | February 15, 2023

2968; Sizitaki mbichi hizi. Rafiki yangu mpendwa,Bila shaka unakumbuka moja ya hadithi ambazo tulijifunza shuleni.Ambapo sungura aliziona ndizi, akaamua azirukie ili aweze kula.Akaruka na kuruka sana, lakini hakuweza kuzifikia.Akakazana kuruka tena na tena, lakini bado hakuzifikia ndizi hizo.Mwisho akajiambia hata hivyo ndizi zenyewe ni mbichi, sizitaki. Kwa kusoma hadithi hiyo (more…)

2967; Haifai kwangu.

By | February 14, 2023

2967; Haifai kwangu. Rafiki yangu mpendwa,Tofauti kubwa ya watu waliofanikiwa na walioshindwa ni hii; waliofanikiwa wanaona suluhisho kwenye kila tatizo, wakati walioshindwa waliona tatizo kwenye kila suluhisho. Waonyeshe waliofakiwa njia fulani yenye matokeo mazuri kwa wengine na wataona jinsi gani njia hiyo inaweza kuwafaa na wao pia.Lakini mwonyeshe aliyeshindwa njia (more…)

2966; Kwa nini usiwe wewe?

By | February 13, 2023

2966; Kwa nini usiwe wewe? Rafiki yangu mpendwa,Kwa mambo yote makubwa unayotaka kufanya au kufikia, tayari kuna wengine wanafanya au wameshafikia.Swali kubwa unalopaswa kujiuliza ili likusukume ni kwa nini na wewe pia usiwe? Kuna vipindi ambavyo watu huwa wanalalamikia sana biashara. Uchumi unakuwa mgumu na wateja wanakosa nguvu ya kununua.Lakini (more…)

2965; Siamini.

By | February 12, 2023

2965; Siamini. Rafiki yangu mpendwa,Kumekuwa na sababu moja pendwa kwa watu wengi wanaoshindwa kufanya yale wanayopaswa kufanya. Sababu hiyo ni; “SIna muda.”Karibu kila mtu anatumia kauli hiyo kama sababu ya kushindwa kufanya makubwa. Lakini niseme ukweli kabisa, mimi siamini kabisa kwamba hakuna muda.Naamini bila ya shaka yoyote kwamba muda tayari (more…)

2964; Onyesha kazi yako.

By | February 11, 2023

2964; Onyesha kazi yako. Rafiki yangu mpendwa,Wakati upo shuleni, ulifundishwa namna sahihi ya kufanya hisabati.Kila swali la hisabati lilikuwa na sehemu tatu.Sehemu hizo ni swali, kazi, jibu.Katika kujibu maswali hayo ya hisabati hukutakiwa tu kutoa jibu sahihi, bali ulitakiwa kuonyesha njia uliyotumia kupata jibu hilo.Mara nyingi, hata kama ulikosa jibu, (more…)

2963; Imani na matamanio makubwa.

By | February 10, 2023

2963; Imani na matamanio makubwa. Rafiki yangu mpendwa,Ili uweze kufikia mafanikio makubwa unayoyataka kwenye maisha yako, unapaswa kuchukua hatua kubwa pia.Hatua ambazo siyo za kawaida na wengi hawawezi kuzichukua. Unapaswa kuchukua hatua kubwa kwa namna ambayo wengine wanakushangaa, ya kwamba unawezaje kuchukua hatua za aina hiyo. Unapaswa kufanya kazi kwa (more…)

2962; Weka dau lako hapa.

By | February 9, 2023

2962; Weka dau lako hapa. Rafiki yangu mpendwa, Huwa sishauri mtu yeyote mwenye akili timamu acheze kamari au michezo mingine ya kubahatisha, ambayo kwangu yote hayo ni kitu kimoja. Lakini mcheza kamari au michezo hiyo ya kubahatisha akisikia hayo, anakimbilia kukuambia kwenye maisha kila kitu ni kamari. Hapo akimaanisha hakuna (more…)

2961; Uza maziwa, siyo ng’ombe.

By | February 8, 2023

2961; Uza maziwa, siyo ng’ombe. Rafiki yangu mpendwa,Ukiwa na ng’ombe, ambaye unamkamua maziwa, halafu akajitokeza mtu na kukuambia ng’ombe wako anatoa maziwa vizuri, niuzie maana nina uhitaji sana wa maziwa.Kama ndiye ng’ombe pekee uliyenaye na ndiye tegemeo kwako, unajua vyema kwamba hutakubali kumuuza ng’ombe huyo, bali utamwambia umuuzie maziwa. Kadhalika (more…)

2960; Usiwauzie, wafundishe.

By | February 7, 2023

2960; Usiwauzie, wafundishe. Rafiki yangu mpendwa,Mauzo yanakuwa magumu kwa wengi kwa sababu wamekuwa wakikazana kuwalazimisha watu kununua.Wanachosahau watu hao ni kwamba hakuna mteja anayependa kuona amelazimishwa kununua. Kuuza ni kufundisha na kufundisha ni kuuza.Wauzaji ambao wamekuwa wanaweka mbele kipaumbele cha kufundisha badala ya kuuza, wamekuwa wanaingiza kipato kikubwa sana. Wafundishe (more…)