2928; Asiwepo wa kuizidi biashara.

By | January 6, 2023

2928; Asiwepo wa kuizidi biashara. Rafiki yangu mpendwa, Matatizo mengi ya kibiashara yamekuwa yanaanzia pale mfanyabiashara anaposhindwa kujitofautisha yeye na biashara yake. Waanzilishi wengi wa biashara huwa wanadhani wao na biashara zao ni kitu kimoja. Na hilo limekuwa linapelekea wafanye maamuzi ambayo yanaiathiri sana biashara. Kosa kubwa wanalofanya ni kuifanya (more…)

2927; Nitavumilia matokeo, siyo mchakato.

By | January 5, 2023

2927; Nitavumilia matokeo, siyo mchakato. Rafiki yangu mpendwa, Kwenye maisha kuna mambo mawili makubwa; mchakato na matokeo. Mchakato ni yale unayofanya, hatua unazochukua kwenye kila jambo. Matokeo ni kile kinachokuja kupatikana kutokana na hatua zinazokuwa zimechukuliwa. Mchakato upo ndani ya uwezo wa mtu. Mtu ana uwezo wa kuamua nini afanye (more…)

2926; Nipe masaa yangu 16.

By | January 4, 2023

2926; Nipe masaa yangu 16. Rafiki yangu mpendwa, Utakumbuka kwenye ukurasa wa 2926 nilikueleza kwa kina uhusiano wangu mimi na wewe na namna tunavyokwenda. Kwenye vipengele 10 nilivyoeleza, kipengele namba 7 kilieleza kwamba mimi ni meneja wako. Meneja wako kwenye masomo, mauzo na mafunzo. Wajibu wa meneja ni kuhakikisha mambo (more…)

2925; Jiamini kupitiliza.

By | January 3, 2023

2925; Jiamini kupitiliza. Rafiki yangu mpendwa, Kwenye safari ya mafanikio makubwa uliyopo, upinzani unaokabiliana nao ni mwingi na mkubwa sana. Kila kitu kinakuzuia wewe usipate mafanikio makubwa unayoyataka. Upinzani huo unaanzia ndani yako mwenyewe. Tabia zako binafsi ni kikwazo kikubwa sana kwako kufanikiwa. Uvivu, uzembe na kukata tamaa na vitu (more…)

2924; Kata Tamaa.

By | January 2, 2023

2924; Kata Tamaa. Rafiki yangu mpendwa, Leo nakupa ruhusa ambayo umekuwa unajinyima kwa muda mrefu. Ruhusa ya kukata tamaa na kuachana na baadhi ya vitu, hata kama unavitaka sana. Umezoea kupata mafunzo yanayokuhamasisha usikate tamaa, upambane mpaka tone la mwisho ili kupata ushindi. Umekuwa unapewa mifano ya watu ambao hawakukata (more…)

2923; Haina maana.

By | January 1, 2023

2923; Haina maana. Kwako rafiki yangu mpendwa ambaye upo kwenye biashara lakini bado hujajitoa kafara kweli kweli ili kufanikiwa kwenye biashara. Leo nakwenda kukuambia kitu ambacho kinaweza kukukatisha kabisa tamaa au kukupa nguvu ya kupambana sana. Kitu chenyewe ni hiki; KAMA LENGO LAKO SIYO KUWA BILIONEA, USIFANYE BIASHARA. Ndiyo, najua (more…)

2922; Mambo yanapokuwa magumu.

By | December 31, 2022

2922; Mambo yanapokuwa magumu. Rafiki yangu mpendwa, Kwenye hii safari ya mafanikio, mara nyingi utakutana na mambo magumu na changamoto. Hata pale unapokamilisha mipango unayokuwa umejiwekea, kufurahia huwa ni kwa muda mfupi. Baada ya hapo unapaswa kurudi kwenye kupambania malengo na mipango mikubwa zaidi ya uliyofikia. Kitu ambacho kifakupeleka kwenye (more…)

2921; Mimi na wewe.

By | December 30, 2022

2921; Mimi na wewe. Rafiki yangu mpendwa, Ninapokuita rafiki, simaanishi kuwa na wajibu wa kukufanya ujisikie vizuri. Bali namaanisha upendo mkubwa nilionao kwako wenye nia ya kuhakikisha unapata kile hasa unachotaka. Na hilo halitakuwa rahisi, ndiyo maana upo hapa. Lengo la ujumbe huu wa leo ni kufafanua mahusiano yangu mimi (more…)