2919; Watatenganishwa na fedha zao.

By | December 28, 2022

2919; Watatenganishwa na fedha zao. Kwako rafiki yangu mpendwa unayewaonea wateja huruma na fedha zao. Wateja wanakuambia hawana fedha au wamebaki na fedha kidogo na wewe unaona hupaswi kuwamalizia fedha zao kwa kuwauzia unachouza. Kama utayaendea mauzo na wateja kwa mtazamo huo, kamwe hutouza. Mauzo yatakuwa magumu sana kwako kwa (more…)

2918; Washindwe kunyamaza.

By | December 27, 2022

2918; Washindwe kunyamaza. Kwako rafiki yangu mpendwa ambaye unashindwa kuwashawishi wateja wa biashara yako kukuletea wateja zaidi. Katika njia zote za masoko zilizopo, njia ya wateja kuambiana ndiyo njia yenye nguvu kubwa na matokeo mazuri. Watu wanaposikia kitu kutoka kwa watu wao wa karibu wanashawishika haraka kuliko wakisikia kutoka kwa (more…)

2916; Saa Mbovu.

By | December 25, 2022

2916; Saa Mbovu. Kwako rafiki yangu mpendwa unayetafuta kitu sahihi kabisa na chenye uhakika wa asilimia 100 ndiyo ukomae nacho. Ukweli ni utasubiri sana nahuenda hutafanya chochote kabisa. Hakuna kitu chochote ambacho kiko sahihi zaidi ya vingine vyote. Kila kitu kina mazuri na mabaya yake, urahisi na changamoto zake. Kadhalika (more…)

2915; Nenda kauze.

By | December 24, 2022

2915; Nenda kauze. Kwako rafiki yangu mpendwa unayekabiliwa na changamoto mbalimbali za kimaisha na biashara kwa ujumla. Kuna njia moja ya uhakika ya kuondoka kwenye changamoto zote zinazokukabili hata kama ni kubwa kiasi gani. Njia hiyo ni kufanya mauzo zaidi. Karibu kila changamoto inayokukabili sasa, inaweza kutatuliwa vizuri kabisa kwa (more…)

2914; Usitoboe sikio.

By | December 23, 2022

2914; Usitoboe sikio. Kwako rafiki yangu mpendwa unayepima mafanikio yasiyo mafanikio. Kipimo kisicho sahihi cha mafanikio kimekuwa ni kikwazo kikubwa kwa wengi kuyafikia mafanikio ya kweli. Moja ya njia ambazo huwa natumia kupata utulivu wakati nafanya kazi kubwa ya uandishi ni kusikiliza muziki. Na katika kusikiliza muziki, huwa kuna nyimbo (more…)

2913; Muhimu zaidi.

By | December 22, 2022

2913; Muhimu zaidi. Kwako rafiki yangu mpendwa unayesema unatingwa na mambo mengi kwenye biashara. Napenda kukuuliza, katika mengi yanayokutinga, mangapi ndiyo muhimu kabisa? Ni mambo yapi machache ambayo ukikusanya nguvu zako hapo unapata matokeo makubwa? Na muhimu zaidi, jambo lipi moja ambalo ukilipa kipaumbele cha kwanza, linaweza kuleta mapinduzi makubwa (more…)

2912; Hakuna Amani.

By | December 21, 2022

2912; Hakuna Amani. Kwako rafiki yangu mpendwa unayedhani mafanikio makubwa yatakuwa chanzo cha amani na utulivu kwako. Nina habari ambazo siyo njema sana kwako. Mafanikio makubwa unayoyasaka hayatakupa amani na utulivu. Kwa hakika, kadiri unavyofanikiwa ndivyo unavyozidi kukosa amani na utulivu. Kwanza kabisa kadiri unavyofanikiwa, wajibu wako pia unaongezeka. Unawajibika (more…)

2911; Misingi.

By | December 20, 2022

2911; Misingi. Kwako rafiki yangu mpendwa unayeona mambo ni magumu na mafanikio hayawezi kufikiwa. Jambo la kwanza ninalotaka kukuhakikishia ni kwamba mara zote mafanikio huwa yapo. Yaani hata mambo yawe magumu kiasi gani, bado mafanikio yapo. Hata hali ya uchumi iwe ngumu kiasi gani, mazingira yawe magumu kiasi gani, mafanikio (more…)

2910; Wakati sahihi wa kutafuta kitu.

By | December 19, 2022

2910; Wakati sahihi wa kutafuta kitu. Kwako rafiki yangu mpendwa ambaye umekuwa unakutana na changamoto kubwa kwenye mambo unayokuwa unayataka. Umekuwa unasubiri mpaka pale unapokihitaji kitu kwa haraka ndiyo unahangaika kukitafuta. Kwa haraka unayokuwa nayo, unajikuta ukishindwa kuzingatia mambo muhimu na hilo linapelekea ufanye makosa. Wakati sahihi wa kutafuta kitu (more…)