2909; Vipaumbele.

By | December 18, 2022

2909; Vipaumbele. Kwako rafiki yangu mpendwa unayelalamika kwamba huna muda wa kufanya baadhi ya mambo ambayo unapaswa kuyafanya. Kiuhalisia, tatizo lako siyo muda, bali tatizo lako ni vipaumbele. Kila siku unapata masaa yako 24, yaliyojaa kabisa na wewe ndiye unayepanga unayatumiaje masaa hayo. Unapolalamika huna muda, unajua kabisa kwamba siyo (more…)

2908; Mabadiliko.

By | December 17, 2022

2908; Mabadiliko. Kwako rafiki yangu mpendwa unayeona mabadiliko ni magumu kuliko mazoea uliuokuwa nayo awali. Hilo ni kweli, Kwa mtazamo wa haraka haraka, mabadiliko huwa yanaonekana ni magumu na mabaya. Huwa ni vigumu sana kuachana na kile ambacho mtu umeshakizoea na kwenda kwenye kitu kipya ambacho hakijazoeleka. Ulichokizoea, hata kama (more…)

2907; Ushauri.

By | December 16, 2022

2907; Ushauri. Kwako rafiki yangu mpendwa unayepoteza muda mwingi kutoa au kupokea ushauri. Nimewahi kusema huko nyuma usitoe ushauri kama hujaombwa na usipokee ushauri kama hujaomba. Wengi hawakulielewa hilo na waliona ni kama kauli tata tu. Lakini hiyo ni kauli yenye nguvu sana ambayo ukiifanyia kazi, utajiepusha na mengi sana (more…)

2906; Kukosa subira kunakuponza.

By | December 15, 2022

2906; Kukosa subira kunakuponza. Kwako rafiki yangu mpendwa unayekata tamaa haraka pale unapokuwa huoni matokeo unayotaka licha ya kuweka juhudi kubwa. Kuweka juhudi ni sehemu moja muhimu katika mafanikio. Na ndilo eneo pekee ambalo una udhibiti nalo. Kuwa na subira ni eneo jingine muhimu sana kwenye safari ya mafanikio, eneo (more…)

2905; Wanakudanganya.

By | December 14, 2022

2905; Wanakudanganya. Kwako rafiki yangu mpendwa unayeshangazwa na jinsi ambavyo watu wanabadilika na kudanganya. Unakuta unawaamini sana watu, lakini ghafla wanakuja kubadilika na kuwa wadanganyifu. Ni vigumu sana kwa watu kubadilika ghafla. Watu huwa wanang’ang’ana sana na tabia zao. Hivyo kama kuna mtu unaona amebadilika, kwa sehemu kubwa anakuwa hajabadilika, (more…)

2904; Roho nzuri.

By | December 13, 2022

2904; Roho nzuri. Kwako rafiki yangu mpendwa unayejiambia unataka kuwa na roho nzuri na ukubalike na watu wote. Hicho ni kitu ambacho hakijawahi kutokea tangu kuwepo kwa maisha hapa duniani. Na kama utaendelea kukisisitiza basi utashindwa vibaya sana. Kwa asili, sisi binadamu ni wavivu, wazembe na tunaopenda kupata manufaa makubwa (more…)

2903; Muda wako ndiyo umekosa thamani kiasi hicho?

By | December 12, 2022

2903; Muda wako ndiyo umekosa thamani kiasi hicho? Kwako rafiki yangu mpendwa ambaye umekuwa unatumia muda kuokoa fedha. Unakuwa mwangalifu sana kwenye kila unachofanya ukiangalia mianya ya fedha kupotea au gharama kubwa kubwa. Katika uangalifu wako huo, umekuwa unaishia kutumia muda wako mwingi zaidi ili kuokoa kiasi hicho cha fedha. (more…)

2902; Mipango kabla na baada ya fedha.

By | December 11, 2022

2902; Mipango kabla na baada ya fedha. Kwako rafiki yangu mpendwa ambaye unakuwa na mipango mizuri kabla hujawa na fedha, ila ukishakuwa nazo mipango hiyo inayeyuka. Watu wamekuwa wanasema wazi kwamba wakiwa hawana fedha wanakuwa na mipango mizuri. Ila wakishazipata fedha wanasahau mipango hiyo mizuri. Wanazitumia mpaka zinaisha ndiyo wanakuja (more…)

2901; Orodha na pesa.

By | December 10, 2022

2901; Orodha na pesa. Kwako rafiki yangu mpendwa unayekuwa ‘bize’ kila siku lakini huoni hatua kubwa ambazo unazipiga. Unakuwa ‘bize’ kweli kweli siku nzima, unakuwa huna muda kabisa. Lakini ukiangalia matokeo unayozalisha, hayaonekani kabisa. Kwa sehemu kubwa, wengi tumerithi mfumo wa kazi unaotumika kwenye ajira nyingi rasmi. Kwenye ajira hizo, (more…)

2900; Sikitika nao, lakini usinunue matatizo yao.

By | December 9, 2022

2900; Sikitika nao, lakini usinunue matatizo yao. Kwako rafiki yangu mpendwa ambaye unapojaribu kujenga urafiki na wateja, wao wanajaribu kuutumia kujinufaisha binafsi. Wanatumia fursa hiyo kukueleza matatizo yao binafsi na kutaka uwakopeshe kile unachouza. Kibinadamu, ni mambo ambayo yanaumiza na unashawishika kutaka kuwasaidia watu wa aina hiyo. Hapo ndipo ninapotaka (more…)