2899; Njia haipotezi.

By | December 8, 2022

2899; Njia haipotezi. Kwako rafiki yangu mpendwa ambaye umekuwa unajaribu njia mbalimbali lakini hupati matokeo unayotaka. Ni rahisi kujiambia tatizo lipo kwenye njia. Kwamba njia hiyo siyo sahihi na inapoteza. Lakini huo siyo ukweli, tatizo halipo kwenye njia, bali lipo kwenye namna unavyofanyia kazi njia hiyo. Kwa mfano, njia ya (more…)

2898; Muda upo.

By | December 7, 2022

2898; Muda upo. Kwako rafiki yangu mpendwa unayelalamika kwamba unachokosa ni muda ndiyo maana unashindwa kufanya yale unayopaswa kutafanya. Hii ni sababu au kisingizio ambacho kila mtu huwa anakitumia. Moja ya misingi yangu ni kwamba chochote kinachofanywa na wengi, hakiwezi kuwa sahihi kwako kupata matokeo bora. Hivyo basi, inapokuja kwenye (more…)

2897; Sababu hazitauza.

By | December 6, 2022

2897; Sababu hazitauza. Kwako rafiki yangu mpendwa unayeshangaa kwa nini unashindwa kuuza licha ya juhudi kubwa unazoweka. Kinachokuzuia kuuza ni sababu nyingi unazokuwa nazo juu ya yale unayofanya au kushindwa kufanya. Unashindwa kukaa kwenye mchakato na kutekeleza viwango ulivyojiwekea. Badala ya kukubali uvivu na uzembe uliopelekea hayo, wewe unajipa sababu (more…)

2896; Kupata viroboto.

By | December 5, 2022

2896; Kupata viroboto. Kwako rafiki yangu mpendwa unayeshangaa kwa nini mambo yako huwa yanakwama licha ya juhudi kubwa unazoweka. Ipo kauli inayosema; ukilala na mbwa utaamka na viroboto. Hii inamaanisha kwamba watu unaojihusisha nao huwa wanakuambukiza yale waliyonayo. Hivyo kama utajihusisha na watu walio hasi na ambao wamekata tamaa, wanaoahirisha (more…)

2895; Hakuna asiyefukuzika.

By | December 4, 2022

2895; Hakuna asiyefukuzika. Kwako rafiki yangu mpendwa ambaye umeshaliona tatizo kwenye biashara yako, lakini unashindwa kulitatua kwa sababu unaona kuna watu hawagusiki. Unaona ukiwagusa wale ambayo ndiyo chanzo cha matatizo ambayo biashara inayapitia, basi biashara itatikisika sana. Hilo linakufanya uendelee kukumbatia uvivu na uzembe unaokusumbua sana. Nina mambo machache ya (more…)

2894; Uko bize kufanya nini?

By | December 3, 2022

2894; Uko bize kufanya nini? Kwako rafiki yangu mpendwa ambaye kila wakati uko bize kiasi cha kukosa muda wa kuyafanyia kazi yake mapya unayojifunza. Pamoja na kuwa kwako bize, hakuna matokeo makubwa na ya tofauti unayozalisha. Na hapo ndipo swali langu linapokuja, uko bize kufanya nini? Kama mambo yanayokuweka bize (more…)

2893; Vinavyofundishika na visivyofundishika.

By | December 2, 2022

2893; Vinavyofundishika na visivyofundishika. Kwako rafiki yangu mpendwa ambaye unajaribu kuwafundisha wafanyakazi wako lakini hawafundishiki. Kuna vitu huwa vinafundishika kwa watu kirahisi na kuna vitu ambavyo havifundishiki kirahisi. Jinsi ya kuifanya kazi ni kitu ambacho kila mtu anaweza kufundishwa. Na kama ataweka umakini kwenye hilo, ataweza kuelewa na kufanya vizuri. (more…)

2892; Dikteta Mwema.

By | December 1, 2022

2892; Dikteta Mwema. Kwako rafiki yangu mpendwa ambaye umejaribu kuwapa wafanyakazi wako kile wanataka lakini bado hawakupi matokeo unayotaka. Wakati Elon Musk anainunua kampuni ya twitter, wengi hawakujua nini kinaenda kutokea. Waliona ni kama mzaha tu na kudhani hilo halitafanikiwa. Alipokamilisha manunuzi na kumfukuza mkurugenzi mkuu na yeye kushika nafasi (more…)

2891; Chipsi Mayai.

By | November 30, 2022

2891; Chipsi Mayai. Kwako rafiki yangu mpendwa ambaye unashangazwa na mvurugano unaojitokeza wakati wa mabadiliko. Mabadiliko yoyote yale huwa yanaambatana na hali ya mvurugano. Hakuna mabadiliko yenye utulivu. Mabadiliko ni sawa na kuandaa chipsi mayai, lazima uyavunje mayai. Kuyavunja mayai inaweza kuonekana kama ni kutaharibu, lakini chipsi zinapokuwa tayari, hilo (more…)

2890; Wanadhani wana akili kuliko wewe.

By | November 29, 2022

2890; Wanadhani wana akili kuliko wewe. Kwako rafiki yangu mpendwa ambaye wafanyakazi wako wanakataa viwango vipya unavyoanzisha. Una kiu kubwa ya kujenga na kukuza biashara yako. Unataka kujenga mfumo wa biashara, uwe na timu bora na ufanye mauzo makubwa. Unaingia gharama ya kupata maarifa na mafunzo sahihi ya kukamilisha hilo. (more…)