3235; Wape kile wanachotaka.

By | November 9, 2023

3235; Wape kile wanachotaka. Rafiki yangu mpendwa,Kitu kimoja kikubwa sana ambacho naendelea kujifunza kwenye biashara ni kwamba ukitumia akili nyingi sana, unaishia kushindwa. Yaani kadiri unavyokazana kuchambua na kupangilia biashara kwa akili kubwa, ndivyo unavyozidi kuipoteza na hata kupelekea ife. Kanuni kuu ya mafanikio kwenye maisha ni kupata unachotaka, wape (more…)

3234; Hamasa na Nidhamu.

By | November 8, 2023

3234; Hamasa na Nidhamu. Rafiki yangu mpendwa,Hamasa na nidhamu ni viungo muhimu sana kwenye mafanikio yoyote makubwa kwenye maisha.Hivi visipokuwepo, ni vigumu sana mtu kuweza kuvuka vikwazo mbalimbali vilivyopo kwenye safari ya mafanikio. Lakini kwa bahati mbaya sana, hivyo pia ni vitu ambavyo haviwezi kufundishwa, kuuziwa wala kulazimishwa.Hivi ni vitu (more…)

3233; Usiseme, onyesha.

By | November 7, 2023

3233; Usiseme, onyesha. Rafiki yangu mpendwa,Hii dunia haijawahi kuishiwa wasemaji.Kila mtu anaweza kusema, kwa kupanga na kuahidi mambo mengi.Lakini inapokuja kwenye ufanyaji, kuna uhaba mkubwa wa watu.Ni watu wachache sana ambao ni wafanyaji kweli kwenye kile wanachotaka. Kila mtu anataka mafanikio makubwa na utajiri.Kila mtu anataka kuwa na maisha mazuri.Lakini (more…)

3232; Umepanga kulipaje?

By | November 6, 2023

3232; Umepanga kulipaje? Rafiki yangu mpendwa,Tunajua kwamba hakuna kitu cha bure.Kwa chochote kile tunachotaka kwenye maisha, huwa kuna gharama ambayo lazima tuilipe. Zipo njia mbili za kulipa gharama ya kupata kile tunachotaka. Njia ya kwanza ni kulipa kwa fedha.Hapa unatoa fedha na kuwalipa wale ambao wanakusaidia kupata kile unachotaka.Njia hii (more…)

3231; Ugumu na ubora.

By | November 5, 2023

3231; Ugumu na ubora. Rafiki yangu mpendwa,Ugumu wa kupata kitu na ubora wake ni vitu ambavyo vinaendana.Kadiri kitu kinavyokuwa kigumu kupatikana ndivyo pia kinavyokuwa bora.Na kitu ambacho ni rahisi kupatikana, huwa pia siyo bora. Hivyo pia ndivyo ilivyo kwa watu unaojihusisha nao.Kadiri inavyokuwa rahisi kwa watu kujihusisha na wewe, ndivyo (more…)

3230; Ni kwa sababu bado hujapata ushindi.

By | November 4, 2023

3230; Ni kwa sababu bado hujapata ushindi. Rafiki yangu mpendwa,Kuna juhudi nyingi na kubwa unazokuwa unaweka kwenye yale unayofanya.Lakini kwa sababu bado hujazalisha matokeo yanayoonekana, wengi watapuuza juhudi zako. Tena wapo ambao watakuona kama umechanganyikiwa kwa hayo unayofanya. Ni mpaka pale unapoweza kuzalisha matokeo makubwa na ya tofauti ndiyo kila (more…)

3229; Usivyoweza kununua.

By | November 3, 2023

3229; Usivyoweza kununua. Rafiki yangu mpendwa,Kuna vitu vingi ambavyo unaweza kuwalipa watu na wakakusaidia kwa namna ambayo unarahisisha na kuharakisha matokeo. Unaweza kuwalipa watu wakufundishe na kukuonyesha kile unachopaswa kukifanya. Unaweza kuwalipa watu wakusaidie kwenye kufanya kile unachopaswa kufanya na ukaweza kuzalisha matokeo makubwa zaidi. Hivyo ndivyo ukuaji mkubwa huwa (more…)

3228; Waelewe watu.

By | November 2, 2023

3228; Waelewe watu. Rafiki yangu mpendwa,Tunaweza kusema kitu kimoja kwa uhakika kwamba biashara ni watu. Kila kitu tunachofanya kwenye biashara kinahusisha watu. Kila tunachofanya kwenye biashara, ni kupitia watu na kwa ajili ya watu. Yaani tunawatumia watu kufanya vitu kwa ajili ya watu. Hivyo basi, kama tunataka kupata mafanikio makubwa (more…)

3227; Kupigiwa makofi.

By | November 1, 2023

3227; Kupigiwa makofi. Rafiki yangu mpendwa,Sisi binadamu kama viumbe wa kijamii huwa tunapenda sana kukubalika na wengine kwenye chochote tunachofanya. Pale wengine wanapotusifia na kutupigia makofi kwenye kile tunachofanya ndiyo tunaona tunafanya kitu sahihi. Lakini ukweli ni kwamba hakuna yeyote aliyewahi kufanya makubwa ambaye alikubalika na kusifiwa mwanzoni.Wote walionekana kama (more…)

3226; Biashara ambayo upo.

By | October 31, 2023

3226; Biashara ambayo upo. Rafiki yangu mpendwa,Kwenye harakati zetu za kupata mafanikio tunayoyataka, huwa tunahangaika na mambo mengi sana. Kwa sababu tunakuwa tunayataka sana matokeo na kwa haraka, huwa tunaona kama tumechelewa sana.Hivyo tunakazana kuharakisha kwa kuhangaika na mambo mengi. Kila fursa ambayo tunaiona au kuisikia tunaiendea kwa kuona hiyo (more…)