Tag Archives: FIKRA TOFAUTI

Nikiwa Mkubwa Nataka Kuwa Muosha Magari.

By | March 3, 2015

Katika pita pita zangu kwenye mtandao nimekutana na habari moja ambayo Mh January Makamba alishirikisha watu. Alikutana na watoto wa mtaani, mmoja anasoma mwingine hasomi. Alimuuliza yule asiyesoma akiwa mkubwa anataka kuwa nani, yeye akajibu anataka kuwa muosha magari. Habari nzima ni ya kusikitisha, kwa sababu watoto hawa wana maisha (more…)

Hakuna Kitu Chenye Maana…

By | January 30, 2015

Hakuna kitu chenye maana duniani, Ila sisi wenyewe ndio tunavipa vitu maana. Ukiweza kulijua hili, utajipunguzia matatizo mengi sana. Kwa mfano kama unaona dhahabu ina maana, kuliko shaba, kumbuka vyote hivi ni madini ambayo yanapatikana kwenye ardhi. Tumeweka maana kubwa kwenye dhahabu kwa sababu haipatikani kirahisi kama shaba. Kama nyama (more…)

Nafasi Ya Wewe Kuwa Bora Kila Siku… NA ZAWADI YA TSH 365,000/=

By | January 29, 2015

Kama mpaka sasa huna utaratibu wa kujifunza kila siku, tayari upo nyuma sana katika kufikia mafanikio kwenye jambo lolote unalofanya kwenye maisha yako. Kujifunza kila siku ni hitaji la chini sana la wewe kuweza kufikia mafanikio. Na tunaposema kujifunza kila siku ni kila siku kweli, jumatatu mpaka jumapili na kurudia (more…)

KAWAIDA Ni Tafsida Ya HOVYO…

By | January 29, 2015

Huwa tuna utaratibu wa kupunguza ukali wa maneno, kwa kiswahili tunaita tafsida. Yaani badala ya kusema mtu amezaa tunasema amejifungua, japokuwa yote ni yale yale tu, ila kujifungua linapunguza ukali wa uhalisia wenyewe. Maneno kama kujisaidia, kufanya tendo la ndoa na mengine mengi ni maneno mazuri yanayotumika badala ya maneno (more…)

Unataka Kuiona Dunia? Vua Miwani…

By | January 27, 2015

Unachokiona sasa hivi sio dunia halisi, bali ni dunia unayotaka kuiona wewe. Hii ni kwa sababu kila mtu ni kama amevaa miwani yake ambayo inamuonesha kile anachotaka kuona. Umewahi kuvaa miwani ya rangi? Unaonaje kitu unapokiangalia? Je unaonaje kitu kile unapovua miwani? Hiko ndio kinachotokea kweye maisha yako ya kila (more…)

Naomba Ufanye Changamoto Hii Ya Siku Kumi, Utabadili Sana Maisha Yako.

By | January 19, 2015

Binadamu tunapenda kulalamika sana na hata kuwalaumu wengine. Hakuna mtu anayependa aonekane kwamba yeye ndio amechangia kusindwa kwa jambo fulani. Hivyo katika jambo lolote lile linalotokea watu hukimbilia kumtafuta mchawi, yaani mtu wa kulaumu. SOMA; Haya Ni Maajabu Ya Dunia Ambayo Unayafanya Kila Siku. Sasa kwa tabia hii ya kulalamika (more…)

Haya Ni Maajabu Ya Dunia Ambayo Unayafanya Kila Siku.

By | January 17, 2015

Dunia ina maajabu mengi sana, na sehemu kubwa ya maajabu hayo hayapo mbali sana kwani unayafanya wewe mwenyewe kwenye maisha yako kila siku. Ni maajabu kwa sababu haiingii akilini unawezaje kufanya mambo hayo kwenye maisha yako na huku ukishindwa kufanya mengine ya muhimu zaidi kwenye maisha yako. Unaweza kupanga kikosi (more…)

Kauli Mbili Za Kuacha Kutumia Leo, Maana Zinaashiria Kushindwa.

By | January 14, 2015

Kuna kauli nyingi ambazo watu wengi hupenda kutumia. Katika kauli hizi kuna ambazo hutusukuma mbele na kutufanya tufikie malengo yetu. Pia kuna kauli nyingine zinaashiria kushindwa na kukata tamaa. Kauli hizi zinaweza kukuzuia kufikia mafanikio makubwa. Zifuatazo ni kauli mbili za kuacha kutumia leo ili kuweza kifikia malengo yako. 1. (more…)

Ni Nini Hasa Kinakuzuia Mpaka Sasa?

By | January 12, 2015

Huenda malengo uliyoweka mwaka huu uliweka pia mwaka jana, na mwaka mwingine kabla ya mwaka jana. Umekuwa ukiweka malengo hayo hayo na muda mfupi unayasahau. Unaanza mwaka kwa shauku… Mwaka huu nitaanza kufanya mazoezi… Mwaka huu nitaacha ulevi… Mwaka huu nitaanzisha biashara… Mwaka huu nitaboresha maisha yangu. Ila mwezi wa (more…)