Tag Archives: KURASA 365 ZA MWAKA 2015

UKURASA WA 88; Usinunue Matatizo Ya Watu.

By | March 29, 2015

Binadamu ni viumbe wa kujumuika, yaani tunaishi vizuri kwenye jamii, kwa kusaidiana hapa na pale. Lakini katika kusaidiana huku kuna wakati ambapo tunatoa msaada ambao unatuumiza sana sisi na pia haumsaidii sana yule ambaye tunampatia. Msaada huu ni pale ambapo unanunua matatizo yya mtu. SOMA; Tabia Hizi Zitakusaidia Sana Kufikia (more…)

UKURASA WA 87; Kuna Jambo Moja La Ziada La Kufanya.

By | March 28, 2015

Inapokuja kwneye kazi, biashara au jambo lingine tunalofanya ili kutengeneza kipato, mara zote huwa kuna kuwa na jambo moja la ziada la kufanya. Kwa mfano kama umesema leo utafanya vitu fulani vitatu, utakapomaliza kufanya vitu hivyo utaona kuna kitu kingine cha ziada cha kufanya. SOMA; Tabia Hizi Zitakusaidia Sana Kufikia (more…)

UKURASA WA 86; Jifunze Kusikiliza.

By | March 27, 2015

Tuna masikio mawili na mdomo mmoja kwa sababu moja kubwa sana. Kusikiliza ni bora kuliko kuongea. Yaani unahitaji kusikiliza mara mbili ya unavyoongea. Lakini kwenye maisha yetu ya kawaida mambo ni kinyume kabisa na hapo. Watu wanaongea mara mbili ya wanavyosikiliza. Kila mtu anakazana kuongea na mwishowe hakuna tena mazungumzo (more…)

UKURASA WA 85; Jipe Miadi.

By | March 26, 2015

Kwa mfano ukataka kuonana na mimi ili tuzungumze jambo lolote, tutawekeana miadi. Kwamba siku fulani na muda fulani tutakuwa pamoja tukizungumzia jambo fulani. Na tunapokutana hatutegemei kuwa na usumbufu mwingine wowote, ni mimi na wewe. Nikikupigia simu sasa hivi, utaacha jambo lolote ambalo unafanya na kujibu simu hiyo, hata kama (more…)

UKURASA WA 84; Pata Muda Wa Kuishi.

By | March 25, 2015

Kwa masikitiko makubwa sana naomba kukuambia kwamba bado hujapata muda wa kuishi. Na kama hutachukua hatua mapema basi utajikuta mpaka siku unakufa hujapata muda wa kuishi. Kuna usemi maarufu unasema kwamba maisha ni kile kinachoendelea wakati wewe unaweka mipango mingine. SOMA; KITABU; Jinsi Ya Kufaidika Na Mabadiliko Yanayotokea Kwenye Maisha. (more…)

UKURASA WA 83; Unahitaji Kuwa Sahihi Au Kuwa Na Furaha?

By | March 24, 2015

Kuwa sahihi na wakati huo huo kuwa na furaha ni kama vitu viwili ambavyo haviwezi kutokea kwa wakati mmoja. Na hii ni sahihi sana hasa kwenye maisha yako na mahusiano yako na watu wengine. Ni vigumu sana wewe kuonesha kwamba upo sahihi na wakati huo huo ukawa na furaha. Hii (more…)

UKURASA WA 81; Achana Na Ubishi, Hautakusaidia Lolote.

By | March 22, 2015

Ukishaamua ni kitu gani ambacho unataka kufanya kwenye maisha yako, basi hapo ndio unafunga mjadala. Usijiingize kwenye ubishi kuhusiana na kile unachofanya. Kama umeshaamua kwamba wewe utakuwa mjasiriamali, anza kufanya ujasiriamali, jua kabisa mpaka unakufa wewe utakuwa mjasiriamali. Kuanza kuingia kwenye ubishi kama mjasiriamali anazaliwa au anatengenezwa hakutakusaidia lolote. Kuanza (more…)

UKURASA WA 80; Utabiri Mzuri Wa Kesho.

By | March 21, 2015

Je unahitaji mtu wa kukusaidia kuitabiri vizuri kesho yako? Huna haja ya kwenda kwa wapiga ramli au watabiri wa nyota, kwani mtabiri bora kabisa tayari upo nae hapo ulipo. Mtabiri huyo ni wewe mwenyewe. Unafikiria kama biashara unayofanya itakuletea mafanikio makubwa baadae? Unafikiria kama kazi unayofanya utadumu nayo kwa muda (more…)

UKURASA WA 79; Usitegemee Nyundo Tu, Kuna Zana Nyingine Pia.

By | March 20, 2015

Wenye busara walipata kusema maneno haya mazuri sana; Kama zana pekee uliyonayo ni nyundo, basi kila kinachokuja mbele yako kitaonekana kama msumari. Umeielewa vizuri kauli hiyo? Kama hujaielewa tafuta mtoto mdogo halafu mpe nyundo akae nayo tu na uone atakuwa anafanya nini. Atagonga kila kitu. SOMA; Hivi Ndivyo Unavyoweza Kuwa (more…)

UKURASA WA 78; Hiki Ndio Kitu Unachoweza Kufanya, Bila Ya Kujali Uwezo Wako.

By | March 19, 2015

Jambo moja la kushangaza kwetu binadamu ni kwamba kuna vitu ambavyo tunaweza kufanya na kuna vitu ambavyo hatuwezi kufanya. Vitu ambavyo tunaweza kufanya ni vile vitu ambavyo tumekuwa tunafanya kila siku, au tunaona watu wengine wakiwa wanavifanya. Hii inatupa imani kwmaba vinawezekana kufanyika na tunaweza kuvifanya bila ya tatizo. SOMA; (more…)