Tag Archives: KURASA 365 ZA MWAKA 2015

UKURASA WA 57; Dunia Haina Usawa…

By | February 26, 2015

Kuna wakati ambao utafanya kila unachotakiwa kufanya na kusubiri upate matokeo uliyotegemea kupata ila huyapati. Unafanya kila kilicho ndani ya uwezo wako, unakazana sana kuhakikisha mambo yote yanakwenda sawa ila mwisho wa siku hupati kile ulichotarajia kupata. Unapata kilicho tofauti kabisa, au hupati kabisa, au unaishia kupoteza kabisa. SOMA; Mwalimu (more…)

UKURASA WA 56; Unajaribu Kumdanganya Nani?

By | February 25, 2015

Unajua kwamba maisha yako ni yako, na wewe mwenyewe ndio utaishi maisha hayo mpaka utakapokufa, sasa unajaribu kumdanganya nani? Unajua kabisa kwamba kazi unayofanya huifurahii, kipato unachopata hakikutoshi, lakini unapokuwa na watu unakazana uonekane unafanya kazi muhimu, na inakupa kipato cha kutosha, unajaribu kumdanganya nani? SOMA; UKURASA WA 18; Hakuna (more…)

UKURASA WA 55; Usikubali Kirahisi…

By | February 24, 2015

Maisha yako hivi, unaweza kuwa unahitaji kitu fulani na ili kupata kitu hiko inabidi umwombe mtu mwingine. Unapoendakumwomba mtu huyo anakupa jibu rahisi, HAPANA, HAIWEZEKANI. Wewe unachofanya ni nini? Unakubali, unarudi nyuma na kuwa shahidi mzuri, kwamba ulijaribu sana, lakini haikuwezekana, uliambiwa hapana, uliambiwa haiwezekani. Hapo ndio unapokosea, unakubali kirahisi, (more…)

UKURASA WA 54; Kufa MTUPU….

By | February 23, 2015

Moja ya njia zitakazokuwezesha kufanya kazi iliyobora kwa wakati ambao bado unaishi hapa duniani ni kupanga kufa MTUPU. Kwa lugha ya kiingereza tunasema DIE EMPTY. Kila mmoja wetu amezaliwa na mziki mzuri sana ambao upo ndani yake. Lakini ni wachache sana ambao wanaweza kuimba mziki huu. Na ninaposema mziki simaanishi (more…)

UKURASA WA 53; Hakuna Kinachodumu Milele…

By | February 22, 2015

Moja ya siri kubwa unayopaswa kuijua ili kupata uhuru kwenye maisha ni kwamba hakuna kinachodumu milele. Kama vile ambavyo sisi binadamu hatutadumu milele, siku moja utafikia mwisho, utakufa. Ndivyo ilivyo kwa kila kitu kwenye maisha, kuna wakati kitafika mwisho. SOMA; Hiki Ndio Kitakachotokea Miaka 100 Ijayo.. Matatizo uliyonayo hayatadumu milele, (more…)

UKURASA WA 52; Epuka Miluzi Mingine…

By | February 21, 2015

Waswahili wanasema miluzi mingi humpoteza mbwa. Hii sio kweli kwambwa tu, ni kweli hata kwa sisi binadamu. Kelele nyingi zitakupoteza, achana nazo. Dunia ina kelele nyingi sana, ambazo unaweza kutamani kuzifuatilia, kujua zaidi kuhusu kelele hizo. Ila huu wote ni upotevu wa muda, kelele hizi hazina msaada wowote kwa wewe (more…)

UKURASA WA 51; Uadilifu, Kioungo Muhimu Cha Kufikia Mafanikio.

By | February 20, 2015

Viungo vingine muhimu sawa na uadilifu ni KUFANYA KAZI KWA BIDII NA MAARIFA na UAMINIFU. Ukibonyeza hizo hapo chini unajifunza zaidi kuhusu viungo hivyo viwili. SOMA; UKURASA WA 06; Kazi Ndio Msingi Wa Maendeleo. SOMA; UKURASA WA 38; Uaminifu, Kitu Muhimu Kitakachokuwezesha Kupata Unachotaka. Uadilifu ni kiungo muhimu sana cha (more…)

UKURASA WA 50; Njia Mbili Za Kukuondolea Matatizo Yako Ya Kifedha.

By | February 19, 2015

Tunaweza kusema matatizo yote duniani chimbuko lake ni fedha. Au kama sio yote basi sehemu kubwa ya matatizo inaanza na matatizo ya fedha. Sina haja ya kurudia hapa kusema kwa nini fedha ni muhimu, kila mtu anajua na ndio maana tunaitafuta kwa nguvu. Pamoja na kufanya kazi kwa juhudi na (more…)

UKURASA WA 49; Uelekeo Ni Muhimu Kuliko Mwendo Kasi..

By | February 18, 2015

Kama hujui unakokwenda, kuongeza mwendo hakutakufikisha unakotaka kufika. Kuongeza mwendo kutazidi kukupoteza, kukupeleka mbali zaidi na huenda ukawa mbali zaidi na unakotaka kufika. Hivyo jukumu lako kubwa kwenye maisha sio kuongeza mwendo bali kujua kwanza unakokwenda ni wapi. SOMA; Sababu 5 Kwa Nini Ni Marufuku Wewe Kukata Tamaa. Ukishajua unakokwenda (more…)

UKURASA WA 48; Ni Marufuku Kubadili Lengo…

By | February 17, 2015

Kuna usemi unakwenda, ujinga ni kufanya jambo lile lile na kw anjia ile ile halafu ukategemea majibu tofauti. Yaani kama unalima shamba lako na unapanda mbegu fulani na kutumia mbolea fulani na ukanyeshea vizuri, kama usipopata mazao mazuri, hata wakati mwingine ukilima hivyo hivyo utapata kama ulivyopata. SOMA; UKURASA WA (more…)