Tag Archives: KURASA 365 ZA MWAKA 2015

UKURASA WA 47; Kuwa Na Subira, Hakuna Unachopoteza.

By | February 16, 2015

Wenye busara walisema; haraka haraka haina baraka. Hawakuishia hapo, waksema tena, pole pole ndio mwendo. Lakini dunia ya sasa inatufanya tuone tuna busara zaidi, kwamba hatuna muda wa kusubiri, nataka hiki na nakitaka sasa hivi. Huku ni kujidanganya. Kwa sababu mwaka huu 2015 umeamua kubadili maisha yako haimaanishi utaanza kuona (more…)

UKURASA WA 46; Kuwa Mtaalamu Uliyebobea..

By | February 15, 2015

Katika fani yoyote ile, watu wanaolipwa sana au wanaopata kipato kikubwa ni wale ambao ni wataalamu sana na waliobobea. Hawa ni watu ambao wamechagua kufanya kitu na kujifunza kuhusu kitu hiko nje ndani. Wanajua mbinu zote za kuweza kufanya kazi iliyobora na wakitoa kazi yao kila mtu anaifurahia na kuipenda. (more…)

UKURASA WA 45; Uwekezaji Muhimu Kwako Kufanya Na Unaolipa Sana.

By | February 14, 2015

Kila mtu anatafuta fursa nzuri sana ya kuwekeza. Watu wanafikiria ni biashara gani nzuri wakifanya watapata faida kubwa. Wengine wanafikiria ni kilimo gani wakifanya watapata faidia na kufikia mafanikio. Wengine wanafikiria ni hisa za kampuni gani wakinunua watapata faida kubwa. Yote haya yatawezekana kama utafanya uwekezaji wa msingi sana ambao (more…)

UKURASA WA 44; Usiondoe Macho Kwenye Zawadi…

By | February 13, 2015

Vikwazo ni kile unachokiona pale unapoondoa macho yako kwenye malengo yako. Kauli hii ni ya kweli kabisa. Unapoacha kuangalia kile unachotaka, unapoacha kuweka msisitizo kwenye kile unachotaka kupata ndio unaanza kuona vikwazo, ndio unapoanza kuona changamoto na ndio unapoanza kupata mawazo ya kukata tamaa. Kama kweli unataka kupata unachotaka, fanya (more…)

UKURASA WA 43; Ushauri Wa Bure Una Gharama Kubwa.

By | February 12, 2015

Ushauri wa bure hauna gharama mpaka pale utakapoanza kuutumia. Siku hizi kila mtu anajua kutoa ushauri, kuwa makini sana kabla hujatumia ushauri wowote unaopewa. Hasa ushauri unaotolewa na kila mtu. Kuna maneno rahisi ya mtaani utasikia biashara fulani inalipa kweli, fulani kaanza kuifanya na sasa hivi yuko vizuri. Au utasikia (more…)

UKURASA WA 42; Usitafute Sababu, Chukua Hatua…

By | February 11, 2015

Katika jambo moja ambalo tunaweza kukubaliana wote ni kwamba kwa chochote unachofanya ni lazima utakutana na changamoto. Kama tulivyowahi kujifunza, kitu pekee ambacho tuna uhakika nacho ni kutokuwa na uhakika. Unapanga vizuri jinsi biashara yako itakuletea faida, unaishia kupata hasara. Unapanga vizuri jinsi utafanya kilimo chako na upate mazao mazuri (more…)

UKURASA WA 42; Usitafute Sababu, Chukua Hatua…

By | February 11, 2015

Katika jambo moja ambalo tunaweza kukubaliana wote ni kwamba kwa chochote unachofanya ni lazima utakutana na changamoto. Kama tulivyowahi kujifunza, kitu pekee ambacho tuna uhakika nacho ni kutokuwa na uhakika. Unapanga vizuri jinsi biashara yako itakuletea faida, unaishia kupata hasara. Unapanga vizuri jinsi utafanya kilimo chako na upate mazao mazuri (more…)

UKURASA WA 41; Usisubiri Ukamilifu…

By | February 10, 2015

Moja ya kitu kinachowazuia wengi kufikia mafanikio ni kutaka UKAMILIFU. Wanataka kuwa wakamilifu kwa kile wanachofanya. Wanataka kila kitu kiwe tayari kabla ya kuanza. Na wanataka wanachofanya kiwe kwa ukamilifu. Lakini kwa bahati mbaya sana hakuna aliye mkamilifu. Hakuna wakati ambapo kila kitu kitakuwa tayari kwa ajili ya wewe kuanza (more…)

UKURASA WA 40; Amua Kuwa Wewe…

By | February 9, 2015

Duniani kuna watu zaidi ya bilioni saba. Lakini katika watu wote hawa, hakuna aliyefanana na wewe moja kwa moja. Ulivyo wewe, uko wewe tu dunia nzima. Hajawahi kuwepo kama wewe na hatakuja kuwepo mwingine kama wewe. SOMA; Fikra TANO Zinazoua Mafanikio Na Jinsi Ya Kuziepuka. Sasa kwanini unahangaika kuwa kama (more…)

UKURASA WA 39; Jitengenezee Bahati Yako Mwenyewe…

By | February 8, 2015

Kuna watu wana bahati eh!! Unamuona mtu anaanza kazi, mara anapandishwa cheo na unamuona akiwa na kipato kikubwa kuliko wewe ambaye umekuwa kwenye kazi hiyo kwa muda mrefu. Unamuona mtu anaanza biashara na baada ya muda anapata faida kubwa kuliko wewe ambaye umekuwa kwenye biashara hiyo kwa muda mrefu. Unaishia (more…)