Tag Archives: KURASA 365 ZA MWAKA 2015

UKURASA WA 38; Uaminifu, Kitu Muhimu Kitakachokuwezesha Kupata Unachotaka.

By | February 7, 2015

Kwa mfano akaja mtu kwako akakuambia ana shida na anahutaji tsh laki moja ili akafanye mambo yake muhimu na atakurejeshea. Mtu huyu humfahamu kabisa, je utatoa fedha hiyo na kumpatia? Vipi akaja mtu mwingine ambaye ulishasikia habari zake kwamba akipewa fedha anarudisha. Au huenda ulishampa fedha kipindi cha nyuma na (more…)

UKURASA WA 37; Sababu Ya Wewe Kutenda Wema…

By | February 6, 2015

Usitende wema kwa sababu dini inakuambia ufanye hivyo, ukitumia kigezo cha dini, kuna mazingira yanaweza kukupa nafasi ya kutokutenda wema. Usitende wema kwa sababu unataka watu wakuone, ukitumia sababu hii utafanya mambo mabaya ukiwa kwenye kificho. Usitende wema kwa sababu unayemtendea ni mtu unayemheshimu au kumuonea aibu, ukitumia sababu hii (more…)

UKURASA WA 36; Mafanikio Sio Kitu Kimoja.

By | February 5, 2015

Japokuwa kila mtu ana maana yake ya mafanikio, bado mafanikio si kitu kimoja hata kwa huyo mtu mmoja. Kwa mfano tuseme wewe maana yako ya mafanikio ni kuishi kwenye nyumba ya kifahari ufukweni, kuendesha gari la kifahari na kuwa na bilioni moja kama akiba. Sasa mafanikio sio pale unapokuwa na (more…)

UKURASA WA 35; Usijaribu Kumfurahisha Kila Mtu.

By | February 4, 2015

Kama umewahi kusikia hadithi moja ambapo mtu na mke wake walikuwa wanasafiri jangwani na wameoanda ngamia. Wakapishana na watu ambao walisema watu hawa wana roho mbaya sana, wanampanda ngamia mmoja watu wawili? Waliposikia vile, mwanaume akamwambia mke wake ashuke na atembee kwa miguu, yeye akabaki amepanga. Walikutana na watu wengine (more…)

UKURASA WA 34; Jali Mambo Yako.

By | February 3, 2015

Katika wakati wowote ule na popote ulipo kuna mambo mengi sana yanayoendelea. Kama utataka kujali kila kitu utashindwa kufikia mafanikio makubwa. Kama utataka kujua kila kitu kinachoendelea, nani kafanya nini, utakuwa unajali mabo mengine na mambo ya watu wengine na kujinyima muda wa kufuatilia mambo yako. Kumbuka tulivyosema kwenye kuweka (more…)

UKURASA WA 33; Tengeneza Mtandao Wako Wa Mafanikio.

By | February 2, 2015

Ukweli ni kwamba hakuna mtu anayeweza kufanya kila kitu yeye mwenyewe. Na hata kwenye mafanikio, hakuna mtu ambaye anaweza kusema amefikia mafanikio yeye mwenyewe kwa nguvu zake mwenyewe tu. Ili kufikia mafanikio unahitaji ushirikiano wa watu wengi sana. Ni muhimu sana kutengeneza mtandao ambao utakufikisha kwenye mafanikio. Shirikiana na watu (more…)

UKURASA WA 32; Mambo Yanapokuwa Magumu…

By | February 1, 2015

Mambo yanapokuwa magumu, huu ni uhakika, yatakuwa magumu, unafanya nini? Umeshaweka malengo na mipango yako vizuri. Umeshajitoa kufanya kazi kwa bidii na maarifa. Umekazana kwa juhudi zako zote, umekuwa mvumilivu lakini mambo hayae kabisa, huoni mabadiliko yoyote. Unafanya nini? Unakubali kwamba lengo hili haliwezekani na hivyo unaachana nalo? Kosa kubwa (more…)

UKURASA WA 31; Umetoka Wapi, Upo Wapi Na Unaelekea Wapi?

By | January 31, 2015

Ili kufikia mafanikio makubw akwenye maisha yako ni lazima uwe na njia ya kuweza kujipima. Ni lazima uweze kujipima kama kweli upo kwenye njia sahihi ya kukufikisha kwenye mafanikio. Ni muhimu sana kujua unakotoka, hii itakufanya ujue ni kazi kiasi gani unahitaji kufanya ili kufika unakotaka. Ni muhimu pia kujua (more…)

UKURASA WA 30; Nenda Hatua Ya Ziada…

By | January 30, 2015

Mafanikio yana upendeleo mmoja, yanaenda kwa watu ambao wanafanya mambo kwa ubora wa hali ya juu sana. Hawa ni watu wameamua kwenda hatua ya ziada kwenye jambo lolote wanalofanya. Hawakubali tu kufanya kama kila mtu anavyofanya. Watu hawa wanajua unapokwenda hatua ya ziada unajijengea nafasi kubwa ya kufikia mafanikio makubwa. (more…)

UKURASA WA 29; Kitu Pekee Unachoweza Kuwa Na Uhakika Nacho…

By | January 29, 2015

Kitu pekee unachoweza kuwa na uhakika nacho ni kutokuwa na uhakika. Hujanielewa? Tumia mifano hii; Unapanga kwamba utakwenda kwenye mkutano, umeambiwa mkutano utaanza saa sita na kumalizika saa nane. Wewe unapanga baada ya mkutano wa saa nane, saa nane na nusu utakutana na mtu muhimu sana. Unapanga mambo yako vizuri (more…)