Tag Archives: KURASA 365 ZA MWAKA 2015

UKURASA WA 28; Kwa Nini Nisiwe Mimi…

By | January 28, 2015

Kama kuna watu ambao walianzia chini sana na leo wana mafanikio makubwa, kwa nini nisiwe mimi? Kama kuna watu ambao hawakupata elimu kubwa ila wameweza kuleta mabadiliko makubwa, kwa nini nisiwe mimi? Kama kuna watu ambao wametoka familia za kimasikini kabisa ila leo wameweza kutengeneza biashara kubwa, kwa nini nisiwe (more…)

UKURASA WA 27; Jaribu Mambo Mapya…

By | January 27, 2015

Kama unafanya kile ambacho kila siku unafanya, utapata matokeo ambayo kila siku uayapata. Kama kuna kitu kipya ambacho unataka kupata, unahitaji kujaribu kufanya mambo mapya. Kufanya mambo mapya sio kitu rahisi, inahitaji ujasiri wa kuweza kujihoji na kudhubutu kuchukua. Hii ni kwa sababu binadamu hatupendi mabadiliko. SOMA; Kozi 1100 Unazoweza (more…)

UKURASA WA 26; Lazima Kuna Atakayekuwa Zaidi Yako.

By | January 26, 2015

Katika jambo lolote unalofanya kwenye maisha, lazima kuna mtu ambaye anafanya zaidi yako. Kama ni biashara kuna ambaye atakuwa anafanya zaidi yako. Kama ni kazi kuna ambaye atakuwa anafanya zaidi yako. SOMA; Mambo Matatu Muhimu Ya Kufanya Siku Ya Jumapili Ili Kuwa Na Wiki Yenye Mafanikio Ukinunua gari utakutana na (more…)

UKURASA WA 25; Hakuna Njia Ya Mkato…

By | January 25, 2015

Akija mtu na kukuambia kuna njia ya mkato ya kufikia mafanikio, kimbia haraka sana na usiendelee kusikiliza. Maana ukiendelea kusikiliza unaweza kujikuta umeshaanza kushawishika. Hakuna nia ya mkato ya kufikia mafanikio, na kama ipo mafanikio utakayoyapata hayatadumu. SOMA; Sheria 12 Kwa Wanaoanza Biashara Kutoka Kwa Bilionea Mark Cuban. Kila kitu (more…)

UKURASA WA 24; Kila Kitu Kina Gharama…

By | January 24, 2015

Mtu mmoja mwenye mafanikio aliwahi kuulizwa ni ipi siri ya mafanikio ambayo unaweza kumshauri mtu yeyote na yeye akafanikiwa? Mtu yule alijibu ili kuwa na mafanikio kwenye maisha, bila ya kujali unaanzia wapi unahitaji vitu viwili; 1. Kujua ni nini unataka. 2. Kujua gharama unayotakiw akulipa na kuwa tayari kuilipa. (more…)

UKURASA WA 23; Pata Muda Wa Kupumzika…

By | January 23, 2015

Kijana mmoja alikwenda kwa mtu aliyefanikiwa kumuomba ushauri. Kijana; Naomba uniambie itanichukua muda gani kufikia mafanikio makubwa kwa hiki ninachofanya? Mshauri; Itakuchukua miaka kumi. Kijana; Nipo tayari kufanya kazi usiku na mchana, je itanichukua muda gani? Mshauri; Miaka ishirini. Ukweli ni kwamba katika safari yetu ya kufikia mafanikio tunaweza kufikiri (more…)

UKURASA WA 22; Usiogope Kufanya Makosa…

By | January 22, 2015

Katika maisha, kazi na hata biashara kuna kitu kimoja ambacho tuna uhakika nacho. Kitu hiko ni kwamba ni lazima utafanya makosa. Hata uwe umejiandaa kwa kiasi gani, hata uweke mambo vizuri kiasi gani bado utafanya makosa. Hii ni kwa sababu hakuna mtu aliyezaliwa na kitabu cha matumizi kwamba maisha yako (more…)

UKURASA WA 21; Weka Vipaumbele Kwenye Maisha Yako.

By | January 21, 2015

Kuna mambo mengi sana ambayo unatamani kuyafanya kwenye maisha yako, ila kwa bahati mbaya sana huwezi kuyafanya yote. Huwezi kufanya mambo yote unayotamani kufanya kwa sababu kuu mbili; 1. Huna muda wa kuweza kuyafanya yote hayo, una masaa 24 tu kwa siku na bado una malengo ya kuyafanyia kazi. 2. (more…)

UKURASA WA 20; Geuza Changamoto Kuwa Fursa.

By | January 20, 2015

Changamoto au vikwazo unavyokutana navyo kwenye maisha vinaweza kukukatisha tamaa na vile vile vinaweza kuwa fursa nzuri ya wewe kufikia mafanikio. Hakuna kitu chochote kinachotokea kwenye maisha yako ambaho huwezi kukigeuza kuwa fursa nzuri ya wewe kupata mafanikio zaidi. SOMA; #HADITHI_FUNZO; Kikwazo Kinavyoweza Kugeuka Kuwa Fursa. Katika kila tatizo unalipata, (more…)

UKURASA WA 19; Ishi Leo..

By | January 19, 2015

Leo ndio siku pekee unayoweza kuifurahia.. Leo ndio siku pekee unayoweza kuiathiri.. Leo ndio siku pekee unayoweza kuibadili.. Na leo ndio siku pekee unayoweza kuchukua hatua ya kuboresha maisha yako. Cha kushangaza wengi hatuishi leo, tunapoteza muda wetu mzuri kwa kuishi jana na kuishi kesho. Unaishi jana pale ambapo unaendelea (more…)